Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Monday, June 30, 2014

TAARIFA ZAIDI JUU YA TARATIBU WA MAZISHI YA MWALIMU NKWABI NG'WANAKILALA






Habarini za leo. Kwa wale wana SAUT, napenda kuwafahamisha kuwa mwili wa mwalimu wetu mpendwa Nkwabi Ng'wanakilala utafika Dar leo jioni. Mazishi yatafanyika nyumbani kwake kesho tarehe Moja Kibamba CCM (kama unatoka Ubungo ni mkono wa kushoto, nimeelezwa kuwa ukiuliza tu Ng'wanakilala unaonyeshwa) kwa ibada itakayoanza saa Nne asubuhi. Karibuni tumsindikize mwalimu wetu katika safari yake ya mwisho hapa duniani.

R.I.P NKWABI NG'WANAKILALA MWALIMU WETU!

TASNIA YA HABARI INAZIDI KUPOTEZA WATU WA KUISAIDIA TASNIA  HIYO NCHINI KWELI  SAUT TUMEMPOTEZA MTU.APUMZIKE KWA AMANI .MINA.  


Karibu Singida blogspot.  inawapa pole wanahabari wote hasa wanafunzi  na  chuo cha Mt. Agustino kwa kumpoteza mwalimu Nkwabi Ng'wanakilala.Mwenyezi Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya Mwalimu wetu.

Tuesday, June 10, 2014

WATATU WAFARIKI DUNIA KATIKA KIJIJI CHA IRISYA TARAFA YA SEPUKA WILAYA YA IKUNGI

Na, Doris Meghji Jumanne Juni 10,2014
Singida

watu wawili wameuwa na wawili kujurehiwa kwa kukatwa katwa na kuchomwa na vitu vyenye ncha kali na watu wasiojulikana katika kijiji na kata ya Irisya Tarafa ya Sepuka wilaya ya Ikungi mkoani Singida

Kwa mujibu wa taarifa ya jana toka kwa Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Singida SACP Geofrey Kamwela amesema tukio hilo limegundulika Juni 08 majira ya saa mbili asubuhi ambapo miili ya watu wawili ambaye ni Musa Mkuki mwenye umri wa miaka 92 na mkwewe Tatu Sefu mwenye umri wa miaka 69 wote wakazi wa kijiji cha Irsya ilikutwa katika mazingira tofauti ambapo mwili wa mwanamke huyo ulikutwa nje ya nyumba yake ukiwa umelala chini na Mwili wa mwanaume wake ukiwa umelala kitandani ndani ya nyumba yao.


Katika tukio hilo majeruhi wawili Jasmini Idd mwenye umri wa miaka 17 mwanafunzi wa shule ya sekondari Gumanga ambaye alifariki dunia wakiwa anapatiawa matibabu katika zahanati ya kijiji cha Sepuka na mdogo wake Musa Nassor mwenye umri wa miaka 12 mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi Kisuluda wote wakiwa ni wajukuu wa familia hiyo ambaye kwa sasa amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Singida kwa matibabu zaida

Kwa mujibu wa jeshi hilo limesema uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa kubainika kwa kuuwa kwa watu hao ni baada ya majirani kuona mwili mmoja ukiwa nje na baadaye kufuatilia ndani ndipo walipogundua mwili mwengine wa marehemu pamoja na majeruhi hao wawili.

Aidha kwa uchunguzi wa daktari umeonyesha kuwa vifo hivyo vimetokana na kuvuja damu kwa wingi kutokana na majeraha waliopata

Hata hivyo chanzo cha mauji hayo bado hakijajulika hivyo jeshi la polisi linaendela na uchnguzi ikiwa ni pamoja na kuwatafuta waliohusika na mauji hayo.

Hivyo jeshi hilo linatowa wito kwa raia wema kushirikiana nalo bega kwa bega na kutoa taarifa zitakazosaidia kwabaini watuhumiwa waliofanya mauaji hayo.
MWISHO.