Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Wednesday, January 29, 2014

MTAMA KUBADILI MAISHA YA WANANCHI WA MKOA WA SINGIDA KIUCHUMI


Na,Doris  Meghji Jumanne Januari 28,2014
Singida

Zao la mtama mkoani Singida linatarajiwa kuwa mkombozi kwa wananchi na wakulima wa mkoa huo kiuchumi.
Mkuu wa wilaya ya Singida Mwl. Queen Mulozi akiwa ofisini kwake jana(Picha na Doris Meghji)
Mkuu wa wailya ya Singida  Mwl. Queen Mulozi amebanisha kuwa  ukuombozi wa kiuchumi kwa wananchi wa mkoa  wa singida umekuja mara baada ya kampuni ya Bia Tanzania kuhitaji tani 700 ya zao la mtama kwa mwaka kwa lengo kutengeneza kinyaji hicho kwa kutumia zao hilo.

amesema “fursa imekuja ya zao la mtama kuwa zao la biashara, wakulima wakaze buti kuhakikisha tunajikita kwenye kilimo cha kuleta tija na kuondokana na umaskini” alisema mkuu huyo wa wilaya
aidha katika maandalizi ya kutekeleza mpango huo wa ulimaji wa zao la mtama wiliya ya singida na mkoa kwa ujumla umepanga kuanzisha mashamba ya bega kwa bega badala ya kuwa na shamba mmoja la mtama liwe hapa na lingine kule kwa lengo la kuwa karibu.
Mwl.Queen Mulozi Mkuu wa wilaya ya Singida (picha na Doris MeghjI)
Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya ya Singida amesema katika bajeti ya 2014/2015 kila halmashauri imeagizwa kununua mashine tano za kupura mtama likiwa ni agizo la mkuu wa mkoa wa Singida Dr. Parseko Kone ikiwa ni moja ya maandalizi ya kulima zao hilo kibiashara katika kusaidia mkulima kuzuia upotevu wa zao hilo nyakati za uvunaji na uhifadhi wa zao hilo

kwa mujibu wa mkuu huyo wa wilaya amesema baadhi ya mabenki ya CRDB na NMB mkoani singida yako tayari kukopesha wakulima fedha kwa ajili ya kununua mashine hizo hivyo kilimo hicho cha biashara cha zao hilo la mtama kinatarajiwa kuanza rasmi mwaka 2015.
Mkuu wa wilaya ya Singida Queen Mulozi akisisitiza jambo juu ya fursa ya soko la zao la mtama katika mkoa wa singida (picha na Doris Meghji)

Mwl Mulozi amewapongeza wananachi wa wilaya yake kwa jitihada walizozionyesha mwaka huu katika msimu wa kilimo amesema “hali inaridhisha ya msimu huu wa kilimo nimepita tarehe tisa mwezi januari na tarehe 12 mwezi januari nimejiridhisha kama mvua zitaendelea vizuri kunyesha hatutakuwa na shida ya upungufu wa chakula, maeneo ya kama Merya,Msange,Ukhandi,Makuro Ikhanoda hali ya kilomo cha mtama kiko vizuri.alisema mkuu huyo.
vitunguu ni mmoja ya zao la biashara liloanishwa katika kitabu cha muongozi cha kilimo na mifugo mkoa wa singida (picha na Doris Meghji)

Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi na wakulima wa wilaya yake kuendelea kulima mazao ya biashara na chakula yaliyoanishwa katika kitabu cha muongozo wa kilimo na mifugo cha mkoa wa singida kulingana na hali ya hewa ya mkoa huo kwa kulima mazao ya alizeti,vitunguu,pamba,uwele,mtama,mhogo,viazivitamu na zao la asali kupitia ufugaji nyuki kwa kutunza misitu katika maeneo yao.
mwisho



Tuesday, January 28, 2014

MAGAZETI LEO JANUARI 28,2014 yapo hapa

Kurasa za mwanzo na mwisho za magazeti ya Tanzania leo Januari 28,2014 yapo hapa kwa habari za nyumbani,kimataifa,udaku na michezo pitia hapa uperuzi


































Saturday, January 25, 2014

RUSHWA YA KILO 12 NA NUSI ZA NYAMA ZAMPANDISHA KIZIMBANI

Na Evarista Lucas
Singida
 Jan.24,2014
Afisa mifugo na mkaguzi wa nyama katika machinjio ya Mitunduruni manispaa ya Singida,Edwin Shangwel Mtae,amepandishwa  kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi mjini hapa;kwa tuhuma ya kupokea rushwa ya nyama ya ng'ombe kilo 12 na nusu.

Mwendesha  mashitaka  na mwanasheria wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoa wa Singida; Bwana Dominic Maganga, mbele ya hakimu Joyce Minde amedai kuwa ; mnamo Jeptemba 28 mwaka 2013,mtuhumiwa aliomba na kupokea rushwa ya nyama ya ng'ombe,yenye uzito wa kilo 12 na nusu  na yenye thamani ya  shilingi 62,500 za kitanzania.

Amesema kuwa; kitendo alichokifanya mtuhumiwa ni kinyume na kifungu cha 15 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa no.11/2007.
Maganga ameendelea kusema kuwa , kwa mujibu wa taarifa walizozipokea ofisini kwao ni kwamba ; mtuhumiwa Mtae alikuwa amejenga tabia sugu ya kuomba rushwa ya nyama za mifugo hususani maini,figo na moyo toka kwa wafanyabishara wa nyama; ambapo mfanyabiashara asiye kubalina na ombi hilo la rushwa ya nyama,alikuwa hawapi  kibali cha kuuza nyama ya mifugo.
Sanjari na hayo Maganga amesema; mnamo Septemba 28 mwaka 2013 majira ya asubuhi,mtuhumiwa aliwekewa mtego wa rushwa na kukamatwa na maafisa wa TAKUKURU wa mkoa wa Singida,akiwa amepokea rushwa ya nyama kiasi cha kilo 12 na nusu.
Kwa upande mwingine;mtuhumiwa Mtae amekanusha kutenda makosa hayo,na kesi yake inatarajiwa kutajwa tena februari sita mwaka huu; ambapo amefanikiwa kutekeleza masharti ya dhamana ambayo ni kuwa na wadhamini wawili wa ahadi ya shilingi laki tano kila mmoja.
MWISHO.

SIDO SINGIDA - YAWAASWA KUTUMIA MIKOPO YAO VIZURI

 Na Evarista Lucas
Jan 25,2013
Singida
 
 
MENEJA mikopo wa shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) mkoa wa Singida; Bwana Ruben Mwanja amewasihi wachukua mikopo ya SIDO kutoitumia vibaya mikopo hiyo kwa  kuongeza wake wengine au kuvunja ndoa za watu bali itumike  katika  kuendeleza biashara zao na kujiongezea kipato.

Mwanja ameyasema hayo mapema juzi wakati akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi mikopo mbalimbali yenye thamani ya shilingi milioni 18.9 za kitanzania kwa wanachama 39 wa kikundi cha Urafiki cha Singida mjini.

Amesema; uzoefu unaonyesha wazi kwamba baadhi ya wanawake wanaobahatika kupata mikopo,hukorofishanana au kutengana kabisa waume zao kwa ajili ya mikopo hiyo.
 
Licha ya hayo;Mwanja,amewataka wajasiriamali hao kutumia mikopo yao vizuri na kwa malengo yaliyokusudiwa,na pia mikopo hiyo isaidie kuimarisha ndoa zao. Amesema; wapo baadhi ya wanaume wakishapata mkopo wa kuendeleza biashara zao,hukimbilia kuoa mke mwingine.
 
Kwa upande wake meneja wa SIDO mkoa wa Singida Bwana Shoma Kibenda; amekipongeza kikundi cha Urafiki kutokana na sababu  kwamba kina utamaduni mzuri wa kurudisha mikopo kwa wakati na bila matatizo.
 
Kibenda amewataka wanakikundi hao wapige hatua zaidi kwa kuangalia uwezekano wa kuanzisha viwanda vidogo kama njia moja wapo ya kujiongezea kipato zaidi.
 
Katika hafla hiyo; Mikopo iliyotolewa  kima cha chini kilikuwa shilingi 300,000 na cha juu,kilikuwa ni shilingi 500,000 kwa mwanachama mmoja mmoja ambapo riba ya mikopo hiyo ni asilimia 1.8 kwa mwezi.
MWISHO.

Thursday, January 23, 2014

WIND BENEATH MY WINGS (Lyrics) - BETTE MIDLER

MAAFA - MVOMERO MVUA KUBWA YANYESHA JANA NA KUKATA MAWASILIANO.

Daraja la Dumila wilayani Mvomero likiwa limekatika baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha maafa mkoani Morogoro

Mafuriko yalivyosomba daraja hilo

Wasafiri wakiwa wamekwama kusafiri baada ya daraja kusombwa na maji.






Mvua kubwa iliyonyesha wilayani Mvomero, Morogoro usiku wa kuamkia jana imesababisha madhara makubwa ikiwemo kukatika kwa daraja la Dumila linalounganisha barabara za Morogoro na Dodoma na kusababisha watumiaji na wasafari wa barabara hiyo kukwama.

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS JANUARI 23, 2014 YAPO HAPA

Kurasa za mwanzo na mwisho za magazeti ya leo Januari 23, 2014 yapo hapa habari za kitaifa na kimataifa, Udaku na Michezo