Na, Doris Meghji Jumatatu Mei 05, 2014
Singida
Mkuu wa wilaya ya Singda Mwl Queen Mulozi amewaagiza watendaji wa kata na waratibu wa elimu kata kuhakkisha wanakamilisha ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara ifikapo Juni 15 mwaka huu.
Agizo hilo limetolewa leo na Mkuu huyo wa wilaya ya Singida kwa watendaji wa kata na waratibu wa elimu kata ikiwa ni mmoja ya mpango wa mkoa kuhakikisha ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara katika shule zote sekondari za kata mkoani Singida zinakamilika mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu.
Aidha katka kutekeleza agizo hilo kwa watendaji wa kata na waratibu wa elimu kata kunatokana na michango toka wananchi hivyo mkuu wa wilaya huyo amewataka watendaji hao wanakamilisha ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara Juni 15 mwaka huu.
Kwa mujibu wa mmoja wa watendaji kata afisa mtendaji wa kata Mtamaa Mohamed Kipamila amesema kwa upande wa manispaa ya Singida ni kata nne tu zilizokamilisha upauzi wa vyumba vitatu vya maabara ambazo ni kata ya Mughanga, Ipembe, Mfumbuu na kata ya Mandewa huku kata nyingine zimepaua vyumba viwili au chumba kimoja.
Kuitishwa kwa kikao hicho cha watendaji na waratibu elimu kata ni kuendelea na zoezi la uchangishaji wa wananchi michango ya hali na mali lengo likiwa ni kukamilisha ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara ifikapo Juni 15 mwaka huu
Hata hivyo mkoa wa singida umejiwekea utaratibu katika kutatua changamoto zinazoikiabili sekta ya elimu ambapo mwaka huu ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara unakamilika, huku ujenzi wa nyumba za kuishi walimu unatarajia kuanza Julai hadi mwishoni mwezi Juni mwakani.
Halmashauri ya wilaya ya Singida na manispaa ya singida ina jumla ya kata 37 zinaunda halmashuri zote mbili kati ya kata hizo kata 16 ni za manispaa ya Singida na halmashauri ya wilaya ya Singida ikiundwa na kata 21.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment