Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Tuesday, April 15, 2014

WAANDISHI WA HABARI MKOA WA SINGIDA WATAKIWA KUZINGATIA MAADILI YA TAALUMA YAO KATIKA UANDISHI WA HABARI KATIKA MAZINGIRA HATARISHI-BI LILIAN TIMBUKA AWAASA WAANDISHI

MAFUNZO  JUU YA  MAADILI NA UANDISHI WA HABARI KATIKA MAZINGIRA HATARISHI KWA  WAANDISHI WA HABARI MKOA WA SINGIDA YALIYOANDALIWA NA BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) YALIFANYIKA JUMANNE APRIL 08 HADI APRIL 11,2014 KATIKA OFISI ZA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA SINGIDA (SINGPRESS)
Na, Doris Meghji Jumanne April 15,2014
Singida

 Waandishi wa habari mkoa wa singida wametakiwa kunzingatia maadili ya taaluma yao ya habari lengo likiwa ni kupunguza migogoro katika kuandika habari kwenye mazingira hatarishi.

Mwezeshaji Juma Thomas na Lilian Timbuka wakiwasikiliza waandishi wa habari wanapowasilisha kazi zao mara bada ya kupewa mafuzo juu ya uzingatiaji wa maadili ya taaluma ya uandishi wa habari hasa katika kuandika habari kwenye mazingira hatarishi huku wakitakiwa kutokuwa chanzo cha migogoro kutoka na uandishi wao( Picha na Doris Meghji)

Bi Lilian Timbuka  mmoja wa wawezeshaji wa mafunzo hayo amwewataka waandishi wa habari wa mkoa wa Singida kunzingatia maadili yanaiongoza taaluma hiyo ya habari kwenye mafunzo ya Siku nne yalioandaliwa na baraza la habari  Tanzania ikiwa ni mmoja ya njia ya kuwanjengea uwezo waandishi wa habari nchini juu ya maadili na uandishi wa habari katika mazingira hatarishi.

Mwenyekiti ya SingPres Seif Takaza na baadhi ya wanachama wa Singida press Club wakifuatilia mafunzo katika mafunzoya maadili ya tasnia ya Habari na uandishi wa habarai katika mazingira hatarishi (picha na Doris Meghji)
Aidha awewaasa waandishi wa habari mkoa wa Singida kujenga utamaduni wa kujisomea machapisho na vitabu mbali mbali ili waweze kujiongezea ufahamu juu ya mambo mbali mbali "watanzania wa leo sio wa zamani sasa watanzania wamebadilika kukuwa kwa teknolojia kunawafanya watanzania kupata taarifa hadi vijijini hivyo ni vyema kujijengea utaratibu huo wa kujisomea machapisho mbali mbali  ili mjue vitu gani vinaendela katika dunia hii" aisisitiza mwezeshaji huyo.

Kijana Aman Moses akiwakilisha mmoja ya kundi la waandishi wa habari mara baada ya kupewa zoezi wafanya juu ya uandishi wa habari unaozingatia maadili na uandishi wa habari katika mazingira hatarishi kwenye mafunzo hayo ( Picha na Doris Meghji)
 Hivyo aliwataadharisha waandishi hao kuwa makini katika kuandika habari zao kwa kuanzingatia maadili kwa kuwa sheria kandamizi za uhuru wa habari bado zinatumika nchini na kuwataka wae makini na kuandiska habari za ukweli na uhakika kwa kuzingatia haki za binadamu ikiwa ni paoja na kupunguza migogoro na kuto kuwa chanzo na kichochoteo cha migogoro miongoni wa jamii na kuwataka kuwa wasuluhishi nadi ya jamii kwa kuzifanyia tafiti habari wanazo andika

Abby Nkungu na baadhi ya waansishi wa habari toka kituo cha radio cha Standard radio FM kilichopo manispaa ya Singida wakifuatila uwasilishawaji wa mmoja ya kundi baada ya kupewa zoezi la kuandika habari kwa kunzingatia maadili ya taaluma ya uandishi wa habari katika mazingira hatarishi.(picha na Doris Meghji)

kwa niaba ya waandishi wa habari hao mara baada ya mafunzo Damino Mkumbo Makamu Mwenyekiti wa klabu ya waandishiwa habari mkoa wa Singida amlishukuru baraza la habari Tanzania (MCT) kwa kutoa mafunzo hayo kwa wanahabari wa mkoa wa singida na kusema kuwa mafunzo hayo yamekuja muda muaafaka kwa kuwa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi wa chaguzi mbali mbali za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa madiniwani wabunge na rais mwaka 2015

Bi Anita mratibu wa mafunzo toka Baraza la Habarai Tanzania (MCT)  akiwasiliza waandishi wanapowasilisha kazi zao na kuanza kujadiliwa na darasa katika katika mafunzo hayo.(picha na Doris Meghji)

Aidha Makamu Mwenyeki Mkumbo  amehaidi kubadilika kwa uandishi wa waandishi wa habari wa mkoa wake kwa kwa sasa wamejengewa uwezo na  kuelewa cha kufanya katika uandishi wa o kwa kuzingatia maadili  na miongozo ya taaluma yao ikiwa ni pamoja na kuzingatia  kuzingatia haki za banadamu  katika kuelimisha ,kuhabarisha na kuionya jamii ya watanzania kuptia kalamu zao.


Phesto Sanga akinyoosha kidole kutaka kutoa maoni juu ya kazi iliyowasilishwa na mmoja ya kikundi kwenye mafuzo hayo.(picha na Doris Meghji)   
Hata hivyo zaidi ya waandishi wa habari 20 wamejengewa uwezo  katika mafuzo hayo mkoani Singida.

Mwisho.









No comments:

Post a Comment