NA. Doris Meghji ALHAMISI OKTOBA 07,2016
SINGIDA
Wananchi mkoani Singida wametakiwa
kutumia fursa ya uhakika wa soko la asali la kimataifa liliojitokeza kwa asali yao
kuaminiwa kimataifa imefahamika
hilo limejitokeza leo kwa kaimu
mkurugenzi mkuu wa TANTRADE NCHINI kwenye ufunguzi wa mafunzo ya uwezeshaji
wafanyabiashara wadogo na wakati wa sekta ya nyuki,bidhaa ya asali ili
kulifikia soko la ushindani kwa wananchi
waliojikita katika sekta ya ufugaji nyuki mkoani SINGIDA huku suala la kujiunga katika umoja wao
kutiliwa mkazo kwenye Ufunguzi wa mafunzo hayo.
EDWIN RUTAGERUKA KAIMU MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA MAENDELEO YA BIASHARA TANZANIA - TANTRADE |
Asali ni moja ya zao la misitu la
kipaumbele mkoani hapa, soko zuri la zao hili lilikuwa changamoto kwa wajasiriamali wa zao hilo hasa
kwa kutakiwa kufuga kisasa na kuchakata kisasa kwa asali yao kisasa kwa uhakika
wa soko.
Aidha katika kufungua mafunzo hayo mkuu
wa mkoa wa singida amewataka wananchi
wake kuzalisha asali ya kutosha ili iweze kukidhi mahitaji ya viwanda vilivyopo
vya kuchakata asali huku suala vifungashio nalo kuliongelea pia
Mhandisi MATHEW MTIGUMWE MKUU WA MKOA WA SINGIDA |
Rais wa chama cha ushirika
wa vijana wajasiriamali na wataalam wa miradi mkoanini singida ametaka vijana
kujitumia fursa hiyo ya soko wa zao hilo.
PHILIMON KIHEMI RAIS WA CHAMA CHA USHRIKA WA VIJANA WAJASIRIAMALI NA WATAALAM WA MIRADI MKOA WA SINGIDA |
Hata hivyo mkoa wa SINGIDA ni mkoa wa pili kwa kuzalisha asali nchini
No comments:
Post a Comment