HABARI KATIKA PICHA - KUTOKA SINGIDA
|
Ni Mbunge wa viti maalumu(CCM)Mkoa wa Singida,Bi Marther Mosses Mlata akiongea na wananchi pamoja na wanachama wa UWT Kata ya Ibaga,tarafa ya Kirumi alipokuwa katika ziara ya kukiimarisha chama cha Mapinduzi wilayani Mkalama. |
|
Ni Mbunge wa viti maalumu(CCM) Mkoa wa Singida,Bi Marther Mosses Mlata(wa pili kutoka kulia) akimkabidhi pikipiki mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Mkalama,Bi Elipendo Machafuko(aliyepanda pikipiki) atakayotumia kuwatembelea wanachama wa jumuiya hiyo.Wengine walioshuhudiwa hafla ya makabidhiano hayo ni pamoja na Katibu wa CCM wilaya ya Mkalama,Bw.Amosi Shimba(wa kwanza kulia),Bi Hadija Kisuda-mwenyekiti wa UWT wilaya ya Singida vijijini(wa tatu kutoka kulia) na katibu wa UWT Mkoa wa Singida,Bi Anjela Robert(wa kwanza kutoka kushoto). |
|
Ni Katibu msaidizi wa CCM Wilaya ya Mkalala,Bi Matrher Zingula (wa pili kutoka kulia) akimkaribisha Mbunge wa viti maalumu(CCM) Mkoa wa Singida,Bi Marther Mosses Mlata(wa tatu kutoka kulia)alipotembelea wilayani hapa kwa ziara ya kukiimarisha chama na wa nne kutoka kulia ni Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Singida vijijini,Bi Hadija Kisuda |
|
Ni Baadhi ya wajumbe wa Baraza la UWT wilaya ya Mkalama waliohudhuria kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa ofisi za Chama Cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Mkalama. |
Ni Baadhi ya pikipiki zilizokabidhiwa kwa wenyeviti wa wilaya wa UWT katika Mkoa wa Singida kwa lengo la kuwarahisishia suala la usafiri.PICHA zote Na,Jumbe Ismailly.
|
Ni Katibu wa CCM wilaya ya Mkalama,Bw.Amosi Shimba(wa pili kutoka kushoto) akimkabidhi zawadi ya mbuzi aliyetolewa na wanachama wa jumuiya hiyo.Wengini ni Mbunge wa viti maalumu (CCM) Mkoa wa Singida,Bi Marther Mosses Mlata(wa pili kutoka kulia) akimpokea mbuzi,Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Ikungi,Bi Christina S.Hamisi(wa tatu kutoka kulia),Bi Jenifer Miano-Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Iramba(wa nne kutoka kulia)na Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Singida vijiji,Bi,Hadija Kisuda(wa tano kutoka kushoto). |
|
Ni Mbunge wa viti maalumu (CCM) Mkoa wa Singida,Bi Marther Mosses Mlata(wa kwanza kulia)akiwakabidhi makatibu wa matawi ya jumuiya ya UWT baiskeli moja kwa kila kata. |
Ni Katibu wa UWT Mkoa wa Singida,Bi Anjela Robert( wa kwanza kushito) akimuelekeza mbunge wa viti maalumu (CCM) Mkoa wa Singida,Bi Marther Mosses Mlata(wa pili kutoka kulia) akimshauri kuonyesha zawadi aliyowapelekea wanachama wa jumuiya hiyo.Wengine ni Bi Christina S.Hamisi(wa kwanza kulia),Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Mkalama,Bi Elipendo Machafuko(wa tatu kutoka kulia) na mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Iramba,Bi Jenifer Miano(wa pili kutoka kushoto)
(PICHA ZOTE NA JUMBE ISMAILY)
No comments:
Post a Comment