Na, Doris Meghji Jumanne
Juni 10,2014
Singida
watu wawili wameuwa na
wawili kujurehiwa kwa kukatwa katwa na kuchomwa na vitu vyenye ncha
kali na watu wasiojulikana katika kijiji na kata ya Irisya Tarafa ya
Sepuka wilaya ya Ikungi mkoani Singida
Kwa mujibu wa taarifa ya
jana toka kwa Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Singida SACP Geofrey
Kamwela amesema tukio hilo limegundulika Juni 08 majira ya saa
mbili asubuhi ambapo miili ya watu wawili ambaye ni Musa Mkuki
mwenye umri wa miaka 92 na mkwewe Tatu Sefu mwenye umri wa miaka 69
wote wakazi wa kijiji cha Irsya ilikutwa katika mazingira tofauti
ambapo mwili wa mwanamke huyo ulikutwa nje ya nyumba yake ukiwa
umelala chini na Mwili wa mwanaume wake ukiwa umelala kitandani ndani
ya nyumba yao.
Katika tukio hilo majeruhi
wawili Jasmini Idd mwenye umri wa miaka 17 mwanafunzi wa shule ya
sekondari Gumanga ambaye alifariki dunia wakiwa anapatiawa matibabu
katika zahanati ya kijiji cha Sepuka na mdogo wake Musa Nassor
mwenye umri wa miaka 12 mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi
Kisuluda wote wakiwa ni wajukuu wa familia hiyo ambaye kwa sasa
amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Singida kwa matibabu zaida
Kwa mujibu wa jeshi hilo
limesema uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa kubainika kwa kuuwa kwa
watu hao ni baada ya majirani kuona mwili mmoja ukiwa nje na baadaye
kufuatilia ndani ndipo walipogundua mwili mwengine wa marehemu pamoja
na majeruhi hao wawili.
Aidha kwa uchunguzi wa
daktari umeonyesha kuwa vifo hivyo vimetokana na kuvuja damu kwa
wingi kutokana na majeraha waliopata
Hata hivyo chanzo cha
mauji hayo bado hakijajulika hivyo jeshi la polisi linaendela na
uchnguzi ikiwa ni pamoja na kuwatafuta waliohusika na mauji
hayo.
Hivyo jeshi hilo linatowa wito kwa raia wema kushirikiana nalo
bega kwa bega na kutoa taarifa zitakazosaidia kwabaini watuhumiwa
waliofanya mauaji hayo.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment