Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Friday, January 16, 2015

MKUU WA MKOA WA SINGIDA AZIAGIZA SERIKALI ZA MITAA KUZITUMIA SHERIA NDOGO KATIKA KUHIFADHI MAZINGIRA MKOANI HUMU

Na, Doris Meghji  Ijumaa Januari 16,2015
Mkalama – Singida
Mkuu wa mkoa wa Singida Dr. Parseko Kone akipanda mti katika siku ya upandaji miti kimkoa katika shule ya Sekondari  Nkito wilaya ya Mkalama (Picha na Doris Meghji)

Mkuu wa  mkoa wa Singida Dr. Parseko Kone ameziagaiza  mamlaka za serikali za mitaa mkoani Singida kutumia sheria ndogo  walizojiwekea katika hifadhi ya mazingira ikiwa ni pamoja na utaratibu wa kupanda miti kumi kwa kwaya za vijijini na miti mitano kwa kaya za mijini kila mwaka usimamiwe kimamilifu ili kuikinga mkoa huo dhidi ya jangwa.



Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone akihutubia siku ya upandaji miti kimkoa katika shule ya sekondari ya Nkinto wilaya ya Mkalama (Picha na Doris Meghji)
Mkuu wa mkoa huyo ameziagiza mamlaka hizo za serikali za mitaa jana katika siku ya upandaji miti kimkoa  katika kijiji cha Nkinto halmashauri ya wilaya ya Mkalama inayoadhimishwa kila Januari kumi na tano mkoani hapa
Mmoja wa wananachi wa kijiji cha Nkinto akipanda mti katika siku ya upandaji miti kimkoa wilayani Mkalama (Picha na Doris Meghji)

Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkalama na wananchi na wakazi wa kijiji  Nkinto wakipanda miti katika shule ya sekondari Nkinto(Picha na Doris Meghji)
Aidha amesema katika kukabiliana na hali ya kuenea kwa jangwa ametaka hatua mbali mbali zichukuliwe na serikali kwa kuanzisha kampeni mbali mbali za upandaji miti mfano  ni kampeni ya Misitu ni Mali,Moto na Mazingira,uhamasishaji wa kila kaya kupanda miti isiopungua kumi na taasisi zenye matumizi makubwa ya miti zimeagizwa kuanzishwa mashamba yao ya miti,huku kuunda programu ya kukuza na kueneza misitu  Tanzania chini ya wizara ya maliasili na utalli na kushirikisha wananchi katika kuhifadhi uoto wa asili kupitia mradi wa PFM (Particpatory Forest Management)
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone akimwelekeza mwanafunzi wa shule a Msingi Nkinto kupanda mti kwenye siku ya upandaji miti kimkoa wilayani Mkalama (Picha na Doris Meghji)
Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa Dkt. Kone ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Singida kuifadhi uoto wa asili kwa kuwa  miti mingi wanayopanda inakufa hivyo amewaomba  watu binafsi na vijiji watenge maeneo ya hifadhi za misitu ya uoto wa asili kwa kuwa huota haraka. Ametoa wito wa hifadhi za misitu ya asili kutumika kwa shughuli za ufugaji nyuki,ili kuongeza kipato cha wananchi kutokana na zao hilo la asali.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone akitia msisitizo juu ya faida za misiti kwa wananchi wa kijiji cha Nkinto wilaya ya Mkalama mkoa wa Singida (picha na Doris Meghji)
Hata hivyo mkoa wa singida una jumla ya vijiji 230 vyenye misitu ya asili vya ukubwa wa hekta zipatazo  laki tano ishirini miatatu ishrini na tano nukta arobaini na tano (520,325.48)    
Afisa Maliasili Mkoa wa Singida Bwana Charles Kidua akitoa taarifa fupi ya upandaji miti siku ya upandaji miti kimkoa wilaani Mkalama(picha na Doris Meghji)
Awali afisa maliasili mkoa wa Singida Charles Kidua akisoma taarifa fupi ya siku ya upandaji miti kimkoa amezitaja mbinu mbali mbali ambazo idara ya maliasili mkoa wa singida imejipanga za upandaji miti ni kwa kila wilaya kutenga maeneo kwa ajili ya ukarabati kwa upandaji miti maeneo yaliyolengwa yasiyotumika kwa shughuli za kilimo kuanzia eka moja na kuendelea,wananchi wataweza  kushiriki katika upandaji na utunzaji wa miti na kutoa fursa ya elimu ya upandaji miti kwa jamii nzima.
Kamati a Ulinzi na usalama mkoa wa Singida kulia ni ACP Thobias Sedoyeka kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida,Katikati ni Agatha Komba mkuu wa magereza mkoa wa Singida na kamishna wa Uhamiaji mkoa wa Singida.( Picha na Doris Meghji)
Aidha kwa suala uhamasishaji amesema  suala la kuzihamasisha taasisi za kidini na zisizo za kiserikali kupanda miti angalau isiopungua mitano kwenye maeneo ya kuabudia na za kufanyia shughuli zao tayari viongozi wa taasisi hizo zimejulishwa huku mbinu ya kuanza kutoa  zawadi kwa taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali na  watu binafsi wanaopanda miti kwa wingi.
Katikati ni mkuu wa wilaya  ya Mkalama  Edward Ole   Lenga akifurahiya watumbuizaji katika siku hio ya upandaji miti kimkoa (picha na Doris Meghji)
Amesema pamoja na na upandaji miti unaenda sambamba na uhifadhi wa uoto wa asili uliopo amesma upandaji miti pekee hautoweza kupambambana na mabadiliko ya hali ya tabia nchi bila kuhifadhi uoto wa asili.hivyo mkoa umetomia njia shrikishi jamii katika kuhifadhi misitu ya asili iliyopo ambao ni misitu ya Mgori,Minunghe na Sekenke Tulya pia ukiwepo msitu wa watu binafsi mfano wa msitu wa Sombi katkika kijiji cha Msikii wenye hekta 40.
Dc Edward Ole Lenga kipanda mti katika siku ya upandaji miti kimkoa wilaani Mkalama katika kijiji cha Nkinto (picha na Doris Meghji)

