Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Tuesday, July 21, 2015

UCHAGUZI WA MADIWANI WA VITI MAALUM KWA TIKETI YA CCM KUFANYIKA KESHO WILAYA YA SINGIDA MJINI

Na, Doris Meghji  Jumanne Julai 21,2015
Singida
Bi Leah Samike akikabidhi fomu ya kugombea ubunge viti maalum kwa tiketi ya CCM kwa  kaimu katibu wa UWT  Singida Mjini bi Zaituni Mlau ( Picha na Doris Meghji)
Jumla ya wagombea 23 wa nafasi ya udiwani wa viti maalum kwa tiketi ya CCM wamejitokeza kugombea nafasi hiyo  jimbo la Singida mjini huku zikiwa  zimebaki saa kadhaa tu zoezi la upigaji kura wa uchagua madiwani sita kati ya idadi hiyo iliyojitokeza kufanyika.
Bi Leah Samike akikabidhi fomu ya kugombea ubunge viti maalum kwa tiketi ya CCM kwa  kaimu katibu wa UWT  Singida Mjini Bi Zaituni Mlau ( Picha na Doris Meghji)
Idadi hiyo ya wagombea wa udiwani viti maalum imetolewa na kaimu katibu wa UWT wilaya ya Singida mjini Bi Zaituni Mlau  wakati wa urudishaji wa fomu za kugombea nafasi hiyo Julai 19 katika ofisi za UWT wilaya ya Singida mjini
 Baadhiingida mjini  ya wagombea wa nafasi ya udiwani viti maalum kwa tiketi ya CCM wilaya ya Singida mjini wakirudisha fomu kwa kaimu Katibu wa UWT wilaya ya Singida mjini Bi Zaituni Mlau ( Picha na Doris Meghji)

Katika zoezi hilo la upigaji kura wa kuwachagua madiwani wa viti maalum unaotarajiwa kufanyika kesho katika ukumbi wa mikutano VETA ndani ya manispaa ya Singida, ni madiwani sita tu ndio wanaohitajika kuchaguliwa miongoni mwa wagombea hao 23 ambao ni wa tatu kutoka tarafa moja na watatu kutoka tarafa nyingi zinazounda jimbo la Singida mjini

 Hata hivyo jimbo la Singida mjini lina tarafa mbili, Tarafa ya Unyakumi na Tarafa ya Mungumaji zenye jumla kata 18 ambapo theluthi moja ya idadi ya kata hizo ndio idada ya madiwani wa viti maalum wanaohitajika  kuwakilisha wanawake katika baraza la madiwani wa manispaa ya Singida

kwa upande wa wabunge wa viti maalum ni wagombea watatu wa nafasi ya ubunge wa viti maalum kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi wamerudisha fomu katika ofisi ya CCM wilaya ya Singida mjini

Wagomba hao ni Aziza Awadhi Ntandu,Leah Willium Samike na Sophia Josephin Nkungu ndio waliojitokeza kuchukua fomu na kurudisha za ubunge viti maalum kupitia chama hicho.
Bi Leah Samike akikabidhi fomu ya kugombea ubunge  wa jimbo kwa tiketi ya CCM  ofisi za CCM  wilaya ya Singida Mjini ( Picha na Doris Meghji)

Kwa mujibu wa mmoja wa wagombea wao Bi Leah Willium Samike amewashauri wanawake na waandishi wa habari kujitokeza na kugombea nafasi hizo ili nao waweze kuwa nauwakilishi mkubwa kwenye nafasi hizo  za maamuzi.
Bi Leah Samike akikabidhi fomu ya kugombea ubunge wa jimbo la  CCM kwa  katibu wa CCM   Singida Mjini Bi  Magdalena Ndwete  ( Picha na Doris Meghji)

Leah Samike akiwa mmoja  ya wagombea na  mwandishi wa habari aliyejikita katika upigaji  picha za kihabari amesema lengo la kugombea nafasi hiyo ni kuwasadia wananchi wa jimbo la singida kuwa na hali nzuri kiuchumi kwa kuimarisha uwezo wao kichumi katika sekta ya kilimo kupitia zao la alizeti, kwa kuanzisha viwanda vitakavyokamua alizeti hiyo ambapo itabadilisha na kukuza pato la mkulima wa zao hilo jimboni Singida.
Leah Samike akiwa ofisi za CCM wilaya ya Singida mjini tayari kwa kurudisha fomu za ugombea wa nafasi ya ubunge wa jimbo Singida mjini ( Picha na Doris Meghji)

Hii ikiwa ni pamoja na kuendeleza michezo kwa kuanzisha timu za watoto wa miaka sita hadi 12 ikiwa ni kuendeleza na kukuza michezo kwa wananchi wa jimbo hilo na taifa kwa ujumla
Katibu wa CCM wilaya ya Singida mjini Magdalena Ndwete akipokea fomu toka kwa mgombea ubunge Bi Leah Samike katika ofisi ya CCM singida mjini (Picha na Doris Meghji)

Mgombea Samike amewashauri waandishi wa habari kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi hizo za uwalilishi ili nao waweze kupaza sauti katika masual na changamoto mbali mbali zinazo wakabili wananchi wa tasnia hiyo ya habari katika utekelezaji wa majumukumu yao nchini.
 
Bi Magdalena Ndwete Katibu wa CCM wilaya ya Singida Mjini akitoa maelezo juu ya wagombea waliojitokeza kuchukua fomu na kurudisha kwa wakati za nafasi ya ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Singida Mjini ( Picha na Doris Meghji)
Hapa nakutana na katibu Bi Magdalena Ndwete wa CCM wilaya ya Singida mjini ananijuza juu ya akina nani waliojitokeza kutia nia na kufanikiwa kurudisha fomu hizo za ugombea kwa wakati.
Dada zake Leah Samike akiwa ofisi za CCM wilaya ya Singida mjini tayari kwa  kumsindikiza ndugu yao kurudisha fomu za ugombea wa nafasi ya ubunge wa jimbo Singida mjini ( Picha na Doris Meghji)

Katika kutolea maelezo suala hilo katibu wa CCM  wilaya ya Singida mjini  anataja majina ya watia nia 8 waliojitokeza kuwania nafasi hiyo ambao ni Hassan Philipo Mazara, Mussa Ramadhan Sima,Aman Adrew Rai,Leah Willium Samike, Philemon Joseph Kihemi, Ammhed Mohamed Athuman, Rajab Juma Mrao na Juma Ahhmed Kidabu
Leah Samike akiingia  ofisi za CCM wilaya ya Singida mjini tayari kwa kurudisha fomu za ugombea wa nafasi ya ubunge wa jimbo Singida mjini ( Picha na Doris Meghji)

Katibu wa CCM wilaya ya Singida Mjini Bi Ndwete amesema ni wagombea saba tu ndio waliofanikiwa kurudisha fomu hizo za  nafasi hiyo ya ubunge jimbo la Singida mjini.
Bi Magdalena Ndwete Katibu wa CCM wilaya ya Singida Mjini akipokea fomu ya Mgombea Leah Samike aliyegombea ubunge Jimbo la Singida mjini  kwa tiketi ya CCM Picha na Doris Meghji)
Katibu Ndwete alisema baada ya wagombea hao kurudisha fomu watakaa kikao pamoja na kamati ya siasa ya wilaya ya singida  mjini ili kuwapa maelezo na maelekezo  ya zoezi la kampeni lifanyike kwa wagombea kutakiwa kutotoa lugha za matusi na za kupakana matope  wakati wa kufanya kampeni zao ndani ya jimbo hilo
Bi Magdalena Ndwete Katibu wa CCM wilaya ya Singida Mjini akitoa maelezo juu ya wagombea waliojitokeza kuchukua fomu na kurudisha kwa wakati za nafasi ya ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Singida Mjini ( Picha na Doris Meghji)

Hata hivyo kikao hicho kimepunguza kiwango cha fedha za uchangiaji wa gharama za uchaguzi kutoka milioni 5 kwa kila mgombea hadi kufikia milioni 2.5 katika uchaguzi huo.
Leah Solomon  akiwa ofisi za  UWT  wilaya ya Singida mjini tayari kwa kurudisha fomu za ugombea wa nafasi ya udiwani wa viti maalum wilaya ya  Singida mjini ( Picha na Doris Meghji)
Upigaji kura za  maoni  za kuwachagua  wagombea wa nafasi ya ubunge  kwa tiketi ya CCM wa jimbo na madiwani wa kata unatarajiwa kufanyika Agosti Mosi mwaka huu, huku Leah Samike akiwa mgombea pekee wa kike  amejitokeza kugombea nafasi hiyo kwa tiketi ya chama cha mapinduzi.
MWISHO.





Friday, July 17, 2015

UCHUKUAJI WA FOMU ZA KUGOMBEA UBUNGENA UDIWANI MIKOANI SINGIDA

Na, Doris Meghji Ijumaa 1jumaa Julai 17, 2015
Singida - Ugombeaji  Ubunge na udiwani
Bi Leah Solomon mgombea wa udiwani wa viti maalum akikabidhiwa fomu na kaimu katibu wa UWT wilaya ya Singida mjini Zaituni Mlau ofisi za jumuhiya hiyo ( Picha na Doris Meghji)

Wanachama  na makada wa chama cha Mapinduzi wamejitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kugombea nafasi za ubunge na udiwani mkoani Singida

Hii imejidhiirisha wazi leo siku ya pili tangu chama hicho kianze kugawa fomu kwa watia nia ngazi ya ubunge na udiwani  ambapo jimbo la singida mjini hadi muda majira ya saa tano asubuhi  huu ni watia nia watatu ngazi ya ubunge wa jimbo la Singida mjini ambao ni Hassan Philipo Mazara, Aman AP Rai na Mussa Ramadhan Sima hilo ni jimbo la Singida mjini
Bi Magdalena Ndwete katibu wa CCM wilaya ya Singida mjini akiwa ofisini kwa ajili ya utoaji wa fomu za kugombea nafasi ya ubunge jimbo la Singida mjini.( picha na Doris Meghji)

Aidha kwa upande wabunge viti maalum kwa jimbo la Singida  kaskazini  waliojitokeza kuchukua fomu ni Elizabeth Lucas Kitiku,Martha Nehemia Gwau na Aysharose Ndogholi Mattembe huku watia nia kwa nafasi ya udiwani viti maalum ni wanachama 17 wamejitoeza kuchukua fomu za kugombea nafasi hizo kwa chama cha mapinduzi jimbo la Singida kaskazi.
Bi Magdalena Ndwete katibu wa CCM wilaya ya Singida mjini akiwa ofisini kwa ajili ya utoaji wa fomu za kugombea nafasi ya ubunge jimbo la Singida mjini.( picha na Doris Meghji)
Kwa mujibu wa katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Singida mjini Bi Magdalena Ndwete ametaja idadi hiyo ya watia nia waliojitokeza kuchukua fomu ya nafasi ya ubunge jimbo la Singida mjini huku akiwawataka wanachama na makada wajitokeze kwa wingi kugombea nafasi hizo za uongozi kwa kuwa ni haki ya kila mwanachama kuchagua au kuchaguliwa katika kuwawakilisha wanachama  wenzao na wananchi katika ngazi za maamuzi.
Wagombea mbali mbali walofika kuchukua fomu za kugombea udiwani wa viti maalum wilaya ya Singida mjini katika ofisi ya UWT Singida mjini (Picha na Doris Meghji)

