|
MKUU WA MKOA WA SINGIDA DKT PARSEKO KONE AKIFUNGUA KIKAO CHA USHAURI CHA MKOA WA SINGIDA (PICHA NA Doris Meghji) |
Na, Doris Meghji Jumatatu April 07,2014
Singida
Mamlaka za serikali za mitaa za mitaa mkoani Singida zimeagizwa kulipa uzito na kipaumbele suala la ujasiliamali kwa kutenga fedha za kuwakopesha wanawake na vijana ikiwa ni pamoja na kuanisha maeno ya kufanyia shughuli za miradi yao kwa lengo la kupunguza tatizo la ajira na kipato kwa wananchi wenye mtazamo chanya imeleezwa
|
Mwl Queen Mulozi na wakuu wa wilaya wenzake wa mkoa wa Singida (picha na Doris Meghji) |
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa mkoa wa Singida DKT. PARSEKO KONE wakati akifungua kikao cha ushauri cha mkoa (RCC) katika ukumbi wa VETA April 05 manispaa ya Singida.
Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa huyo amezitaka mamalaka hizo za mitaa kuendelea kulipa uzito wa peeke suala la ujasilimali kwa kutenga fedha za kwakuopesha wananwake na vijana kupitia vikundi ikiwa ni pamoja na kuanisha maendo ya kufanyia shughuli kwa vijana ikiwemo kuwezesha miradi ya kati na midogo iliyothaminiwa kwa kina na isiyo na gharama kubwa za uendeshaji..
|
Baadhi ya wajumbe toka sekretariati ya mkoa wa Singida kwenye kikao cha ushauri cha mkoa wa Singida (picha Doris Meghji) |
" kama vile miradi midogo midogo ya umwagiliaji, ufugaji wa kuku wa asili kibiashara na ufugaji nyuki tukiweka juhudi kwenye maeneo haya tutapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la ukosefu wa ajira na kipato kama mtazamo wa wananchi utaendela kubadilika nakuwa na mwitikio chanya." alisema mkuu huyo wa mkoa
Hata hivyo hali ya utekelezaji wa baadhi ya miradi ianasua sua kutokana na mtirirko wa upokeaji wa fedha toka seriklai na kwa wafadhali, hivyo mkuu wa mkoa huyo amewataka kuijiwekea vipaumbele vya kutekeleza kwa muda uliobaki wa mwaka 2013/2014 ili miradi itakayokosa fedha ikiwezekana iaharishwe hadi mwakani bia kusahau kuzingatia maelekezo ya serikali kwa kuepuka kuingia mikataba kabla yakuwa na fedha za uhakika ili kuepuka madeni yanayodaiwa na wazabuni na wakandarasi mbali mbali .
|
Baadhi ya Wajumbe wa kikao cha ushauri cha mkoa wa Singida ( Picha na Doris Meghji) |
mkoa wa singida uliidhinishiwa na bunge jumbla ya shilingi 113,308,560,988/= kwa ajili ya mishahara ,matumizi mengineyo na miradi ya maendeleo kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2013/2014 kati ya fedha hizo fedha za miradi ya maendeleo shilingi 16,986,660,748/= ni fedha za hapa nchini huku shilingi 14,689.215,593/=ni fedha za nje
|
kushoto ni Katibu Tawala mkoa wa singida Liana Hassan kulia ni Dkt Parseko Kone ( Picha na Doris Meghji) |
|
Aidha katika ukopeaji wa fedha za matumizi mkoa wa singida hadi kufikia Disemba 2013 ulipokea shilingi 5,516,452,765/= sawa na asilimia 47.6 ya fedha iliyoidhinishwa kwa ajili ya sekretairate ya mkoa ,kiasi cha shilingi 696,436,033/= zikwa kwa ajili ya mautumizi mengineyo na shilingi 2,297,923,500/= kw ajili ya mishahara na shilingi 2,522,092,931 zikiwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
|
IT wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Singida Picha na Doris Meghji) |
kwa kipindi cha fedha cha mwaka 2014/2015 mkoa wa singida umepanga bajeti ya jumla shilingi 170,130,998 208/= shilingi14,910,538,416/= zikiwa za matumizi mengineyo,fedha za mishara 102,451,801,577/= shilingi 117362,339,993/= za matumizi ya kawaida huku fedha za ndani za miradi ya maendeleo zikiwa ni shilingi 22,284,268,950/= na fedha za nje za miaradi ya maendeleo ni shilingi 22,502,072,123/= huku mapato ya ndani kuwa ni shilingi 7,982,317,142/=
MWISHO.