Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Friday, May 9, 2014

MEDIA DAY - NA WALEMAVU



 MEDIA DAY - NA WALEMAVU Na, Doris Meghji Ijumaa Mei 09 2014
 Singida

Shule ya Msingi Ikungi mchanganyiko ni moja kati ya shule zenye kuhudumia wanafunzi  wasio na ulemavu na wenye Ulemamvu  wilaya ya Ikingu Mkoani Singida Ikiwa ni siku ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa habari Duniani inayoadhimishwa kila mwaka  Mei  03 Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Singida imeamua kuadhimisha siku   kwa kuitembelea shule ya Msingi Ikungi Mchanganyiko kwa kutoa msaada wa vifaa na chakula ikiwa ni moja ya jitihada ya kuuunga mkono juhudi za serikali katika kumwendeleza mtoto mwenye ulemavu nchini.

 Mwenyekiti wa klabu za waandishi wa habari mkoa wa Singida Seif Takaza akiongoza jobo hilo la waandishi wa habari wa mkoa huo amesema licha ya changamoto sekta ya habari nchini wajibu na jukumu la wanahabari ni kuleta maendeleo kwa jamii hivyo klabu hiyo imeazimia kwa dhati kushirikiana na wanafunzi hao wa shule hiyo kwa kuwapatia misaada mbali mbali ya kibinadamu na kutoa fursa kwao kupaza sauti zao kupitia vyombo vya Habari juu ya changamoto wanazokumbana nazo

Aidha amesema jukumu la kuhabarisha ,kufichua,kuonya na kuelimisha jamii juu ya aina yoyote ya ukatili na unyanyapaa wanaofanyiwa watu wenye ulemavu kwa kuandika habari hizo na kuzitangaza  klabu hiyo itaendelea kupaza sauti katika kupinga ukatilii na unyanaya paa wa aina yoyote wanaofanyiwa watu wenye ulemavu. Hivyo klabu hiyo imetoa msaada wa vifaa na vyakula vyenye thamani ya shiling 804,000/= ambavyo ni sahani za plastiki 30 , vikombe vya plastiki 30, ndoo ndogo  5, kilo 100 za unga wa sembe, kilo 150 za mchele,kilo 25 za unga wa ngano,kilo 50 za sukari huku madaftari 300,kalamu 150, majani ya chai katoni  1, mafuta ya kula lita 40 na maharagwe madebe 2 ikiwa ni mchango wao katika kuisaidia jamii hiyo ya walemavu kwenye kuadhimisha siku hiyo ya uhuru wa habari duniani ambayo kitaifa imefanyika  Jumamosi Mei 03 jijini Arusha mwaka huu.

Naye mwalimu mkuu wa shule ya Ikungi mchanganyiko Olvery Tamilly ameishukuru klabu ya wanahabari wa mkoa wa Singida kwa  kuwakumbuka  watoto wenye ulemavu kwa kusherekea siku hiyo ya uhuru wa habari duniani na watoto wenye ulemavu.

 Aidha katika taarifa fupi ya shule hiyo ya Ikungi mchanganyiko Mkuu wa shule hiyo amezitaja changamoto mbali mbali zinazoikabii shule hiyo ya Ikungi mchanganyiko kuwa ni kukosekana kwa mafuta maalum ya ngozi kwa wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi,upatikanaji wa maji ya uhakika katika mazingira ya shule ,ukosefu wa kompyuta maalum kwa wanafunzi wenye ulemavu wa macho ili  kwenda na mfumo wa mawasiliano licha ya kuwa na mwalimu mtaalam mmoja wa kuwafunza jinsi ya utumiaji wa kopyuta hzio bila shida kwa mujibu wa mwl. Tamilly

ameleza kuwa changamoto nyingine ni kutoka kwa baadhi ya wazazi na walezi wa watoto hao wenye ulemavu kuwatelekeza watoto hao mara baada ya kuwepeleka shuleni hapo

 hivyo amewaaomba wazazi na walezi wa watoto kuja kufuatilia maendeleo ya watoto hao kwa kuwa watoto wenye ulemavu sana na watoto wasio na ulemavu  Aidha katika kuendesha shule hiyo 
amsema  shule ina utaratibu wa kuanza na tiba kabla ya kumuanzishia mafunzo mtoto, hivyo uendeshaji wa kituo hicho hutegemea zaidi uwezeshaji wa toka serikali kuu na wafadhili kama chama cha wasiona Tanzania (TLB) na WFP Hata hiyvo mwalimu huyo ameiomba jamii kuitumia shule hiyo kwa kuwapeleka watoto wenye ulemavu ili waweze kuendeleza na sio kuwawaficha majumbani kwao kuwa watoto wenye ulemavu nisawa na watoto wasio na ulemavu

Katika kutembelea baadhi ya  wanafunzi hao kwenye madarasa hayo msaada wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia vinahitajika kwa wananfunzi hao wenye ulemavu ikiwa ni lenzi la kusomea kwa watoto wenye uoni hafifu,mashine au vifaa vya kuandikia vya nukta nundu kwa watoto wasiona,huku na mafuta maalum kwa walemavu ya ngozi yanayowasaidia kujikinga na mionzi ya jua kuku mavazi ya mikono mirefu,kofia za kuwawezesha kufunika kichwa na masikio ili kujikinga na miale ya jua.

 Shule hiyo ya Ikungi Mchanganyiko imechukua wanafunzi 1200 ambapo wanafunzi 104 ndio wenye ulemavu mbali mbali ikiwemo alibinisim 44,wasiona 58 na wene ulemavu wa vinungo 02 na wasio na ulemavu 96. Hata hivyo shule ya Ikungi Mchanganyiko ni umbali wa kilomita 36 kutoka Manispaa ya Singida ilianza kupokea rasmi wanafunzi wenye ulemavu mchanganiko mwaka 1980 kutoka singida mjini hivi sasa shule hio inapokea wanafunzi mbali mbali wenye  ulemavu kutoka maeneo mbali mbali ya nchi. Katika kuadhimisha siku ya uhuru wa habari duniani kauli mbiu mwaka huu ni 
 HABARI NI CHACHU YA MAENDELEO YENYE LENGO LA KUKUZA DEMOKRASIA KWA MTU BINAFSI,JAMII NA TAIFA KWA UJUMLA"
mwisho  


  

No comments:

Post a Comment