Zoezi hilo la uchukuaji wa fomu za kugombea nafasi ya ubunge kwa upande wa jimbo Singida mjini ni shilingi 100,000/= kwa wa ajili ya kulipia fomu huku hela ya mchango wa gharama za uchaguzi kuwa shilingi milioni tano (5,000,000/=) ambazo licha ya kamati ya siasa ya wilaya kupitisha kiasi hicho cha fedha kimeonekana kuwa kikwazo na tatizo kwa baadhi ya watia nia wasio kuwa na uwezo mkubwa kifedha  kugombea nafasi hiyo.
Zaituni Mlau kaimu Katibu UWT wilaya ya Singida mjini akimpatia fomu Janeth Nyakonji mmoja wa watia nia wa kugombea nafasi ya udiwani wa viti maalum Singida mjini ofisi za UWT wilaya ya Singida Mjini(Picha na Doris Meghji)

Katika kupata ufafanuzi juu ya mchango huo wa uchaguzi kutoka kwa katibu wa CCM wilaya ya Singida mjini amesema tuliache suala hilo la  kuchangia gharama za uchaguzi wa kuwa hadi sasa suala hilo ameiachia kamati ya siasa wilaya.
Zaituni Mlau kaimu Katibu UWT wilaya ya Singida mjini akikagua kadi ya mmoja wa wagombea wa udiwani Viti maalum jimbo la Singida mjini.(Picha na Doris Meghji)

Nao madiwani viti maalum wilaya ya Singida mjini zaidi ya watia nia kumi (10) wamejitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi hizo udiwani jimbo la singida mjini ambapo  Hadija Hassan Simba,Joyce John Sisha ,Mwandami Rajab Kunde, Hamida Amri Said, Anisa Awadhi Mbaraka, Mwanaidi Ally Njira,Mwahija Swalehe Abdalla, Mwajuma Husein Shaa,Leah  Solomon Lisu na Margareth Malecela wamejitokeza kuchukua fomu hizo za udwani viti maalum.
Kaimu katibu wa UWT wilaya yya Singida vijijini Amina Omary akigawa fomu za kugombea ubunge na udiwani viti maalum jimbo la Singida kaskazini  (Picha na Doris Meghji)

 kwa upande wa wilaya ya singida mjini ambapo uchangiji wake ni shilingi elfu kumi ya fomu (10,000/-) na uchangiaji wa gharama za uchaguzi kuwa shilingi laki mbili (200,000/-) kwa kila mtia nia wa kugombea nafasi hizo ya udiwani wa viti maalum.
Mmoja wa watia nia wa kugombea udiwani viti maalum jimbo la Singida kaskazi akijaza fomu ya kugombea nafasi hio katika ofisi ya UWT wilaya ya Singida vijijini (Picha na Doris Meghji)

Aidha kwa mujibu wa kaimu katibu wa UWT wilaya ya Singida mjini Bi Zaituni Hamis Mlau amesema katika zoezi amewaomba wanachama wa UWT kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi hizo za maamuzi jimboni humo.
Kaimu katibu wa UWT wilaya yya Singida vijijini Amina Omary akimwelekeza mmoja wa watia nia ya udiwani viti maalum jimbo la Singida kaskazini (Picha na Doris Meghji)

Bi Amina Omary Adam ni kaimu katibu wa UWT wilaya ya Singida vijijini ambapo jimbo la Singida Kaskazini linapatika ametaja gharama za watia nia ngazi ya udiwani viti maalum wilayani humo uwa ni shilingi 10,000/- kwa ajili ya fomu a kugombea nafasi na 200,000/- ni kwajili ya gharama za uchaguzu kwa wagombea wapya kwa nafasi hiyo huku wagombea wa udiwani wanaotetea nafasi zao kutakiwa kutoa elfu kumi ya fomu na kiasi cha shilingi 250,000/= kwa upande wa gharama za uchaguzi
Fomu ya kugombea nafasi ya ubunge na udiwani za CCM (Picha na Doris Meghji)

