Na,
Doris Meghji Jumapili Mei 10, 2015
Kijiji
cha Ovada Wilaya ya Chemba –Dodoma
Mnara wa simu ya kampuni ya TTCL uliojengwa kijiji cha Ovada wilaya ya Chemba mkoa wa Dodoma (Picha na Doris Meghji) |
Kampuni
ya simu Tanzania TTCL imeombwa kuanzisha huduma ya TTCL PESA ili kuwasaidia wanachi kutuma na kupokea pesa katika
maeneo ambayo mtandao huo unapatikana kwa uhakikika kama mitandao mingine ya
simu nchini inavyofanya.
Wananchi
wa kijiji cha OVADA wilaya ya Chemba wametoa ombi hilo kwa kampuni hiyo ya simu
kwenye uzinduzi rasmi wa mnara wa simu uliyojengwa katika kijiji hicho chini mradi
wa kupeleka mawasiliano vijijini kupitia mfuko wa (UCSAF) kwa kuiomba kampuni
hiyo ya simu kuanzisha huduma hiyo ya kutuma na kupokea pesa kwa njia ya simu
kwa kuwa TTCL ndio mtandao pekee
unaopatikana kwa uhakika kijijini hapo
Meneja waTTCL mkoa wa Singida akitamnulisha wageni katika kijiji cha OVADA kwenye uzinduzi rasmi wa mnara wa mawasilino ya TTCL wilayani Chemba (Picha na Doris Meghji) |
Wakiongea
na blog hii kwa nyakati tofauti bi Garce Vicent mkazi wa Kijiji cha Ovada na
bwana Chilomoto Muyuesegu wameishukuru kampuni hiiyo ya simu kwa kujenga mnara
kijijini hapo kwa kuwarahisha mawasiliano kwa kuwa sasa hawana haja ya kupanda
miti na milima ili kupata mtandao wa simu kwenye kufanya mawsiliano.
“ombi
letu kwa TTCL ni kutuletea huduma ya TTCL pesa ili tuweze kuwatumia au kupkea
pesa kwa njia ya simu kama mitandao mingine,ili isitulazimu kuwa na simu zenye
line ya mitandao mengine tukitaka kufanya hivyo walisema wakazi hao”
Baadhi ya watumishi wa kampuni ya simu ya TTCL mkoa wa Singida wakimsikiliza mgeni rasmi katika Hafla hiyo ya kuzindua mnara wa mawasilino ya simu kijiji cha OVADA (Picha na Doris Meghji) |
wananchi wa kijiji cha OVADA wakiwasiliza viongozi wao katikahafla yauzinduzi rasmi wa mnara wa mawasiliano ya simu ya kampuni ya TTCL (Picha na Doris Meghji) |
Kwa
upande wa meneja mkuu wa kanda ya
kaskazini ya kampuni hiyo TTCL Brown Japhet ambaye anasimamia mkoa wa Kilimanjaro,Arusha,Tanga,Manyara
na Singida amesema uzinduzi wa mnara huo unalenga kuhudumia zaidi ya vijiji
saba katika wilaya ya Chemba ambavyo ni Ovada,Baaba,Jogolo,Dinae Mengu,Takwa na
Kinyamshindo vyenye wakazi zaidi ya kumi na tano elfu wenye kugharibu takribani
shilingi milioni 51,300,000/=
Aidha
amewaomba wananchi wa vijiji hivyo kutunza na kulinda miundo mbinu ya mnara huo
ambao unawapatia mawasiliano kwa kuunga mkono jitihada za serikali kuhakikisha
upatikanaji wa mawasilino kwa urahisi zaidi kwa kuchangia ukuaji wa maendeleo
katika maeneo ya vijijini.
Mh. Diwani Pius Majengo wa kata ya OVADA Akihutubia wananchi wa kikiji cha Ovada katika uzinduzi rasmi wa mnara wa mawasilino ya simu ya TTCL (Picha na Doris Meghji) |
Naye
Diwani wa kata hiyo ya OVADA bwana Pius Majengo kwa niaba ya mgeni rasmi Mkuuwa wilaya ya Chemba ametoa taadhari kwa wananchi wa kijiji na kata
hiyo kutumia fursa hiyo ya mawasilino ya TTCL kutumia vizuri kwa kupeana
taarifa na sio kwa matumizi mengine ya kutukana nana au laa kwa kuwa na
mawsiliano kusilete matatizo miongoni mwao.
Ujenzi
wa mnara huo ulianza rasmi Februari mwaka 2014 na uzinduzi kufanyika MEI 07
MWAKA HUU.
Kwayaya parokia ya OVADA ikitumbuiza katika hafla ya uzinduzi wa mnara wa kampuni ya TTCL wilaya ya Chema mkoa wa Dodoma(Picha na Doris Meghji) |
Mjumbe wa bodiya shule ya Sekondari akipokea mmoja ya simu iliyotolewa na Kampuni ya SIMU ya TTCL katika uzinduzi rasmi wa manara wa simu katika kijiji cha OVADA (Picha na Doris Meghji) |
MWISHO.
No comments:
Post a Comment