Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Thursday, May 15, 2014

WMA - NA ZOEZI LA KAMATA KAMATA BIDHAA ZISIZO KATIKA VIFUNGASHIO NA VIPIMO HALISI - NDANI YA MANISPAA YA SINGIDA

Na, Doris Meghji Alhamis Mei 15,2014
Singida

Baadhi ya wajasiliamali ndani ya Manispaa ya Singida wameshikiriwa bidhaa zao na wakala wa vipimo (WMA) mkoa wa Singida ikiwa ni mmoja ya jitihada za wakala hiyo kuhakikisha wajasiliamali na wafanyabiashara wanatumia vipimo halisi na vifungashio vinavyofaa kwa bidhaa husika

Zoezi hilo limewakumba  baadhi ya wajasiliamali waliojikita katika biashara ya mafuta ya alizeti yaliokuwa yamefungashwa katika chupa za maji ya kunywa  na sio vifungashio vinavyoonyesha taarifa sahiihi za bidhaa hizo ikiwa ni pamoja na kipimo halisi.

Wakiongea kwa nyakati tofauti katika ofisi za wakala wa vipimo wajasiliamali hao ambao ni Esta na Feslista wamemuomba kusamehewa na wakala wa vipimo  kwa kutakiwa kulipa faini ya laki mmoja kila mmoja kwa kuwa hawakujua kama wamevunja sheria ya vipimo kwa kuuza mafuta hayo ya alizeti katika vifungashio ya chupa za maji ya kunywa

wamejieleza kuwa wao ni wajasiliamasali na biashara hiyo huifanya kwa kukupa ili kuweza kujikimu kimaisha, na sasa wamekwisha elewa juu ya sheria hiyo ya vipimo na kuahidi kufuata sheria ingawa ghalama za vifungashio kwao zitaawagharimu katika uendeshaji wa biashara hiyo.


Katika kutaka kujua juu ya zoezi hilo ambalo wakala wa vipimo imeanza kulifanya ndani ya manispaa ya Singida mmoja watumishi wa wakala hiyo alisema mmesmaji wa ofis hiyo atakuwepo kesho kwa mahojiano zaidi.

Hata hivyo mamlaka hiyo inatekeleza wajibu wake katika kuhakikisha wanasimamia vyema masuala la vipimo halisi ikiwa ni pamoja na vifungashio likiwa ni mmoja ya ombi toka shirikikisho la vyama huru vya wafanyakazi kwenye sherehe za Mei Mosi mwaka huu lengo ikiwa ni kutowapunja wakulima hasa katika ufungashaji wa lumbesa kwenye bidhaa za mazao ya wakulima.

MWISHO

Friday, May 9, 2014

MEDIA DAY - NA WALEMAVU



 MEDIA DAY - NA WALEMAVU Na, Doris Meghji Ijumaa Mei 09 2014
 Singida

Shule ya Msingi Ikungi mchanganyiko ni moja kati ya shule zenye kuhudumia wanafunzi  wasio na ulemavu na wenye Ulemamvu  wilaya ya Ikingu Mkoani Singida Ikiwa ni siku ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa habari Duniani inayoadhimishwa kila mwaka  Mei  03 Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Singida imeamua kuadhimisha siku   kwa kuitembelea shule ya Msingi Ikungi Mchanganyiko kwa kutoa msaada wa vifaa na chakula ikiwa ni moja ya jitihada ya kuuunga mkono juhudi za serikali katika kumwendeleza mtoto mwenye ulemavu nchini.

