Benki
ya Posta yajizatiti kupeleka huduma mikioani
Na
Johnson Soah, Singida
May
13, 2015
Benki ya Posta Tanzania (TPB)imejizatiti kupeleka
huduma mikoani ambapo jana Maya 11 mwaka huu imefungua tawi jipya mkoani
Singida, ikiwa ni ishara ya kuleta ushindani mkoani hapa.
Akizungumza katika hafla hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi amesema
kuwa benki hiyo imejipanga kuimarisha huduma zake kwa kufungua matawi mengi ili
kuhakikisha wakazi wengi wanajiunga na benki hiyo.
“Kwa kutambua mahitaji ya wananchi tumejipanga
kuimarisha huduma zetu kwa kufungua matawi mengi nchi nzima na leo mmeona
tumefungua tawi jipya hapa, hivyo ni fursa kwenu wakazi wa mkoa huu na mfanye
hima kuichangamkia”. Alisema.
Naye mwanyekiti wa bodi ya benki hiyo Profesa
Lettice Rutashobya amesema kuwa ni vyema wananchi kutambua kuwa benki ya posta
ni benki ya Watanzania, hivyo ni wajibu wao kujiunga na Benki yao.
“Wakazi wa Mkoa huu na Watanzania kwa Ujumla, hii ni
benki yenu ya kitanzania hivyo ni wajibu wenu kujiunga kwani gharama zake ni
nafuu”. Alisisitiza.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Singida, Bw.
Saidi Ally Amanzi amewahimiza wananchi mkoani Singida Kuwa na moyo wa kupenda
,kuthamini na kujivunia benki yao kuliko kuthamini vitu kutoka nje,
“ Hii ni benki yenu, wananchi kuweni na moyo wa kupeinda, kujivunia na kuithamini”.
Alisema Bw. Amanzi huku akionesha msisitizo huku akihimiza kupunguza gharama
zake ili kuvutia wateja wengi zaidi.
Benki ya Posta Tanzania ina matawi ishirini na nane
na mengine madogo madogo 21 na Akaunti 188 nchi nzima.
No comments:
Post a Comment