Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Monday, August 31, 2015

WATUMIAJI WA BIDHAA NCHINI NDIO KICHOCHEO KIKUBWA CHA WAZALISHAJI WA BIDHAA HIZO KUHAIKISHA WANAUZA BIDHAA ZENYE ALAMA YA UBORA ULIOTHIBITISHA NA TBS - AFISA MASOKO MWANDAMIZI TOKA TBS AMETOA RAI HIYO MKOANI SINGIDA.

Na, Doris Meghji Jumatatu Agosti 31,2015
Singida
Ni baadhi ya wajasiriamali walioshiriki kwenye maonyesho hayo wakati wa wakimsubiri mgeni rasmi kuhutubia kwenye  uzinduzi na ufunguzi rasmi wa maonyesho hayo ya SIDO kanda ya kati mkoani Singida kwenye viwanja vya Peoples ( Picha na Doris Meghji)
Umuhimu wa kutumia bidhaa zenye  alama ya ubora uliothibitishwa  na shirika la viwango la taifa (TBS)  utasaidia zaidi wajasiliamali na wazalishaji wa bidhaa kuhakikisha wanauza bidhaa zao zenye alama ya ubora uliothibitshwa na shirika hilo.
 
Afisa masoko mwandamizi toka shirika la viwango la taifa (TBS)  Gladness Kaseka akitoa elimu kwa wananchi waliofika katika banda la maonyesho la TBS kwenye maonyesho ya SIDO kanda ya kati yaliohusisha wajasiriamali wadogo na wakatii mkoani Singida kwenye viwanja vya peoples ( Picha na Doris Meghji)
 Imeelezwa kuwa iwapo  wananchi au watumiaji wa bidhaa  wataelewa na kutambua umuhimu wa kutumia bidhaa zenye alama ya ubora uliothibitishwa na TBS kutasaidiwa  wajasiliamali wadogo na wakati kuzingatia  sheria,kanuni na taratibu za shirika la viwango nchini kwa kuhakisha bidhaa zao wamezisajili na kupewa alama ya bora toka  shirika hilo.
Beatrice Mmbaga mjasiriamali wa usindnikaji wa dagaa toka mkoani Mara Musoma akiongea na karibusingida.blogspot.com kwenye maonyesho ya SIDO kanda ya kati mkoani Singida kwenye viwanja vya Peoples ( Picha na Doris Meghji)
 Bi Gladness Kaseka afisa masoko mwandamizi wa shirika la viwango la Taifa ( TBS) ametoa wito huo kwa wananchi na watumuaji wa bidhaa  wa mkoa wa singida na taifa kwa ujumla  kutumia fursa hiyo ya kupata elimu kwenye Maonyesho ya SIDO  banda la TBS viwanja vya peoples ili kuelewa umuhimu wa kutumia bidhaa hizo katika kuwasaidia wajasilimali hao kuuza bidhaa zenye alama ya ubora uliotibitisha na TBS nchini.
Ni baadhi ya wajasiriamali wakimpokea Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone wakati wa ufunguzi rasmi wa maonyesho hayo ya SIDO kanda ya kati mkoani Singida kwenye viwanja vya Peoples ( Picha na Doris Meghji)
“hapa elimu zaidi ni kwa watumiaji wa bidhaa hawa wakielewa watakuwa wanauliza mbona hii bidhaa aina alama ya ubora? na soko la bidhaa zisozokuwa na alama hiyo ya TBS haitauzika sokoni, hii itawafanya wajasiliamali kuhakikisha wanauza bidhaa zao zenye alama ya ubora uliothibitisha na TBS  kwa sasa wanazalisha na kuuza  wakijua soko lipo atauuza tu.”alisema Bi Gladness Kaseka Afisa masoko huyo wa TBS.
Katika maonyesho hayo shirika hilo la viwango linatoa elemu juu ya utaratibu wa kupata alama ya ubora ya TBS.
Dkt. Parseko Kone Mkuu wa mkoa wa Singida mgeni rasmi katika  ufunguzi wa maeonyesho ya SIDO kanda ya kati akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la SIDO mkoani Singida kwenye viwanja vya Peoples ( Picha na Doris Meghji)
Kwa mujibu wa taarifa ya shirika hilo limetoa maelezo juu serikali hutenga fedha kila mwaka kwa ajili ya kuhudumia wajasiriamali wadogo na wakati pale wanapoomba bidhaa zao wanazozizalisha zithibitishwe ubora, kuwa kati yao wapo wanaosamehewa kulipa ada yoyote kwa sababu ya mitaji kuwa midogo hivyo ili kupata msamahaa huo mjasiliamali anatakiwa kupata barua ya uthibitisho toka ofisi ya SIDO iliyokaribu na chama cha wazalishaji kama vile TAFODA  ikiwa ni pamoja na taarifa fupi toka idara ya Afya iliyopo karibu na mahali  pa uzalishaji au cheti cha  mamlaka ya taifa ya chakula na dawa (TFDA)  kwa wazalishaji wa vyakula ikiwa ni pamoja na leseni ya biashara.
 