 Mwenyekiti wa klabu za waandishi wa habari mkoa wa Singida Seif Takaza akiongoza jobo hilo la waandishi wa habari wa mkoa huo amesema licha ya changamoto sekta ya habari nchini wajibu na jukumu la wanahabari ni kuleta maendeleo kwa jamii hivyo klabu hiyo imeazimia kwa dhati kushirikiana na wanafunzi hao wa shule hiyo kwa kuwapatia misaada mbali mbali ya kibinadamu na kutoa fursa kwao kupaza sauti zao kupitia vyombo vya Habari juu ya changamoto wanazokumbana nazo

Aidha amesema jukumu la kuhabarisha ,kufichua,kuonya na kuelimisha jamii juu ya aina yoyote ya ukatili na unyanyapaa wanaofanyiwa watu wenye ulemavu kwa kuandika habari hizo na kuzitangaza  klabu hiyo itaendelea kupaza sauti katika kupinga ukatilii na unyanaya paa wa aina yoyote wanaofanyiwa watu wenye ulemavu. Hivyo klabu hiyo imetoa msaada wa vifaa na vyakula vyenye thamani ya shiling 804,000/= ambavyo ni sahani za plastiki 30 , vikombe vya plastiki 30, ndoo ndogo  5, kilo 100 za unga wa sembe, kilo 150 za mchele,kilo 25 za unga wa ngano,kilo 50 za sukari huku madaftari 300,kalamu 150, majani ya chai katoni  1, mafuta ya kula lita 40 na maharagwe madebe 2 ikiwa ni mchango wao katika kuisaidia jamii hiyo ya walemavu kwenye kuadhimisha siku hiyo ya uhuru wa habari duniani ambayo kitaifa imefanyika  Jumamosi Mei 03 jijini Arusha mwaka huu.

Naye mwalimu mkuu wa shule ya Ikungi mchanganyiko Olvery Tamilly ameishukuru klabu ya wanahabari wa mkoa wa Singida kwa  kuwakumbuka  watoto wenye ulemavu kwa kusherekea siku hiyo ya uhuru wa habari duniani na watoto wenye ulemavu.

 Aidha katika taarifa fupi ya shule hiyo ya Ikungi mchanganyiko Mkuu wa shule hiyo amezitaja changamoto mbali mbali zinazoikabii shule hiyo ya Ikungi mchanganyiko kuwa ni kukosekana kwa mafuta maalum ya ngozi kwa wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi,upatikanaji wa maji ya uhakika katika mazingira ya shule ,ukosefu wa kompyuta maalum kwa wanafunzi wenye ulemavu wa macho ili  kwenda na mfumo wa mawasiliano licha ya kuwa na mwalimu mtaalam mmoja wa kuwafunza jinsi ya utumiaji wa kopyuta hzio bila shida kwa mujibu wa mwl. Tamilly

ameleza kuwa changamoto nyingine ni kutoka kwa baadhi ya wazazi na walezi wa watoto hao wenye ulemavu kuwatelekeza watoto hao mara baada ya kuwepeleka shuleni hapo

 hivyo amewaaomba wazazi na walezi wa watoto kuja kufuatilia maendeleo ya watoto hao kwa kuwa watoto wenye ulemavu sana na watoto wasio na ulemavu  Aidha katika kuendesha shule hiyo 
amsema  shule ina utaratibu wa kuanza na tiba kabla ya kumuanzishia mafunzo mtoto, hivyo uendeshaji wa kituo hicho hutegemea zaidi uwezeshaji wa toka serikali kuu na wafadhili kama chama cha wasiona Tanzania (TLB) na WFP Hata hiyvo mwalimu huyo ameiomba jamii kuitumia shule hiyo kwa kuwapeleka watoto wenye ulemavu ili waweze kuendeleza na sio kuwawaficha majumbani kwao kuwa watoto wenye ulemavu nisawa na watoto wasio na ulemavu

Katika kutembelea baadhi ya  wanafunzi hao kwenye madarasa hayo msaada wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia vinahitajika kwa wananfunzi hao wenye ulemavu ikiwa ni lenzi la kusomea kwa watoto wenye uoni hafifu,mashine au vifaa vya kuandikia vya nukta nundu kwa watoto wasiona,huku na mafuta maalum kwa walemavu ya ngozi yanayowasaidia kujikinga na mionzi ya jua kuku mavazi ya mikono mirefu,kofia za kuwawezesha kufunika kichwa na masikio ili kujikinga na miale ya jua.

