Na, Doris Meghji Ijumaa Tarehe 18,2015
Singida
Halmashauri za wilaya mkoani Singida
zimetakiwa kujipanga vizuri katika kuhakikisha tatizo la utoro wanafunzi na utoro wa reja reja wa walimu linakwisha
mkoani humo licha ya UFAULU KUONGEZEKA KWA ASILIMIA 10 ukilinganisha na mwaka
jana
akitoa moja ya azimio la kuhkikisha
utoro wa reja reja wa walimu linashughulikiwa Katibu wa idara ya utumishi ya
walimu mkoa wa Singida SAMWEL OLESAITABAU ameitaka sheria ya walimu na utumishi
wa walimu itumike.
Taarifa zaidi na Doris Meghji kutoka
Mkoani singida
Suala la utoro wa wanafunzi linaeonekana
bado ni tatizo kubwa ambapo wanafunzi 267 hawakuweza kufanya mtihani wa darasa
la saba mwaka huu hilo limejitokeza katika kikao hicho cha uchaguzi wa
wanafunzi kujiunga na kidato cha kwanza mwaka
kesho tatizo hilo linahitaji ushirikiano wa ngazi zote huku utoro wa
reja reje wa walimu ambao umeokana ni moja ya changamoto katika sekta hiyo nalo limewekewa azimio.
INSERT
SAMWEL OLESAITABAU
KATIBU WA IDARA YA UTUMISHI WA WALIMU
MKOA WA SINGIDA
Tiluganilwa Mayunga ni kaimu katibu
tawala mkoa wa singida anafungua kikao hicho kwa kusisistiza masuala mbali mbali
hasa katika kuendeleza sekta hiyo ya elimu
INSERT
TILUGANILWA MAYUNGA KAIMU KATIBU TAWALA MKOA WA SINGIDA.
Katika kikao hicho suala la ufaulu wa wanafunzi mwaka huu umeonekana kuongezaka
kutoka aslimia 48.0 hadi kufikia asillimi 58.41 ambapo jumla ya wanafunzi
22,928 walifanya mtihani huo kati ya hao ni wasichana ni 12,629 na wavulana
10,318 sawa na asilimi 98.7 kwa mkoa wa Singida
Hata hivyo katika kupanga matokeo hayo halmashauri ya wilaya ya mkalama imepongezwa kwa kupanda kwa kiwango cha ufaulu wake kutoka aslimia 25 ya mwaka jana 2014 hadi kufikia 43.2 mwaka huu.
Mwisho.