Beatrice Mmbaga Mjasiriamali mdogo wa kusindika dagaa toka mkoa wa mara Musoma akitoa maelezo yake juu ya changamoto ya kupata alama za uthibitisho wa ubora wa bidhaa toka TBS na vifungashio toka SIDO kunako mgarimu mlaji wa bidhaa zao kwa kuwa bei inakuwa kubwa kutokana na gharama hizo ( Picha na Doris Meghji)
Nao  baadhi ya wajasiriamali walioshiriki katika maonyesho hayo mjasiriamali Beatrice Mmbaga kutoka Musoma msindikaji wa dagaa ameeleza changamoto ya wao kuhusu jengo hasa katika suala la kupata alama hizo  za ubora toka TBS ni mpaka   kibali toka TFDA, hivyo ameimba SIDO iweze kuwapatia majengo  au vyumba kwa ajili ya wajasiriali hao kuwa na maeneo ya kuzalishia na kusindika bidhaa zao lengo la kuwawezesha wajasiriamali hao kupata alama hizo za ubora toka TBS ili waeze kukubalika katika soko la ndani na nje ya nchi.
 Bwana Henrick Mdede meneja masoko wa SIDO makao mkuu ya SIDO taifa akiongelea suala la changamoto za wajasiriamali kuhusu usogezwaji wa huduma karibu na wajasiriamali ikiwa ni pamoja na vifungashio kwenye  maonyesho ya SIDO kanda ya kati mkoani Singida kwenye viwanja vya Peoples ( Picha na Doris Meghji)
Katika kulitolea maelezo suala hilo la wajasiriamali Meneja Masoko toka SIDO makao makuu  Henrick L. Mdede amekiri wajasiriamali kuwa na changamoto nyingi hasa suala kusogeza huduma kwenye maeneo yao kwa kushirikiana na halmashauri za wilaya  nchini kwa ajili ya kujenga kongano mbali mbali za uzalishaji kwa wadogo huko wilayani
amesema wilaya nyingi zimeweza kutoa maeneo mbali mbali,
Ni baadhi ya wajasiriamali walioshiriki kwenye maonyesho hayo wakati wa wakimsubiri mgeni rasmi kuhutubia kwenye  uzinduzi rasmi wa maonyesho hayo ya SIDO kanda ya kati mkoani Singida kwenye viwanja vya Peoples ( Picha na Doris Meghji)
  suala la ufinyu wa bajeti limeokena kuwa ni moja ya changamoto kubwa hasa ufinyi wa bajeti  ya serikali kwa shirika hilo la kuhudumia viwanda vidogo vidogo (SIDO)  kupitia wizara ya viwanda na biashara  kuhusu suala fedha ya kulipia upimaji wa ardhi kwenye viwanja au maeneo, kulipa fidia kwenye viwanja hivyo kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya kongano  za uzalishaji wa bidhaa kwa wajasiliamali wagodo wanaozalisha bidhaa hizo imekuwa ni tatizo katika utatuzi wa changamoto hiyo nchini.
Ni mjasiriamali Bi Beatrice Mmbaga toka Musoma Msindikaji wa dagaa akiongea na karibu Singida Blogspot kwenye maonyesho hayo ya SIDO kanda ya kati akielezea juu ya changamotozo zinazowakabili juu ya suala la vifungashio vya bidhaa zao hasa katika kupata soko la uhakika ndani na nje ya nchi ndani viwanja vya Peoples leo  ( Picha na Doris Meghji)
Huku suala la vifungashio ameiomba serikali kuwavutia wawekezaji wengi kuwekeza kwenye viwanda kwa kufufua viwanda na kuanzisha viwanda vipya nchini ili kulitatua tatizo hilo ambalo kwa sasa vifungashio huagizwa nje ya nchi hali ambayo umuumiza mlaji na mtumiaji wa bidhaa hizo nchini.
Ni baadhi ya wajasiriamali wakimpokea Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone wakati wa uzinduzi rasmi wa maonyesho hayo ya SIDO kanda ya kati mkoani Singida kwenye viwanja vya Peoples ( Picha na Doris Meghji)
Maonyesho hayo ya SIDO kanda ya kati ambayo wajasiriamali 205 wamefanikiwa kushiriki toka mikoa kumi (10) kati mikoa hio ni mkoa wa Dodoma, Kigoma,Singida,Shinyanga na Tabora ndio mikoa inayounda SIDO kanda ya kati nchini.
MWISHO.


No comments:

Post a Comment