Na, Doris Meghji Ijumaa Septemba 11,2015
Singida
MGOMBEA urais wa Umoja wa Katiba ya Wanachi (UKAWA) Edward Lowasa, anatarajiwa kuwasili mkoani
Singida, kesho kwa ajili ya kuomba ridhaa
ya wananchi kumpa kura za kuwa raisi
katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba 25, mwaka huu.
Mgombea huyo ambaye atawasili na kupokelewa katika ngome kuu ya
chama hicho Wilayani Ikungi, majira ya saa 8 mchana siku ya Jumamosi akitokea
mkoani Dodoma.
Ujio wa mgombea huyo wa UKAWA toka Chama cha Demokrasia na
Mandeleo ni kwa mujibu wa Mwenyekiti wa CHADEMA mkoani Singida Shabani Limu, akitoa taarifa hiyo kuwa mgombea
huyo pia atawanadi wabunge na madiwani katika maeneo yao na kuongea na wananchi kwa kunadi
sera za chama hicho.
“Tumeona vyema aanzie kwenye ngome kuu yenye wapenzi wengi Ikungi,
kwa kufanya mkutano mkubwa utakaohudhuriwa na wapenzi wa chama hicho
watakaompokea mkoa mzima hapo.
Mwenyekiti Limu amesema
siku hiyohiyo atawasili Singida mjini saa 10 jioni katika viwanja vya Peoples’
na kufanya mkutano mkubwa wa kampeni kwa
kuongea na wananchi wa jimbo la SINGIDA
MJINI.
Majira ya saa 5 asubuhi, siku inayofuata atafanya mikutano kama
hiyo Wilayani Singida vijijini katika kijiji cha Ilongero kilichopo jimbo la SINGIDA
Akitoa taarifa hizo pia kwa niaba ya uongozi wa CHADEMA kanda ya
kati, inayojumuisha mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida, ziara hiyo ni ya
awamu ya kwanza, ambapo awamu ya pili atakuja mapema mwezi Oktoba Wilayani
Manyoni katika majimbo ya Manyoni Mashariki na Magharibi.
Katika ziara hiyo ya siku 2,pamoja na mambo mengine, mgombea huyo
atanadi sera na kufafanua ilani ya UKAWA inayounda umoja vyama vinne vya siasa
hapa nchini.
“Lengo ni moja tu la kutaka wananchi wa Singida kubadili mwelekeo
wa fikra za kung’ang’ania na kuipenda CCM yenye ilani zilizoimbwa bila
kutekelezeka zaidi ya miaka 50 iliyopita.
Hata hivyo alipongeza wananchi hao kwa kuonyesha mabadiliko katika
uchaguzi mkuu uliopita wa 2010 ambapo
kati kata 136 zilizoko mkoani hapa wao walipata kata 5.
Huku uchaguzi wa serikali za mitaa ulipfanyika mwaka jana walipata
vijiji 43 na vitongoji 260 wilayani Ikungi.
“Tulipata vijiji 43 kati ya vijiji 45 na vitongoji 260 kati ya 287
vilivyoko wilaya nzima ya Ikungi”
Na kuongeza kuwa” hivi vyote vinavyoshikiliwa na CHADEMA kutoka
katika Jimbo la Mashariki lililo chini ya mwanasheria wa chama hicho Tundu
Lissu.
Kutokana na hilo ametoa wito kwa kuwataka wananchi wote mkoani
hapa kumlaki na kusikiliza sera zitazowahamasisha ili kusaidia kumchagua ili
awaletee maendeleo.
MWISHO
No comments:
Post a Comment