Na,Doris Meghji Jumane Mei 06,2014
Singida
Mtoto mwenye umri wa miaka miwili afariki dunia juzi mara baada ya kuzama ndani ya karo la maji liliopo kwenye kiwanja jirani na nyumbani kwao eneo la Mwantanda Kata ya Mandewa Manispaa ya Singida
Taarifa hiyo kwa waandishi wa habari toka kwa Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Singida SACP Geofrey Kamwela imeleza kifo cha mtoto aitwae Silvester Elias kimemfika akiwa anacheza na watoto wenzake ambapo mtoto huyo alipanda ukuta uliozungushiwa karo lenye urefu wa futi mbili kutoka usawa wa ardhi na kuteleza kisha kutumbukia kwenye karo liliojengwa la kuhifadhia maji kwa ajili ya matumizi ya shuguli za ujenzi lenye kina cha futi 8.
Aidha kwa Mujibu wa taarifa hiyo toka kwa kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida imesema hakuna mtu au watu waliokamatwa kutokana na tukio hilo na jeshi hilo linaendelea na uchunguzi.
Wakati huo huo mtu mmoja afariki dunia na Mwingine kujeruhiwa kutoka na ajali ya gari lenye shehena ya mafuta lenye usajiri namba T467 BAG /T 478 BAG aina IVECO likiendeshwa na dereva Faustine Augustino Mkazi wa mwanza mara baada ya kuacha njia na kupinduka jana majira ya saa tisa na nusu mchana eneo la mlima Sekenke barabara ya Singida Igunga kata ya Ulemo wilaya ya Iramba mkoa wa Singida
kwa mujibu wa Kamanda Kamwela amesema gari hilo liloluwa limebeba sehena ya mafuta ya taa liliacha njia na kupindika na kusababisha kifo cha mtu mmoja aitwaye Latipha Shabani anayekadiriwa kuwa na umri wa mika 38 mkazi wa kipawa - Dar es salaam ambaye alikuwa abiria katika gari hilo huku dereva wa gari hilo akiwa amejeruhiwa kichwani na
kulazwa katika hospitali ya wilaya ya Igunga mkoani Tabaora
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Kiomboni wilaya ya Iramba mkoa wa Singida
Jeshi hilo la polisi linafanya uchunguzi kuhusu chanzo cha ajali hiyo na dereva wa gari hilo anashikiliwa na posili kwa uchunguzi zaidi.
Hivyo jeshi hilo la polisi linatoa wito kwa madereva wa magari yote wanaopita mkoani Singida kutoka mikoa mingine au nje ya nchi kuwa makini hususani wafikapo maeneo ya mlima na mteremko
No comments:
Post a Comment