Hata hivyo katibu huyo Amina Omary Adamu amewaasa wanawake wajitokeze kwa wingi kuwania nafasi hizo za waamuzi kwa kuwa ni zama za kidemokrasia kuchagua na kuchaguliwa ikiwa ni haki ya kikatiba kwa chama hicho kuchagua na kuchaguliwa.
Zaituni Mlau kaimu katibu wa UWT wilaya ya Singida mjini akikagua kadi ya mtia nia aliyefika kuchukua fomu ya uchaguzi ( picha na Doris Meghji)
Wilaya ya singida vijijini ina jumla ya kata 21 zinazounda jimbo la singida kaskazini yenye tarafa tatu mkoani Singida
Utoaji wa fomu umeanza rasmi juzi Julai 15 na kutarajiwa kukamilika Jumapili  saa kumi kamili jioni Julai 19 mwaka huu

MWISHO.
  


Wednesday, July 15, 2015

MNARA WA 3G WA AIRTEL WAZINDULIWA RASMI - NKUNGI WILAYANI MKALAMA

Na, Doris Meghji Jumatano Julai 15,2015
Nkungi - Mkalama
MNARA WA 3G  WAAIRTEL ULIOZINDULIWA RASMI JULAI 12,2015 KIJIJI CHA NKUNGI WILAYANI MKALAMA (PICHA NA DORIS MEGHJI)
Wananchi na wakazi wa kijiji cha  Nkungi kata ya Mududa wilaya ya Mkalama  mkoani Singida wameombwa kutumia vizuri  fursa ya  uwepo wa mnara wa mawasiliano toka kampuni ya Airtel kwa  huduma za mawasiliano  na kiuchumi zinapatikana na kutolewa na kampuni hiyo  kwa maendeleo yao.
BAADHI YA WATEJA WA MTANDAO WA AIRTEL WAKIELEKEZWA KUJIUNGA NA MTANDAO HUO KIJIJINI NKUNGI WILAYA YA MKALAMA (PICHA NA DORIS MEGHJI0

Ombi hilo limetolewa na katibu tawala wa wilaya ya Mkalama  Benjamin Mwombeki  jana kijijini Nkungi katika uzinduzi rasmi wa mnara wa kampuni ya  mawasilino nchini   Airtel kwa kuwataka wananchi hao kutumia fursa  ya uwepo wa mnara huo kijijini hapo .
KATIKATI NI KATIBU TAWALA BENAJAMIN MWOMBEKI KUSHOTO NI VEO WA NKUNGI HUU KULIA NI MWENYEKITI WA SERIKALI YA KIJIJI CHA NKUNGI (PICHA NA DORIS MEGHJI)

Kwa upande wa mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Nkungi wilayani Mkalama Mohamed Idd Imbeve ametoa shukurani kwa kampuni hiyo kuweka mnara huo kijijini hapo na kuomba kampuni ya Aitrel kuboresha huduma ya Airtel Money ili kusadia watumiaji na wateja wa mtandao wa simu wa kampuni hiyo kijijini Nkungi.
MSHEREHESHAJI AKIWAELEKEZA WANANCHI WALIOFIKA MNADANI HAPO SIKU YA UZINDUZI RASMI WA MNARA WA 3G KIJIJINI NKUNGI (PICHA NA DORIS MEGHJI)

