Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Friday, September 11, 2015

MGOMBEA URAIS EDWRD LOWASSA TOKA WA UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI ( UKAWA) KUTARAJIWA KESHO MKOANI SINGIDA KUFANYA KAMPENI YA KUOMBA RIDHAA YA KUONGOZA WATANZANI.

Na, Doris Meghji Ijumaa Septemba 11,2015
Singida
 
Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Mendeleo ( CHADEMA) Mkoa wa Singida  Shabani Limu akitoa taarifa kwa waandishi nwa habari juu ya ziara ya Kampeni ya Mgombea urais wa UKAWA kupitia tiketi ya CHADEMA  anayetarajiwa kufika  kesho mkoani Singida ( Picha na Doris Meghji)
MGOMBEA urais wa Umoja wa Katiba ya Wanachi (UKAWA)  Edward Lowasa, anatarajiwa kuwasili mkoani Singida, kesho  kwa ajili ya kuomba ridhaa ya wananchi  kumpa kura za kuwa raisi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba 25, mwaka huu.
 Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Mendeleo ( CHADEMA) Mkoa wa Singida   akiongea na waandishi wa habari waliofika ofisi kwake kutapa taarifa ya ziara ya Kampeni ya Mgombea urais wa UKAWA kupitia tiketi ya CHADEMA  mkoani Singida ( Picha na Doris Meghji)

Mgombea huyo ambaye atawasili na kupokelewa katika ngome kuu ya chama hicho Wilayani Ikungi, majira ya saa 8 mchana siku ya Jumamosi akitokea mkoani Dodoma.

Ujio wa mgombea huyo wa UKAWA toka Chama cha Demokrasia na Mandeleo ni kwa mujibu wa Mwenyekiti wa CHADEMA mkoani Singida  Shabani Limu, akitoa taarifa hiyo kuwa mgombea huyo pia atawanadi wabunge na madiwani  katika maeneo yao na kuongea na wananchi kwa  kunadi sera za chama hicho.
 
Shabani Limu Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Mendeleo ( CHADEMA) Mkoa wa Singida  Akifurahia jambo wakati akiongea na waandishi wa habari waliofika ofisi kwake kutapa taarifa ya ziara ya Kampeni ya Mgombea urais wa UKAWA kupitia tiketi ya CHADEMA  mkoani Singida ( Picha na Doris Meghji)
“Tumeona vyema aanzie kwenye ngome kuu yenye wapenzi wengi Ikungi, kwa kufanya mkutano mkubwa utakaohudhuriwa na wapenzi wa chama hicho watakaompokea mkoa mzima hapo.

Mwenyekiti  Limu amesema siku hiyohiyo atawasili Singida mjini saa 10 jioni katika viwanja vya Peoples’ na kufanya mkutano mkubwa wa kampeni  kwa kuongea na wananchi  wa jimbo la SINGIDA MJINI.

Majira ya saa 5 asubuhi, siku inayofuata atafanya mikutano kama hiyo Wilayani Singida vijijini katika kijiji cha Ilongero kilichopo jimbo la SINGIDA
Shabani Limu Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Mendeleo ( CHADEMA) Mkoa wa Singida  Akifurahia jambo wakati akiongea na waandishi wa habari waliofika ofisi kwake kutapa taarifa ya ziara ya Kampeni ya Mgombea urais wa UKAWA kupitia tiketi ya CHADEMA  mkoani Singida ( Picha na Doris Meghji)
KASKAZINI na jimbo la IRAMBA MASHARIKI katika mji mdogo IGUGUNO 5:30 hada saa saba mchana na hatimaye kumalizia wilayani Iramba jimbo la Iramba magharibi majira ya  8:30 hadi  9:30 adhuhuri
   
Akitoa taarifa hizo pia kwa niaba ya uongozi wa CHADEMA kanda ya kati, inayojumuisha mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida, ziara hiyo ni ya awamu ya kwanza, ambapo awamu ya pili atakuja mapema mwezi Oktoba Wilayani Manyoni katika majimbo ya Manyoni Mashariki na Magharibi.

Katika ziara hiyo ya siku 2,pamoja na mambo mengine, mgombea huyo atanadi sera na kufafanua ilani ya UKAWA inayounda umoja vyama vinne vya siasa hapa nchini.
“Lengo ni moja tu la kutaka wananchi wa Singida kubadili mwelekeo wa fikra za kung’ang’ania na kuipenda CCM yenye ilani zilizoimbwa bila kutekelezeka zaidi ya miaka 50 iliyopita.

Hata hivyo alipongeza wananchi hao kwa kuonyesha mabadiliko katika uchaguzi mkuu uliopita wa 2010  ambapo kati kata 136 zilizoko mkoani hapa wao walipata kata 5.

Huku uchaguzi wa serikali za mitaa ulipfanyika mwaka jana walipata vijiji 43 na vitongoji 260 wilayani Ikungi.

“Tulipata vijiji 43 kati ya vijiji 45 na vitongoji 260 kati ya 287 vilivyoko wilaya nzima ya Ikungi”

Na kuongeza kuwa” hivi vyote vinavyoshikiliwa na CHADEMA kutoka katika Jimbo la Mashariki lililo chini ya mwanasheria wa chama hicho Tundu Lissu.
Kutokana na hilo ametoa wito kwa kuwataka wananchi wote mkoani hapa kumlaki na kusikiliza sera zitazowahamasisha ili kusaidia kumchagua ili awaletee maendeleo.
MWISHO



Thursday, September 10, 2015

KAMPENI ZA WAGOMBEA URAIS ZAONGEZA PATO KWA VIJANA


Awila  Silla,  Singida

WAKATI wagombea wa vyama mbalimbali nchini, wakiendelea na kampeni za kuomba  kura kwa wananchi ili wawachague katika nafasi walizooomba kwenye maeneo yao,  baadhi ya vijana wametumia kampeni hizo kubuni miradi ya kuwaongezea kipato.

Sospeter Charles(22), aliyetokea Wilayani Manyoni na kuja mjini Singida,  ni mmoja wa aliyebuni mradi wa kuuza vitambulisho vinavyoonesha picha za wagombea wa urais na wagombea wao wenza,  akiuuza  mitaani na kwenye mikusanyiko ya mikutano yenye wafuasi wa wagombea hao wanakofanyia kampeni.

Mfano wa wagombea hao ni pamoja na John Magufuli anayegombea nafasi ya uraisi na mgombea mwenza Samia Suluhu Sahani kwa tiketi ya CCM na mgombea Uraisi Edward Lowasa na Juma Haji Duni ambaye ni mgombea mwenza kupitia tiketi ya vyama shirika vinavyounda Ukawa.

Akizungumza na Mwananchi kijana huyo  aliyenaswa na kamera kwenye harakati zake za kuuza vitambulisho hivyo, alisema amehamasika kufanya biashara hiyo baada ya tathimini yake na kugundua kuwa vitambulisho hivyo vinavuta hisia za wapenzi wa vyama hivyo.

“Nimeona hii ni habari ya mjini kwa sasa, wapenzi wa vyama hivyo wanahamisika sana, nikaona bora nijaribu kutafuta soko la wateja ili niwauzie vitambulisho katika msimu huu wa kampeni mtaani” alisema Sospeter ambaye ameamua kusitisha  biashara yake ya vinyago na kuamua kuuza vitambulisho hivyo.

Na kuongeza kuwa, nimeifurahia sana kwani ina faida ya chapuchapu isiyoumiza kichwa, labda sanasana ni kinachonishumbua ni kuzunguka tu mtaani.

Akielezea mafanikio ya biashara hiyo, Sospeter anasema wazo hilo amelianza juzi siku ya Jumamosi alipokuja mgombea  mwenza wa CCM Samia Suluhu ambaye  alianza kwa kujaribu .

“Sikuamini, kwani nilikuwa na elfu 30 kama mtaji,  nikanunua vitambulisho 20 mchanganyiko ambavyo  niliviuza kwenye mkusanyiko wa wapenzi wa CCM ambavyo viliisha vyote kwa bei ya elfu 2 kila kimoja

Anasema hata hivyo vitambulisho vyenye wateja wengi muda wote ni vya UKAWA tofauti na vile vya CCM amba vyo aliuza siku alipokuja mgombea wake tena baada ya shikilizo la kupewa  masharti na wapenzi wa chama hicho kuficha vile vya UKAWA ili kutoa fursa ya soko la wagombea wa CCM.
 
MWISHO