Na, Doris Meghji Ijumaa
Mei 02,2014
Singida
Mkuu wa Mkoa wa Singida DKT. Parseko Kone Akihutumia wananchi wa Mkoa wa Singida Katika sherehe za Mei Mosi kwenye viwanja vya Namfua Manispaa ya Singida ( Picha na Doris meghji) |
Ziaidi ya shilingi
Bilioni 2,327 milioni,serikali inadaiwa na watumishi wa halmashuri na
sekretariati ya mkoa wa Singida yakiwa ni madai ya watumishi walimu
na wasio walimu imeelezwa.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Drk. Pareseko Kone na Mama Blandina Marwa mwenyekiti wa RAAWU mkoa wa singida na ndio waandalizi wa Mei Mosi mwaka huu ( Picha na Doris Meghji) |
Mkuu wa mkoa wa Singida
Dkt. Paresko Kone ametaja kiasi cha fedha za madai ya watumishi wa
mkoa huo kwenye sherehe za Mei mosi mwaka huu katika viwanja vya
Namfua kwa kuwataka waajiri kuhakikisha zinakuwepo rejista hai za
madeni kwenye ofisi zao ili kuepuka zoezi la ukusanyaji madeni kwa
utaratibu wa zima moto.
Baadhi ya viongozi wa vyama wafanyakazi wakiwa katika jukwaa la viwanja vya Namfua manispaa ya Singida (picha Doris Meghji) |
Aidha mkuu huyo amewataka
waajiri hao kuhakikisha wanakuwa na rejista hai za madeni ya
watumishi pindi wanapotaikiwa kuwasilisha serikalini kwa kuwa
utaratibu huo wa zima moto unakasoro nyingi ikiwemokutokuwa na
orodha ya madeni kwa wakati yakitakiwa kuwasilisha seriakalini
Afisa habari Grace Gwamagobe Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Singida akiwa katika sherehe za Mei Mosi ( picha na Doris Meghji) |
“Epukeni kutumia fedha
zilizotolewa za malipo ya madai ya watumishi kwenye shughuli zingine
kwani kufanya hivyo ni kosa kubwa ”.Dkt Kone amekemea tabia hiyo
ya baadhi ya waajiri kutumia fedha zilizotolewa za malipo ya madai
ya watumishi.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Singida akitoa utambulisho wa viongozi wa serikali walioudhuria kwenye sherehe za Mei Mosi Jana katika viwanja vya Namfua.(picha na Doris Meghji) |
Katika kujibu risala ya
shrikisho huru la vyama vya wafanyakazi TUCTA juu ya ombi la
kupunguziwa kodi wanayokatwa watumishi kuwa asilimia 9 ya mshahara
wa mfanyakazi , tatizo la kutokuwepo kwa wafanyakazi wa tume yauamuzi
na usuluhishi(CMA) mkoani singida ikiwa ni pamoja na pendekezo la
kima cha chin cha mshahara kuwa 315,000/= mkuu wa mkoa wa Singida
amesema kuna baadhi atayachukuwa na kuayafikisha mamlaka hukusika na
mengine mkoa iyatafanyia kazi ikiwa ni kufanya mawasiliano na mamlaka
na wizara husika ili kutatua kero hizo ikiwemo tume ya usuluhishi na
Uamuzi.
Hussen Mwatawala katibu wa mkuu wa mkoa akiwa na Ramadhan Isango RSO katika jukwaa la viwanja vya Namfua manispaa ya Singida ( picha na Doris Meghji) |
Hata hivyo amewataka kila
mwajiri, mfanyakazi a mtu binafsi kuchukua hatua yakuzuia maambukizi
Mapya ya UKIMWI ili nguvu kazi ya mkoa wa singida iendelee kuongeza
tija katika uzalishaji kwa kuwa ugonjwa wa UKIMWI bado ni tatizo kama
mkoa dalili zinaonyesha sio nzuzi kwa takwimu za mwaka 2013
maambukizi mapya yamefikia alimimi 3.3 kuToka asilimia 2.7 mwaka
2008.
waagizaji wa igizo la UKIMWI lilopendezesha siku hiyo hasa janga hili la la UKIMWI (picha na Doris Meghji) |
kauli mbiu ya Mei Mosi
mwaka huu ni
UTAWALA BORA UTUMIKE KUTATUA KERO ZA WAFANYAKAZI”.
MWISHO.
mmoja wa hakimu wa mkoa wa wa Singida akipata cheti cha Ufanyakazi Bora siku ya mei moi Mwaka huu katika viwanja vya Namfua manispaa ya Singida ( Picha na Doris Meghji) |
Bwana Mselem Katibu wa CWT mkoa wa Singida kipoekea cheti cah ufanyakazi bora katika sherehe za Mei Mosi katika viwanja vya Namfua manispaa ya Singida (picha na Doris Meghji) |
No comments:
Post a Comment