 Shule hiyo ya Ikungi Mchanganyiko imechukua wanafunzi 1200 ambapo wanafunzi 104 ndio wenye ulemavu mbali mbali ikiwemo alibinisim 44,wasiona 58 na wene ulemavu wa vinungo 02 na wasio na ulemavu 96. Hata hivyo shule ya Ikungi Mchanganyiko ni umbali wa kilomita 36 kutoka Manispaa ya Singida ilianza kupokea rasmi wanafunzi wenye ulemavu mchanganiko mwaka 1980 kutoka singida mjini hivi sasa shule hio inapokea wanafunzi mbali mbali wenye  ulemavu kutoka maeneo mbali mbali ya nchi. Katika kuadhimisha siku ya uhuru wa habari duniani kauli mbiu mwaka huu ni 
 HABARI NI CHACHU YA MAENDELEO YENYE LENGO LA KUKUZA DEMOKRASIA KWA MTU BINAFSI,JAMII NA TAIFA KWA UJUMLA"
mwisho  


  

Wednesday, May 7, 2014

WAWILI WAFAFRIKI DUNIA KUTOKANA AJALI MBALI MBALI MKOA WA SINGIDA

Na,Doris Meghji Jumane  Mei 06,2014
Singida

Mtoto mwenye umri wa miaka miwili afariki dunia juzi mara baada ya kuzama ndani ya karo la maji liliopo kwenye kiwanja jirani na nyumbani kwao eneo la Mwantanda  Kata ya Mandewa  Manispaa ya Singida

Taarifa hiyo kwa waandishi wa habari toka kwa Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Singida SACP Geofrey Kamwela imeleza kifo cha mtoto  aitwae Silvester Elias  kimemfika akiwa anacheza na watoto wenzake ambapo mtoto huyo alipanda ukuta uliozungushiwa karo  lenye  urefu wa futi  mbili kutoka usawa wa ardhi na kuteleza kisha kutumbukia kwenye karo liliojengwa   la kuhifadhia maji kwa ajili ya matumizi ya shuguli za ujenzi lenye kina cha futi 8.

Aidha kwa Mujibu wa taarifa hiyo toka kwa kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida imesema hakuna mtu au watu waliokamatwa kutokana na tukio hilo na jeshi hilo linaendelea na uchunguzi.

 Wakati huo huo mtu mmoja afariki dunia na Mwingine kujeruhiwa kutoka na ajali ya gari  lenye shehena ya mafuta lenye usajiri namba T467 BAG /T 478 BAG  aina IVECO  likiendeshwa na dereva Faustine Augustino Mkazi wa mwanza  mara  baada ya kuacha njia na kupinduka  jana majira ya saa tisa na nusu mchana  eneo la mlima Sekenke barabara ya Singida Igunga  kata ya Ulemo wilaya ya Iramba mkoa wa Singida

kwa mujibu wa Kamanda Kamwela amesema  gari hilo liloluwa limebeba sehena ya mafuta ya taa   liliacha njia na kupindika na kusababisha kifo cha mtu mmoja aitwaye Latipha Shabani anayekadiriwa kuwa na umri wa mika 38 mkazi wa kipawa  - Dar es salaam ambaye alikuwa abiria katika gari hilo  huku dereva wa gari hilo akiwa amejeruhiwa kichwani na
kulazwa katika hospitali ya wilaya ya  Igunga mkoani Tabaora

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Kiomboni wilaya ya Iramba mkoa wa Singida

Jeshi hilo la polisi linafanya uchunguzi kuhusu chanzo cha ajali hiyo na dereva wa gari hilo anashikiliwa na posili kwa uchunguzi zaidi.

Hivyo jeshi hilo la polisi linatoa wito kwa madereva wa magari yote wanaopita  mkoani Singida kutoka mikoa mingine au nje ya nchi kuwa makini hususani wafikapo maeneo ya mlima na mteremko

DC SINGIDA MWL. QUEEN MULOZI AAGIZA VYUMBA VITATU VYA MAABARA KATIKA SEKONDARI ZA KATA KUKAMILIKA JUNI 15 MWAKA HUU

Na, Doris Meghji Jumatatu Mei 05, 2014
Singida



Mkuu wa wilaya ya Singda Mwl Queen Mulozi amewaagiza watendaji wa kata na waratibu wa elimu kata kuhakkisha wanakamilisha ujenzi wa vyumba vitatu  vya maabara  ifikapo Juni 15 mwaka huu.