Awali akitoa maelezo kota kampuni hiyo ya Airtel kwenye uzinduzi  rasmi wa mnara huo  Mwakilishi wa Airtel toka Kanda ya kati Hendrick Werner ameomba serikali ya kijiji na wananchi kuutumia mnara huo katika nyaja ya mawasiliano kiuchumi bila kuusau kuulinda mnara huo ili uweze kuwasidia kwenye shughuli hizo
BAADHI YA WATEJA WAKIUNGANISHA NA HUDUMA MBALI MBALI KWENYE SIMU NA LINE ZA MTANDAO WA AIRTEL KIJIJINI NKUNGI (PICHA NA DORIS MEGHJI)
Mnara huo umezinduliwa hapo wenye uwezo wa  3G wa kuhudumia wananchi wanaotumia huduma hiyo kijijini hapo huo ni mmoja kati ya minara miwili iliyojengwa na kampuni hiyo ya Simu kwenye wilaya ya mkalama ikiwa ni moja ya njia ya kusogeza huduma ya mawasilino ya Simu karibu na wananchi mkoani Singida.
NI WANACHAMA SIKU YA MNADA WAKIWA TAYARI KUCHINGA NYAMA KWA AJILI YA NAMA CHOMA SIKU HIYO YA UZINDUZI WA MNARA WA 3G KIJIJINI NKUGI (PICHA NA DORIS MEGHJI)
Katika uzinduzi huo jumla ya watumiaji 304 waliuganisha kwenye mtandao huo huku huduma mbali mbali za mtandao huo ziliuwa ziitolewa za kuunganishwa kwenye mtandao,uuzwaji wa simu za promosheni ikiwa pamoja na kuunganishwa huduma ya Aitel Money zimefanika kwenye uzinduzi huo.
MNADA UIENDELEA HUKU SHUGHULI ZA UZINDUZI ZIKIFANYAKA SIKU HIYO NKUNGI (PICHA NA DORIS MEGHJI)
kwa mujibu wa mtendaji na mwenyeiti wa kijiji hicho mnada huo kijijini Nkungi hufanyika kila tarehe 11 ya mwezi wilayani Mkalama.
Mwisho

ZOEZI LA UCHUKUAJI WA FOMU ZA KUGOMBEA NAFASI YA UDIWANI NA UBUNGE UMEANZA LEO NDANI YA CCM - SINGIDA

Na, Doris Meghji Jumatano Julai 15,015
Singida


Ugawaji  wa fomu za uchaguzi katika kugombea nafasi za  uwakilishi wa wananchi ngazi ya ubunge na udiwani umeanza leo ndani ya chama cha mapinduzi nchini
Hii ni fomu ya kugombea nafasi ya udiwani ubunge kwa chama cha mapinduzi (Picha na Doris Meghji)

Nikitembelea moja ya ofisi ya kata ya chama cha Mapinduzi ndani ya manispaa ya Singida  Kata ya Utemini nakutana na mmoja wa wagombea nafasi ya udiwani Bartazary Kimario akichukua fomu katika kugombea nafasi hiyo udiwani akiwa ni diwani anayeitetea nafasi yake.
Bartazary Kimario akijaza jina lake katika kitabu cha kujiorodhesha cha watia nia katika kugombea nafasi ya udiwani kata ya utemini leo ofisi za chama kata ya utemini (Picha na Doris Meghji)
Aidha katika kupata maelezo juu ya taratibu za kugombea nafasi hiyo katibu wa CCM kata ya Utemini Bi Mary Frank amesema kugombea nafasi hiyo ya udiwani jumla ya shilingi laki tano na elfu zinahitajika kutolewa na kila mtia nia wa  kugombea nafasi hiyo kwa kiasi cha shilingi elfu 10,000/= kwa ajili ya ada ya fomu huku shilingi  500,000/= ikiwa ni mchango wa kampeni ya uchaguzi ndani ya chama hicho.
Mary Frank Katibu wa CCM kata ya utemini akimkatia stakabadhi ya malipo ya fomu na mchango wa kampeni mtia nia ya kugombea nafasi ya udiwani Bartazary Kimario mara baada ya kufika kuchukua fomu ofisini hapo ( Picha na Doris Meghji)
Amesema kila mtia nia wa nafasi hio ya udiwani anatakiwa kuwa na wadhamini 25 wakiwa ni wanachama wa kawaida wa CCM kutakiwa kumdhamini mgombea wa nafasi hiyo.
Mary Frank katibu wa CCM ata ya utemini akimkabidhi fomu mtia nia Bartazary Kimario katika kugombea nafasi hiyo ndani ya CCM leo katika ofisi ya kata (picha na Doris Meghji)

