Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Wednesday, April 16, 2014

SERIKALI YA UINGEREZA IKO TAYARI KUFANYA KAZI BEGA KWA BEGA NA SERIKALI YA TANZANIA KWENYE UZALISHAJI YA UMEME WA UPEPO MKOANI SINGIDA.

Na, Doris Meghji Jumatano Aprili 16,2014
Singida
DC Queen Mulozi  katikati na Stephen Masele Naibu waziri wa Wizara ya Nishati na Madini akiwa pamoja na Waziri wa nchi Kitengo cha Nishati na Mabadiliko ya hali ya hewa nchini Uingereza Gregory Barker wakati akitia saini kwenye kitabu cha wageni katika eneo la mradi(picha Doris Meghji)


Serikali Nchini Uingereza imesema iko yatari kufanya kazi bega kwa bega na serikali ya Tanzania katika mradi wa uzalishaji wa nishati ya Upepo ili kuisaidia Tanzania kukabiliana na changamoto ya uzalishaji wa nishati hiyo kwa watanzania.

Waziri wa Nchi kitengo cha Nishati na Mabadiliko ya hali ya hewa Bw,Gregory Barker amesema hayo mapema wiki hii Mkoani Singida katika ziara yake ya kutembelea mradi wa kuzalisha nishati ya upepo nchini Tanzania ya Wind East Africa LTD
Rashid Shamtee Mkurugenzi wa Wind East Africa LTD nchin Tanzania akitoa maelezo mbele ya  Waziri wa Uingereza wa Nishati na mabadiliko ya hali ya hewa kwenye eneo la mradi.(picha na Doris Meghji)


Aidha Waziri huyo amesema serikali yake itakuwa tayari kufanya kazi na Tanzania hasa katika uzalishaji wa nisati hiyo ya upepo Mkoani Singida kwa kuzalisha nishati safi isiyoathiri mazingira kwa manufaa ya wananchi wa kawaidi wa mkoa huo na Tanzania kwa ujumla

Uingereza iko tayari kushirikiana na Tanzania hasa katika suluhisho la uzalishaji wa nishati safi ya upepo isiyoathiri mazingira tutashirikiana kwa mradi huu kwa lengo  kuwasaidi na kuwanufaisha wananchi wa kawaida hivyo nitarudi tena kuja kusimamia na kuhakikisha mradi huu unafanya kazi” alisisitiza Waziri Barker.
Naibu waziri  Stephene Masele akibadilishana mawazo na Dkt Parseko Kone mkuu wa mkoa wa Singida wakati wakimsubiri kuwasili Waziri wa nishati na mabadiliko ya hali ya hewa Gregory Barker  katika kiwanja cha ndege cha manispaa ya singida (picha na Doris Meghji)
Naye Naibu wa Wizara ya Nishati na madini Mh. Stephen Masele ameishukuru serikali ya uingereza kwa kuonyesha nia na kuwa tayari kufanya kazi na serikali ya Tanzania hasa katika kuwekeza
kwenye mradi wa uzalishaji wa nishati hiyo ya Upepo mkoani Singida  utasaidia  ongezeko la uzalishaji wa nishati ya umeme nchini.

Kulia ni Gregory Barker waziri wa Nishati na mabadilo ya hali ya hewa toka Uingereza akisaini kitabu cha wageni kwenye mradi wa uzalishaji wa nishati ya upepo katikati ni Stephen Masele Naibu waziri wa Nishati na madini kushoto ni Queen Mulozi Mkuu wa wilaya ya Singida (Picha na Doris Meghji)

Naibu waziri huyo amesema ifikapo mwaka 2015 wizara imepanga kufikia malengo ya kuzalisha nishati ya umeme zaidi ya MW 2700 kutoka uzalishaji wa sasa ambao ni MW 1500 hivyo uzalishaji wa Nishati ya upepo ni mmoja ufumbuzi wa nishati mbadala kwa wizara utakaosaidia kuongeza uzalishaji.

“mpango na mikakati ya seriklai ni kuweza kuzalisha umeme toka toka vyanzao mbali mbali nasio kutegemea nishati ya umeme wa maji karibu MW 500 zinazalisha kutokana na nishati hiyo huku asilimia 56 ni kutokana na gasi asilia” alisistiza Naibu waziri Masele

Katika kuanza utekelezaji wa mradi huo Naibu waziri huyo ameliagiza shirika la umeme Tanzania Tanesco kutakiwa kumaliza majadiliono na kampuni ya kuzalisha nishati ya umeme kwa kutumia nguzu ya upepo ya Wind East Africa Limited ili mradi wa uzalishaji umeme huo uanze kufanya kazi mkoani Singida
Baadhi ya wadau wa nje ya nchi na mkoa wa Singida  wakitembealea mradi wa uzalishaji wa umeme wa upepo (Picha na Doris Meghji)

Awali akielezea juu ya mradi huo mkurugenzi wa kampuni ya Windi East LTD nchini Tanzania Rashid Shamte amesema kampuni yake inatarajia kuanza kazi ya ujenzi wa mitambo katikati ya mwaka kesho na kuanza kazi rasmi  ya uzalishaji wa nishati hiyo mwaka 2016 kwa kuzalisha MW 100 za nishati ya upepo na kuuzia TANESCO utakao ingizwa kwenye  gridi ya Taifa mara baada ya shirika hilo la umeme kukamilisha majadiliano na  kampuni yake.

Naye Mwakilishi wa wananchi wa kata hiyo ya Unyamikumbi Mh. Mosese Ikaku Diwani wa kata hiyo ambapo mradi huo wa upepo unatekelezwa  ameomba wizara ya Nishati na Madini  ifanye haraka ili mradi huo uanze utekelezaji wake kwa kuwa wananchi wameupokea kwa mikono miwili mradi huo kwa la kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Balozi Diane Mel rose wa uingereza nchini Tanzania na baadhi ya wageni waliongozana na ugeni huo uliotembela mradi wa uzalishaji wa nishati ya upepo mkoa wa Singida (Picha na Doris Meghji)

Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone ameishukuru  Wizara  ya nishati na madini na serikali ya uingereza kwa kuwa tayari kuwekeza katika mkoa wa Singida katika uzalishaji wa nishati hiyo ya upepo ili kusaidia wananchi wa mkoa huo.
Magari ya msafara wa Waziri wa uingereza na Naibu waziri wa wizara ya nishati na madini  walipotembela mradi wa umeme wa upepo manispaa ya Singida (Picha na Doris Meghji)
Hata hivyo kampuni mbili za Wind East Africa LTD na kampuni ya Power Pull zimeonyesha nia ya kuwekuza katika uzalishaji wa nishati hiyo ya upepo mkoani hapa,
Mwisho




No comments:

Post a Comment