TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bi. Katarina Tengia Revocati kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani kuanzia tarehe 5 Desemba, 2014. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Desemba 11, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, imesema kabla ya uteuzi huo, Bi. Revocati alikuwa Msajili wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Biashara.
Vilevile katika Taarifa hiyo, Rais Kikwete pia amemteua Bwana Rugalema J. Kahyoza kuwa Msajili wa Mahakama Kuu kuanzia tarehe 5 Desemba, 2014. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Kahyoza alikuwa Hakimu Mwandamizi Msaidizi, Mahakama Kuu, Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Menejimenti na Mashauri.
Katika hatua nyingine, Rais Kikwete amemteua Dkt. Fidelice Mafumiko kuwa Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kuanzia tarehe 4 Desemba, 2014. Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Mafumiko alikuwa Naibu Mkuu TEWW.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu Dar es Salaam.
11 Desemba,2014
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu Dar es Salaam.
11 Desemba,2014