Na, Doris Meghji Jumatano Juni 04,2014
Singida
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt Pareseko
Kone ametoa wito kwa wananchi na wakazi wa mkoa wa Singida kujitokeza
kwa wingi katika maeneo yote ambayo mwenge wa Uhuru utapita yakiwemo
maeneo ya mapokezi na kukabidhiwa kwa Mwenge huo,kwa kuwa utakukuwa
na ujumbe maalum ikiwa ni pamoja na kuhimiza maendeleo katika maeneo
itakayoweka mawe ya msingi,kuzindua na kufungua miradi mbali mbali
mkoani Singida
Akiongea na waansishi wa habari jana
mkuu huyo wa mkoa wa Singida amesema mkoa wa singida unapokea leo
Majira ya Saa mbili Asubuhi Mwenge wa Uhuru kutoka mkoani Mbeya
katika kijiji cha Rungwa kata ya Rungwa Tarafa ya Itigi wilayani
Manyoni ambao utakimbimbizwa katika wilaya Sita za mkoa wa singida
kwa kipindi cha siku sita mkoani hapa
Aidha amesema jumla ya miradi sitini
itatembelewa ,kuzinduliwa,kufungua na kuweka mawe ya msingii
itakayohusu sekta za Elimu,Afya,Maji ,Barabara,Biashara,kilimo
Mifugo,Ushrika,Misitu na sekta Binafsi ambayo thamani yake itakuwa
zaidi ya shiling bilioni 5.9 itakapokamilaka.
Ujumbe wa mbio za mwenge mwaka huu ni
@KATIBA NI SHEREIA KUU YA NCHI' yenye kauli mbiu ya Jitokezi kupiga
kura ya Maoni tupate katiba Mpya'
Aidha kupitia ujumbe wa kudumu wa
Mwenye wa UHURU kuhusu mapambano dhidi ya UKWIMI mwaka 2014 ni “
Maambukizi Mapya ,Unyanyapaa na Vifo vitokanavyo na UKIMWI SIFURI
Huku katika suala la mapambano dhidi ya
Rushwa na madawa ya kulenvya kauli mbiu ni PALIPO NA RUSHWA HAKUNA
MAENDELEO na FURAHIA AFYA YAKO SIO DAWA ZA KULEVYA”
MWISHO.
No comments:
Post a Comment