Zoezi hilo la uchukuaji wa fomu hizo  limeanza leo  Julai 15 hadi Julai 19 saa kumi kamili jioni
Hii ni stakabadhi ya ada ya fomu ya kugombea nafasi ya udiwani  kwa tiketi ya CCM (Picha na Doris Meghji)

Hivyo amweataka wananchama na makada wa CCM kujitokeza kugombea nafasi hiyo kwa kuwa ni haki ya kila mwanachama hai  kikatiba wa kata hiyo.
Hii ni stakabadhi ya mchango wa kampeni ndani ya chama hicho katika ngazi ya nafasi ya udiwani (Picha na Doris Meghji)
Mary Frank Katibu wa CCM ata ya Utemini akikagua kadi ya uanachama wa ccm ya  mtia nia Bartazary Kimario mgombea wa nafasi ya udiwani  katika ofisi ya kata ya utemini leo mara baada ya kufika kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo ya udiwani (Picha na Doris Meghji)
Hata hivyo kata ya utemini ni moja kati ya kata 18 zinazounda jimbo la singida mjini mkoani hapa.
MWISHO.



CCM URAIS NA DKT JOHN POMBE MAGUFULI -

 Na, Doris Meghji Jumatano Julai 15,2015
Singida


Mgombea wa urais wa chama cha CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2015 Daktari John Pombe Joseph Magufuli ni mbunge wa jimbo la Chato lililoko mkoa wa Geita na ni waziri wa ujenzi wa Tanzania.

Mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwaomba wajumbe wa mkutano mkuu wa ccm kumtuma na yuko tayari kuwatumikia wanaccm na watanzania kwa ujumla mara baada ya kutangazwa kushinda katika kinyang’anyiro hicho ndani ya CCM.
Alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1959 wilayani Chato Mkoani Kagera.
Kielimu, daktari Magufuli ana Stashahada ya elimu ya sayansi akibobea kwenye masomo ya Kemia, Hisabati.
Mgombea huyo wa urais ana shahada ya umahiri wa Sayansi na shahada ya uzamivu ya kemia.
Aidha daktari Magufuli amewahi kufundisha katika shule ya sekondari Sengerema miaka ya themanini kisha akajiunga na mafunzo ya JKT .
Alizaliwa Oktoba 1959
Alipohitimu, daktari Magufuli na aliaanza kufanya kazi katika kiwanda cha ‘Nyanza Cooperative Union akiwa Mkemia kabla ya kuondoka hapo na kuwania ubunge.
Magufuli alianza mbio za ubunge mwaka 1995 katika jimbo la Chato na kushinda kisha akateuliwa na Rais Benjamin Mkapa kuwa naibu waziri wa Miundombinu.
Katika uchaguzi wa Mwaka wa 2000 pia aligombea ubunge na kushinda na Rais Mkapa akamteua kuwa Waziri wa miundombinu.
Alianza siasa mwaka 1995
Dkt. John Pombe Magufuli Mgombea urais CCM akiwa na Mgombea Mwenza Samia Sluu Hassan akitambulisha rasmi mbele ya wajumbe mara baada ya kumteua katika ushindi wa kuigombea nafasi ya urais mjini Dodoma
Katika uchaguzi wa mwaka 2005 daktari Magufuli aligombea ubunge kwa mara ya tatu na kupita bila kupingwa.
Rais Kikwete alimteua kuongoza wizara ya Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi na baadaye akamhamishia hadi wizara ya Mifugo na uvuvi. Mwaka 2010 alichaguliwa kuwa mbunge kwa mara ya nne na Rais Kikwete alimrudisha katika Wizara ya Miundombinu na ujenzi.
Daktari Magufuli anachukuliwa kuwa ni mwanasiasa mwenye msimamo thabiti, mchapa kazi na asiye yumbishwa au hata kufuata upepo wa kisaisa.
Anatambulika kuwa Mchapa kazi
Watanzaniania wanamkumbuka kwa usimamizi na ujenzi wa barabara na majengo thabiti.
Anakumbukwa kwa kuchukua hatua za kutoa amri za kubomolewa kwa majengo ya kifahari ambayo alihisi yalikiuka sheria za ujenzi.
Na alipokuwa waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Bwana John Magufuli alikwenda hadi bandari ya Dar-es-Salaam na kuizuia meli ya wachina iliyokuwa inashukiwa kufanya uvuvi haramu katika sehemu ya bahari ya Tanzania.
MWISHO