Agizo hilo limetolewa leo  na Mkuu huyo wa wilaya ya Singida kwa watendaji wa kata na waratibu wa elimu kata ikiwa ni mmoja ya mpango wa  mkoa kuhakikisha ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara katika shule zote  sekondari za kata  mkoani Singida  zinakamilika mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu.

Aidha katka kutekeleza agizo hilo kwa watendaji wa kata  na waratibu wa elimu kata    kunatokana na michango toka wananchi hivyo mkuu wa wilaya huyo amewataka watendaji hao  wanakamilisha ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara  Juni 15 mwaka huu.

Kwa mujibu wa mmoja wa watendaji kata  afisa mtendaji wa kata Mtamaa Mohamed Kipamila amesema kwa upande wa manispaa ya Singida ni kata nne tu zilizokamilisha upauzi wa vyumba vitatu vya maabara ambazo ni kata ya Mughanga, Ipembe, Mfumbuu na kata ya Mandewa huku kata nyingine zimepaua vyumba viwili au  chumba kimoja.

Kuitishwa kwa kikao hicho cha watendaji na waratibu elimu kata ni kuendelea na zoezi la uchangishaji wa wananchi michango ya hali na mali lengo likiwa ni kukamilisha ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara ifikapo Juni 15 mwaka huu

Hata hivyo mkoa wa singida umejiwekea  utaratibu katika kutatua changamoto zinazoikiabili sekta ya elimu ambapo mwaka huu ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara unakamilika, huku ujenzi wa nyumba za  kuishi walimu unatarajia kuanza Julai hadi mwishoni mwezi Juni mwakani.

Halmashauri ya wilaya ya Singida na manispaa ya singida ina jumla ya kata 37 zinaunda halmashuri zote mbili  kati ya kata hizo kata 16 ni za manispaa ya Singida na halmashauri ya wilaya ya Singida ikiundwa na kata 21.

Mwisho.






Friday, May 2, 2014

MEI MOSI - SINGIDA

Na, Doris Meghji Ijumaa Mei 02,2014
Singida



Mkuu wa Mkoa wa Singida DKT. Parseko Kone Akihutumia wananchi wa Mkoa wa Singida Katika sherehe za Mei Mosi kwenye viwanja vya Namfua Manispaa ya Singida ( Picha na Doris meghji)

Ziaidi ya shilingi Bilioni 2,327 milioni,serikali inadaiwa na watumishi wa halmashuri na sekretariati ya mkoa wa Singida yakiwa ni madai ya watumishi walimu na wasio walimu imeelezwa.
Mkuu wa Mkoa wa Singida  Drk. Pareseko Kone na Mama Blandina  Marwa  mwenyekiti wa RAAWU mkoa wa singida na ndio waandalizi wa Mei Mosi mwaka huu ( Picha na Doris Meghji)


Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Paresko Kone ametaja kiasi cha fedha za madai ya watumishi wa mkoa huo kwenye sherehe za Mei mosi mwaka huu katika viwanja vya Namfua kwa kuwataka waajiri kuhakikisha zinakuwepo rejista hai za madeni kwenye ofisi zao ili kuepuka zoezi la ukusanyaji madeni kwa utaratibu wa zima moto.
Baadhi ya viongozi wa vyama wafanyakazi wakiwa katika jukwaa la viwanja vya Namfua manispaa ya Singida (picha Doris Meghji)

Aidha mkuu huyo amewataka waajiri hao kuhakikisha wanakuwa na rejista hai za madeni ya watumishi pindi wanapotaikiwa kuwasilisha serikalini kwa kuwa utaratibu huo wa zima moto unakasoro nyingi ikiwemokutokuwa na orodha ya madeni kwa wakati yakitakiwa kuwasilisha seriakalini
Afisa habari Grace Gwamagobe  Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Singida  akiwa katika sherehe za Mei Mosi ( picha na Doris Meghji)

