Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Sunday, December 20, 2015

AZIMIO LA WALIMU LA UTORO WA REJA REJA LA AZIMIWA - MKOANI SINGIDA



Na, Doris Meghji Ijumaa Tarehe 18,2015
Singida

Halmashauri za wilaya mkoani Singida zimetakiwa kujipanga vizuri katika kuhakikisha tatizo la utoro  wanafunzi na utoro wa reja reja wa walimu linakwisha mkoani humo licha ya UFAULU KUONGEZEKA KWA ASILIMIA 10 ukilinganisha na mwaka jana
akitoa moja ya azimio la kuhkikisha utoro wa reja reja wa walimu linashughulikiwa Katibu wa idara ya utumishi ya walimu mkoa wa Singida SAMWEL OLESAITABAU ameitaka sheria ya walimu na utumishi wa walimu itumike.

Taarifa zaidi na Doris Meghji kutoka Mkoani singida

Suala la utoro wa wanafunzi linaeonekana bado ni tatizo kubwa ambapo wanafunzi 267 hawakuweza kufanya mtihani wa darasa la saba mwaka huu hilo limejitokeza katika kikao hicho cha uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na kidato cha kwanza mwaka  kesho tatizo hilo linahitaji ushirikiano wa ngazi zote huku utoro wa reja reje wa walimu ambao umeokana ni moja ya changamoto katika sekta hiyo  nalo limewekewa azimio.
INSERT
SAMWEL OLESAITABAU
KATIBU WA IDARA YA UTUMISHI WA WALIMU MKOA WA SINGIDA

Tiluganilwa Mayunga ni kaimu katibu tawala mkoa wa singida anafungua kikao hicho kwa kusisistiza masuala mbali mbali hasa katika kuendeleza sekta hiyo ya elimu

INSERT
TILUGANILWA MAYUNGA KAIMU KATIBU TAWALA MKOA WA SINGIDA.

Katika kikao hicho suala la ufaulu  wa wanafunzi mwaka huu umeonekana kuongezaka kutoka aslimia 48.0 hadi kufikia asillimi 58.41 ambapo jumla ya wanafunzi 22,928 walifanya mtihani huo kati ya hao ni wasichana ni 12,629 na wavulana 10,318 sawa na asilimi 98.7 kwa mkoa wa Singida

Hata hivyo katika kupanga matokeo hayo halmashauri ya wilaya ya mkalama imepongezwa kwa kupanda kwa kiwango cha ufaulu wake kutoka aslimia 25 ya mwaka jana 2014 hadi kufikia 43.2 mwaka huu.

 Mwisho.

No comments:

Post a Comment