Amesema licha ya juhudi hizo za kuhifadhi misitu ya asili wapo watu wachache wanataka kukwamisha juhudi hizo wakiwemo wahamiaji haramu katika msitu wa Minung’he na sehemu ya msitu wa Mgori.
Viongozi na baadhi ya wananchi wakichukuwa miti kwa ajili ya kupanda katika eneo la shule ya Sekondari ya Nkinto wilaya ya Mkalama (Picha na Doris Meghji)
Jumla miti mia tano arobani (540) imepandwa jana katika shule ya msingi Nkito wilayani Mkalama mkoa wa Singida na  kauli mbiu ya siku ya upandaji miti kitaifa ni MISITU NI UHAI;KATA MTI PANDA MITI” kauli mbiu ambayo mkuu wa mkoa wa Singida haijambaliki kwa kusema kata mti panda miti kwa kutaka kauli hiyo iwe panda miti kata tawi kwanini ukate mti.

MWISHO.





Wednesday, January 14, 2015

Chama Cha Mapinduzi (CCM) MAAZIMIO YA KAMATI KUU YA CCM -: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.






MAAZIMIO YA KAMATI KUU YA CCM -:
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Jana tarehe 13/01/2015 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa chini ya uongozi wa Mwenyekiti wake wa Taifa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete ilifanya kikao chake cha kawaida cha siku moja Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Pamoja na mambo mengine baadhi ya mambo yaliyojadiliwa na Kamati Kuu ni pamoja na:-
1. SAKATA LA AKAUNTI YA ESCROW.
Chama Cha Mapinduzi kimesikitishwa sana na sakata hili. Baada ya kulijadili kwa muda mrefu na kwa kina Kamati Kuu imeamua yafuatayo:-,
i). Pamoja na yale ambayo yameshatekelezwa na serikali, Kamati Kuu imeitaka serikali na vyombo vinavyohusika kuendelea kutekeleza maazimio ya bunge juu ya swala hilo.
ii). Kamati Kuu imewataka wote wanaopewa dhamana wajenge utamaduni wa kuwajibika kwa dhamana zao, na wasipowajibika waliowapa dhamana wachukue hatua za kuwawajibisha.
iii). Aidha Kamati Kuu imeiagiza Kamati Ndogo ya Maadili kuchukua hatua za kimaadili kwa wale wote waliohusika na ukiukwaji wa maadili kwenye sakata la Escrow na wako kwenye vikao vya maamuzi vya Chama. Kikao cha Kamati Ndogo ya Maadili kitafanyika tarehe 19/01/2015 kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo.
2. WALIOPEWA ADHABU KWA KUKIUKA MAADILI YA CHAMA.
Itakumbukwa kuna makada sita wa CCM walipewa adhabu kwa kuhusishwa na ukiukwaji wa maadili kwenye mchakato wa kutaka kuteuliwa na CCM kugombea urais, watamaliza muda wa adhabu zao mwezi wa pili mwaka 2015.
Baada ya muda wa adhabu zao kuisha, itafanyika tathimini kuona kama walizingatia mashariti ya adhabu zao. Na kama kuna ambao watakutwa hawakuzingatia mashariti ya adhabu zao wataongezewa adhabu.
3. SOKO LA MAHINDI.
Kamati Kuu imepokea taarifa ya mwenendo wa soko la mahindi nchini. Baada ya tathimini na uchambuzi, pamoja na kazi iliyofanywa na serikali, Kamati Kuu imeiagiza serikali kuangalia upya mfumo unaotumiwa na Hifadhi ya Taifa ya Chakula ( NFRA)katika ununuzi wa mahindi, ili unufaishe zaidi wakulima badala ya utaratibu wa sasa ambao kwa kiasi kikubwa unanufaisha zaidi mawakala badala ya wakulima moja kwa moja.
4. RATIBA YA VIKAO VYA CHAMA.
Kamati Kuu imepitisha ratiba ya shughuli mbalimbali za Chama kwa mwaka 2015.Aidha ratiba ya mchakato wa kuwapata wagombea wa CCM ndani ya dola utapangwa na vikao vijavyo vya Chama.
Nape Moses Nnauye
CCM Secretary for Ideology & Publicity.

Saturday, January 10, 2015

WANANCHI WA KATA A SANZA WALIA KWA KUKOSA MAWASILIANO YA MITANDAO YA SIMU LICHA YA WAO KUMILIKI SIMU ZA VIGANJANI - IMEFAHAMIKA

Na, Doris Meghji Ijumaa Janauri 09, 2015
Manyoni Singida.

Ukosefu wa mawasiliono miongoni mwa  wananchi wa kata ya Sanza,vijiji na vitongoji vyake imekuwa kero  kwa wananchi ya kata hiyo wilayani Manyoni
Shule ya msingi Sanza halmashauri ya wilaa ya Manyoni (Picha na Doris Meghji)


Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi wa kijiji cha Ikasi kata ya sanza wameziomba kampuni za simu nchini kuwekeza katika kata hiyo na vijiji vyao kwa kujenga minara ya mawasilino ili nao waweze kufurahia huduma kama ilivyo kwa maeneo mengine nchini.
Wananchi wa kata ya Sanza katika ofisi ya mtendaji wa kata hiyo (picha na Doris Meghji)

Kilio hicho cha kuhitaji huduma ya Mawasilino kinakuja pale wananchi hao wakipata shida ya kutunza siri zao za mawasiliono pindi wanapokutana eneo mmoja kwa ajili ya kupata mitandao ya mawasiliano eneo la umbali wa  kilomita mbili kutoka kijiji husika.
Mmoja wa wakina mama wa kata ya Sanza wakiwa na baadhi ya wazee wa kata hiyo katika ofisi ya Mtendaji kata ya Sanza(Picha na Doris Meghji)


Kwa mujibu wa sensa watu na makazi  kijiji hicho cha Ikasi kina wakazi takribani  elfu mbili na hamsini kikiwa ni kijiji kimoja kati ya vijiji vinne vinavounda kata ya sanza.
Baadhi ya wananchi wa kata ya sanza wakiwa kwenye ofisi a mtendaji wa kata hiyo na kilio chao cha kukusa mawasiliano ya mitandao ya Simu (picha na Doris Meghji)
Shughuli kuu ya kiuchumi kwa wananchi hao wa Sanza ni Kilimo cha ufuta,alizeti,mahindi na mtama.


Mwisho

Friday, January 2, 2015

DED - IRAMBA BI HALIMA HANJALI PETER ANUSURIKA KULIPULIWA NA BOMU NYUMBANI KWAKE LEO

Na, Doris Meghji Ijumaa Januari 02,2015
Singida

Kitu kinachodhaniwa ni bomu liliotengezwa kienyeji  kimeripuka leo majira ya saa 1:15 asubuhi na kusababisha madhara  eneo la kiomboi tarafa ya Kisiriri wilaya ya Iramba mkoani Singida
Kamanda wa jeshi la polisi  Mkoa wa Singida ACP Thobias Sedoyeka akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya Tukio hilo la mlipuko wa bomu .