Epukeni kutumia fedha zilizotolewa za malipo ya madai ya watumishi kwenye shughuli zingine kwani kufanya hivyo ni kosa kubwa ”.Dkt Kone amekemea tabia hiyo ya baadhi ya waajiri kutumia fedha zilizotolewa za malipo ya madai ya watumishi. 
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Singida akitoa utambulisho wa viongozi wa serikali walioudhuria kwenye sherehe za Mei Mosi Jana katika viwanja vya Namfua.(picha na Doris Meghji)

Katika kujibu risala ya shrikisho huru la vyama vya wafanyakazi TUCTA juu ya ombi la kupunguziwa kodi wanayokatwa watumishi kuwa asilimia 9 ya mshahara wa mfanyakazi , tatizo la kutokuwepo kwa wafanyakazi wa tume yauamuzi na usuluhishi(CMA) mkoani singida ikiwa ni pamoja na pendekezo la kima cha chin cha mshahara kuwa 315,000/= mkuu wa mkoa wa Singida amesema kuna baadhi atayachukuwa na kuayafikisha mamlaka hukusika na mengine mkoa iyatafanyia kazi ikiwa ni kufanya mawasiliano na mamlaka na wizara husika ili kutatua kero hizo ikiwemo tume ya usuluhishi na Uamuzi.
Hussen Mwatawala katibu wa mkuu wa mkoa akiwa na Ramadhan Isango RSO katika jukwaa la viwanja vya Namfua manispaa ya Singida ( picha na Doris Meghji)

Hata hivyo amewataka kila mwajiri, mfanyakazi a mtu binafsi kuchukua hatua yakuzuia maambukizi Mapya ya UKIMWI ili nguvu kazi ya mkoa wa singida iendelee kuongeza tija katika uzalishaji kwa kuwa ugonjwa wa UKIMWI bado ni tatizo kama mkoa dalili zinaonyesha sio nzuzi kwa takwimu za mwaka 2013 maambukizi mapya yamefikia alimimi 3.3 kuToka asilimia 2.7 mwaka 2008.
waagizaji wa  igizo la  UKIMWI  lilopendezesha siku hiyo  hasa janga hili la la UKIMWI (picha na Doris Meghji)
kauli mbiu ya Mei Mosi mwaka huu ni
 UTAWALA BORA UTUMIKE KUTATUA KERO ZA WAFANYAKAZI”.
MWISHO.

Mmoja wa watumishi wa sekretarieti ya mkoa wa Singida akipokea cheti cha ufanyakazi bora  kwa mkuu wa mkoa wa Singida DKT. PARSEKO KONE katika viwanja vya  Namfua jana katika sherehe za Mei Mosi (picha na Doris Meghji)

Mmoja wa walinzi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Siingida kipokea cheti  cha Ufanyakzi bora na hundi ya fedha  za kwenye sherehe za Mei Mosi Mwaka huu katika viwanja vya Namfua Manispaa ya Singida (Picha na Doris Meghji)
Baadhi ya watumishi toka vyama mbali mbali vya wafanyakazi wamesimama kwa heshima ya mkuu wa mkoa wa Singida akishuka kwa ajili ya kutoa hotuba  siku ya sherehe hizo za Mei Moi jana katika viwanja vya Namfua Manispaa ya Singida( Picha na Doris Meghji)
mmoja wa hakimu wa mkoa wa wa Singida akipata cheti  cha Ufanyakazi Bora siku ya mei moi Mwaka huu katika viwanja vya Namfua  manispaa ya Singida ( Picha na Doris Meghji)
Bwana Mselem Katibu wa CWT mkoa wa Singida kipoekea cheti cah ufanyakazi bora  katika sherehe za Mei Mosi katika viwanja vya Namfua manispaa ya Singida (picha na Doris Meghji)