Habarini za leo. Kwa wale wana SAUT, napenda kuwafahamisha kuwa mwili wa
mwalimu wetu mpendwa Nkwabi Ng'wanakilala utafika Dar leo jioni.
Mazishi yatafanyika nyumbani kwake kesho tarehe Moja Kibamba CCM (kama
unatoka Ubungo ni mkono wa kushoto, nimeelezwa kuwa ukiuliza tu
Ng'wanakilala unaonyeshwa) kwa ibada itakayoanza saa Nne asubuhi.
Karibuni tumsindikize mwalimu wetu katika safari yake ya mwisho hapa
duniani.
No comments:
Post a Comment