Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Friday, November 28, 2014

ZIKIWA ZIMEBAKI SIKU CHACHE KUMALIZIKA KWA ZOEZI LA KUANDIKISHA WANANCHI KATIKA DAFTARI LA WAPIGA KURA - KWENYE UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014


ZOEZI LA KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUPIGA KURA KWA AJILI YA CHAGUZI ZA SERIKALI ZA MITAA - MANISPAA YA SINGIDA.

Baadhi ya wananchi wa mtaa wa Stesheni kata ya Utemini  - ndani ya manispaa ya Singida waliojitokeza leo katika kituo cha Sido kwa ajili ya kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura - kwa ajili ya kuchagua viongozi wa serikali za mitaa inayotarajiwa kufanyika mwezi Disemba mwaka huu (picha na Doris Meghji)




Bi Angelina Mwagoa Karani mwandikishaji wa daftari la kupiga kura Kituo cha SIDO kwa ajili ya wananchi wa mtaa wa Stesheni - Kata ya Utemini Manispaa ya Singida.(picha na Doris Meghji)



Kushoto ni Ally Mtinange Muna wakala wa CCM akiwa kwenye kituo cha kuandikisha wananchi kwenye daftari la kupigia kura ya kumchagua kiongozi wa serikali za mitaa kataika uchaguzi utakofanyika mwezi ujao lengo likiwa ni kufanya utambuzi wa wananchi wanaoishi mtaa wa Stesheni akiwa pamoja na Betha Kawelega mwananchi wa mtaa huo wa stesheni aliyekuja kujiandikisha.(picha na Doris Meghji)


Ratiba ya siku za kujiandikisha katika zoezi hio la kujindikisha katika daftari la kupiga kura za kuchagua viongozi wa serikali za mitaa- unaotarajiwa kufanyika mwezi Disemba mwaka.(picha na Doris Meghji)


 Innocent Ahonga -karani wa waandikishaji wananchi kwenye daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa akimsainisha mmoja wa wananchi waliofika katika kituo cha shule ya msingi utemini - Mtaa wa Utemini kata ya Utemini -Manispaa ya Singida mara baada ya kumuandikisha jina lake.(picha na Doris Meghji)


Mmoja wa wananchi wa mtaa wa utemini aliyefika katika kituo cha shule ya msingi Utemini akisainishwa kwenye daftari la kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa kuchagua viongozi wa serikali za mitaa mara baada ya kujazwa taarifa yake  karani Innocent Ahonga wa kituo cha utemini mtaa wa utemin.(picha na Doris Meghji)


Kijana Innocent Ahonga akitoa maelezo juu ya changamoto mbali mbali zilizojitokeza katika zoezi hilo la uandikishaji wananchi kwenye daftrai la wapiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Disemba 2014.(picha na Doris Meghji)

Karani Ahonga amezitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na mwitikio mdogo wa wananchi kujitokeza kujiandikisha katika mtaa huo wa utemini hadi kufikia majra ya saa nane mchana leo ameandikisha jumla ya wanaanchi 180.

Suala mawakala wa vyama vya siasa limeonnekana ni changamoto nyingine katika utambuzi wa wananchi wa mtaa huo wa utemini hivyo katika kituo hicho  karani Ahonga ameandikisha wananchi hao kwa kuzingatia vitambulisho vya kupigia kura ili kumtambua mwananchi wa mtaa huo.

Ukiwa mwitikio bado ni mdogo hivyo ameshauri tabia ya kutoa elimu kwa umma kwa viongozi wa serikali za mitaa wapite na kuwahabarisha watu ili waweze kufika katika vituo vya kujiandikisha kupiga kura na wananchi mmoja kwa mmoja anyefika katika kituo hicho amuhabarishe na mwingine ili watu wafike kwenye kituo na kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura ili wafanye haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wao wa serikali za mitaa.

Kwa upande wake Angelina Mwagoa karani wa kito cha SIDO mtaa wa stesheni kata ya utemini amesema mkanganyiko wa wananchi kuja kujiandikisha kwa lengo la kupatiwa vitambulisho vya taifa limejitokeza kwa wananchi wa mtaa huo hivyo ametoa ushauri kwa manispaa kutoa tangazo na kuelimisha watu juu ya zoezi hilo ili watu waelewe na kujitokeza kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao

Kuhusu suala la malipo ya posho za makalani hao ndani ya manispaa ya Singida kwa malipo ya shilingi 10,000/= kwa siku  kiasi hicho cha malipo  kimeonekani ni changamoto kwa baadhi ya makarini wa uandikishaji wa daftari hilo ambapo hadi siku ya jana wamelipwa jumla ya shilingi 30,000/= tangu zoezi hilo lianze  siku Jumapili  tarehe 23 mwezi huu .

Zoezi hilo linatarajiwa kukamilika siku ya Jumamosi Novemba 29 mwaka huu majira ya saa 10:00 jioni.
MWISHO