Awila Silla, Singida
WAKATI wagombea wa vyama mbalimbali nchini, wakiendelea na kampeni
za kuomba kura kwa wananchi ili
wawachague katika nafasi walizooomba kwenye maeneo yao, baadhi ya vijana wametumia kampeni hizo kubuni
miradi ya kuwaongezea kipato.
Sospeter Charles(22), aliyetokea Wilayani Manyoni na kuja mjini
Singida, ni mmoja wa aliyebuni mradi wa
kuuza vitambulisho vinavyoonesha picha za wagombea wa urais na wagombea wao wenza,
akiuuza mitaani na kwenye mikusanyiko ya
mikutano yenye wafuasi wa wagombea hao wanakofanyia kampeni.
Mfano wa wagombea hao ni pamoja na John Magufuli anayegombea
nafasi ya uraisi na mgombea mwenza Samia Suluhu Sahani kwa tiketi ya CCM na mgombea Uraisi Edward Lowasa na Juma
Haji Duni ambaye ni mgombea mwenza kupitia tiketi ya vyama shirika vinavyounda Ukawa.
Akizungumza na Mwananchi kijana huyo aliyenaswa na kamera kwenye harakati zake za
kuuza vitambulisho hivyo, alisema amehamasika kufanya biashara hiyo baada ya tathimini
yake na kugundua kuwa vitambulisho hivyo vinavuta hisia za wapenzi wa vyama hivyo.
“Nimeona hii ni habari ya mjini kwa sasa, wapenzi wa vyama
hivyo wanahamisika sana, nikaona bora nijaribu kutafuta soko la wateja ili
niwauzie vitambulisho katika msimu huu wa kampeni mtaani” alisema Sospeter
ambaye ameamua kusitisha biashara yake
ya vinyago na kuamua kuuza vitambulisho hivyo.
Na kuongeza kuwa, nimeifurahia sana kwani ina faida ya
chapuchapu isiyoumiza kichwa, labda sanasana ni kinachonishumbua ni kuzunguka
tu mtaani.
Akielezea mafanikio ya biashara hiyo, Sospeter anasema wazo
hilo amelianza juzi siku ya Jumamosi alipokuja mgombea mwenza wa CCM Samia Suluhu ambaye alianza kwa kujaribu .
“Sikuamini, kwani nilikuwa na elfu 30 kama mtaji, nikanunua vitambulisho 20 mchanganyiko
ambavyo niliviuza kwenye mkusanyiko wa
wapenzi wa CCM ambavyo viliisha vyote kwa bei ya elfu 2 kila kimoja
Anasema hata hivyo vitambulisho vyenye wateja wengi muda
wote ni vya UKAWA tofauti na vile vya CCM amba vyo aliuza siku alipokuja
mgombea wake tena baada ya shikilizo la kupewa
masharti na wapenzi wa chama hicho kuficha vile vya UKAWA ili kutoa
fursa ya soko la wagombea wa CCM.
MWISHO
No comments:
Post a Comment