Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Thursday, October 6, 2016

KAYA 16,000 KUFIKIWA KATIKA UTAFITI WA HALI YA MAAMBUKIZI YA UKIMWI NCHINI IKIWA SAMPULI WAKILISHI YA WATANZANIA KWENYE UTAFITI HUO


NA,DORIS MEGHJI JUMATANO OKTOBA 05,2016
SINGIDA


Jumla ya kaya kumi na sita elfu zinatarijiwa kufikiwa katika utafiti wa hali ya maambukizi ya  Ukimwi nchini ambapo watanzania 42,000 wakiwemo watoto wapatao elfu 8  ikiwa ni sampuli  wakirishi ya watanzania wote nchini wanatarajiwa kufikiwa kwa lengo la kupima na kujua hali ya maambukizi ya ukimwi kila baada ya miaka minne nchini.

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa ICAP ametoa maelezo hayo kwenye moja ya kikao cha wadau wa ukimwi mkoani singida katika kutolea maelezo suala la waandishi wa habari kufikisha ujumbe sahihi juu ya utafiti huo kwa wananchi ili waweze kujitokeza kupima bure afya zao bila malipo

Ukimwi ni moja ya gonjwa linalowasumbua watanzania wengi  na kusababisha yatima na tegemezi wengi, kupatikana kwa takwimu za tafiti mbali mbali za magonjwa zitasaidia sana mipango mbali mbali kufanyika katika kukabilina tatizo hilo kwa upande wa wananchi wako tayari kiasi gani kushiriki kwenye zoezi hilo la utafiti.


Wadau wakuu wa utafiti huo kwa kushirikiana na kitingo cha ctc toka Shirika la Marekani la Chuo Kikuu cha Columbia [ICAP] anaelezea lengo la utafiti huo kwa mwaka huu.


Mihayo  Mageni Lupamba mkuu wa kitengo cha mawasiliano ICAP

Mhandisi Mathew Mtigumwe mkuu wa mkoa wa singida amewasisitiza wananchi wake watoe ushirikiano wa kutosha kwenye utafiti huo



Mhandisi Mathew Mtigumwe Mkuu wa mkoa wa Singida

MWISHO
Attachments area

No comments:

Post a Comment