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP THOBIAS SEDOYEKA amesema tukio hilo la mlipuko huo wa bomu  limetokea majira ya saa mmoja na dakika kumi na tano za asubuhi nyumbani kwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Iramba Bi Halima Hanjali Peter mwenye umri wa miaka 47  kwa kutoboa godoro la spring kiasi cha nusu nchi kwenda chini na upana wa nchi mbili.
Mwandishi wa habari Nathaniel Limu na afisa habari wa jeshi la polisi Shabani Msangi akiwa taari kumsikiliza kamanda wa jeshi la polisi kutoa taarifa kwa vyombo vya habari.(Picha na Doris Meghji)

Aidha amesema kitu hicho ambacho kilikuwa kimewekwa katika bahasha iliyopelekwa kwa Mkurugenzi huyo wa Iramba kutoka kwa katibu mhutasi wake  siku ya Jumanne tarehe 30 mwaka 2014 majira ya saa nne asubuhi ambapo ndani yake kulikuwa na kadi ya kumpongeza ambayo ilikuwa na kikaratasi chenye ujumbe uliosema “poleni sana hatuwezi kufanya dili la milioni tisini halafu mkala peke yenu sisi mkatudhulumu tukawaacha”

Waandishi wa habari wakipata taarifa toka kwa kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida.(Picha na Doris Meghji )


Kwa mujibu wa kamanda Sedoyeka amesema mkurugenzi huyo alipokuta ujumbe huo ,aliamua kwenda na bahasha hiyo nyumbani kwake bila kujua kuna kitu kingine ndani yake.hivyo ilivyofika siku ya tarehe mbili mwezi wa kwanza mwaka 2015 saa moja na robo asubuhi akiwa anajiandaa wakati ameiweka bahasha hiyo juu ya kitanda chake ili  kutoka nayo kitu kilichokuwa ndani ya bahasha hiyo kililipuka kwa kishindo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakipata kiburudisho cha soda ofisi ya kamanda wa po;isi mkoa wa Singida(picha na Doris Meghji)


Hata hivyo hakuna watu wanaoshikiliwa kwa tukio hilo na hakuna mtu aliyejeruhiwa isipokuwa kuchanika kwa gondoro na shuka lililokuwa limetandikwa katika godoro kitanda cha mkurugenzi huyo.

Jeshi la polisi kwa ushirikiano na wataalamu toka jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) na wataalam wa milipuko watafanya uchunguzi wa kitu hicho.

Jeshi la polisi linaendelea na upelelezi ili kumpata mtu aliyeitoa ile barua kwa hatua za uchunguzi zaidi.
MWISHO.





Friday, December 12, 2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - PATA TAARIFA JUU YA TEUZI ZA TAASISI ZA UMMA ALIZOFANYA MH.RAIS JAKAYA KIKWETE

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bi. Katarina Tengia Revocati kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani kuanzia tarehe 5 Desemba, 2014. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Desemba 11, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, imesema kabla ya uteuzi huo, Bi. Revocati alikuwa Msajili wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Biashara.

Vilevile katika Taarifa hiyo, Rais Kikwete pia amemteua Bwana Rugalema J. Kahyoza kuwa Msajili wa Mahakama Kuu kuanzia tarehe 5 Desemba, 2014. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Kahyoza alikuwa Hakimu Mwandamizi Msaidizi, Mahakama Kuu, Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Menejimenti na Mashauri.

Katika hatua nyingine, Rais Kikwete amemteua Dkt. Fidelice Mafumiko kuwa Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kuanzia tarehe 4 Desemba, 2014. Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Mafumiko alikuwa Naibu Mkuu TEWW.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu Dar es Salaam.
11 Desemba,2014

Tuesday, December 9, 2014

PITIA KURASA ZA MBELE NA NYUMA ZA MAGAZITI YA LEO TAREHE 09 DISEMBA 2014

PATA KURASA ZA MBELE NA NYUMA ZA MAGAZETI YA LEO TAREHE 09,DISEMBA 2014.



























 





NAKUTAKIA MIAKA 53 YA UHURU WA TANGANYIKA MWEMA MUNGU AWABARIKI WAPENDWA WTE WA KARIBU SINGIDA BLOGSPOT.

LEO TANZANIA BARA INAADHIMISHA NA KUSHEREHEKEA MIAKA 53 YA UHURU





Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiinua juu bango  likionyesha sasa Tanganyika Huru toka kwa mkoloni  mwaka 1961.



Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Baba wa Taifa letu akiwasili uwanja wa Uhuru jijini Dare- es salaam  mwaka 1961 akiungana na wananchi wa Tanganyika kusherehekea sikukuu ya Uhuru miaka 53 iliyopita.