Wednesday, July 8, 2015

MOHAMED DEWJI- ATANGAZA RASMI LEO KUTOGOMBEA TENA NAFASI YA UBUNGE JIMBO LA SINGIDA MJINI.


Na, Doris Meghji Jumatano Julai 08,2015
Singida

Huyu ndiye Mohamed Dewji Mbunge wa jimbo la Singida Mjini akisalimiana na baadhi ya wanachi waliojitokeza katika viwanja vya Peoples ( Picha Doris Meghji)
Mbunge wa  Jimbo la Singida Mjini Mohamed Gulam Dewji ametangaz rasmi kutogombea tena nafasi ya ubunge katika kipindi hiki cha uchaguzi kutokana  na kuongezeka kwa majukumu katika shuguli zake.
Ni wakazi na wanachi wa jimbo la Singida mjini walivyojitokeza leo  viwanja vya peoples kumsikliliza Mbunge wao Mohamed Dewji akitangaza rasmi kutogombea nafasi hiyo ya ubunge mwaka huu ( Picha Doris Meghji)
Tamko hilo ametoa leo katika viwanja vya peoples ndani ya manispaa ya Singida mbele ya wananchi na wakazi wa jimbo kuwa kutogombea kwake hakuta badilisha dhamira yake ya dhati ya kuliendeleza jimbo, hivyo kupitia Mo Dewji foundation mambo mengi mazuri yatakuja.
Add captionNi wakazi na wanachi wa jimbo la Singida mjini walivyojitokeza leo  viwanja vya peoples kumsikliliza Mbunge wao Mohamed Dewji akitangaza rasmi kutogombea nafasi hiyo ya ubunge mwaka huu ( Picha Doris Meghji)
Mheshimiwa Dewji  amesema  atakuwa tayari bega kwa bega kufanya kazi na kumuuonga mkono kada yoyote atakeyeonyesha nia ya kugombea na  kuchaguliwa na chama cha mapinduzi kugombea nafasi hiyo ya ubunge jimboni Singida
Ni wakazi na wanachi wa jimbo la Singida mjini walivyojitokeza leo  viwanja vya peoples kumsikliliza Mbunge wao Mohamed Dewji akitangaza rasmi kutogombea nafasi hiyo ya ubunge mwaka huu ( Picha Doris Meghji)
Hata hivyo katika uongozi wake ameleta na kupigania maendeleo mbali mbali kwa jimbo hilo  hasa katika sekta ya Elimu  Maji  Afya na maendeleo ya jamii
Mohamed Dewji akihutubia wananchi na wakazi wa Singida ( Picha na Doris Meghji)
Mohamed Dewji amekuwa mbunge wa jimbo la Singida mjini toka mwaka 2005 hadi 2015
Katika kutangaza kutogombea nafasi hiyo kamleta Msanii maarufu Diamond Platnum kutumbuiza na kuzikonga nyoyo za wakazi na wananchi za jimbo katika viwanja hivyo vya peoles.
MWISHO