Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Friday, February 7, 2014

MADIWANI WA HALMASHAURI YA IKUNGI WAITAKA SERIKALI KUINGILIA KATI SUALA LA UVAMIZI WA MISITU

Na Evarista Lucas
Singida,
Februali 07,2014


Wajumbe wa baraza la madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wameitaka Serikali ya Mkoa wa Singida; Kulivalia njuga sula la uvamizi haramu katika msitu wa asili wa Minyughe kama ilivyokuwa kwa usala la uuzaji wa mkaa bara barani
Jambo hilo limezungumzwa mapema leo katika  mkutano wa Baraza la madiwani robo ya pili Oktoba hadi Desemba 2013 uliofanyika  katika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida.
Wakionesha kuchoshwa na jambo hilo; wajumbe hao wamesema kuwa suala la uvamizi wa hifadhi ya asili ya msitu wa Minyughe limekuwa kama wimbo katika vikao mbali mbali na kutokujua kama linafanyiwa kazi.
Sanjari na hayo wajumbe hao wameainisha sababu zinazowafanya kupigia kelele hifadhi hizo ni pamoja na uharibifu unaofanywa na wavamizi ambao wanatoka nje ya Mkoa.
Wameongeza kuwa; wavamizi hao wamejenga makazi ya kudumu na kuendesha biashara mbali mbali kinyume na sheria zikiwemo mashine za kusagia hali inayoikosesha Halmashauri kipato.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa baraza hilo la madiwani Halmashauri ya wilaya ya Ikungi na diwani wa kata ya Siuyu; Bwana Sestine Iyunde amewaasa wajumbe wa Baraza hilo  kutokukata tama na  kuwa ni jukumu lao kutetea msitu huo kwa manufaa ya wananchi wao.
Kwa upande wake mkuu wa idara ya ardhi, maliasili na mazingira Bwana Karolius Lukondo amesema; kutokana na uharibifu katika hifadhi ya asili ya  msitu wa Minyughe;  serikali ya kijiji pamoja na wanachi waliingia maridhiano ya kuutunza Msitu huo.
Amesema; awali msitu huo wa Minyughe ambao ulikuwa chini ya usimamizi wa miradi ya kutoka nje ya nchi ikiwemo SIDA na LANP ambayo ilisimamia kikamilifu utunzaji wa misitu hiyo ikiwea ni mwaka 1992 hadi mwaka 2002.
Lukondo amesema kuwa; mara baada ya wafadhili hao kuondoka ndipo hifadhi ilivamiwa na watu kutoka mikoa mingine na haswa Wasukuma ambao wanafanya shughuli za ukulima na kupelekea ukataji wa misitu.
Aidha; Lukondo amezitaja sababu kubwa zinzopelekea makabila ya nje ya Mkoa huu kufanya uvamizi ni kutokana na rasilimali zilizopo katika msitu huo ikiwemo ardhi yenye rutuba.
Kwa upande mwingine lukondo amesema Serikali imeweka mkataba wa makubaliano ya hifadhi ya pamoja msitu wa Minyughe  kati ya vijiji vinavyouzunguka msitu huo na Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi; na kuhuisha kamati za  usimamizi misitu na sheria ndogo.
Sanjari na hayo makubaliano ya taratibu zote za uhifadhi wa misitu huo kuanzia ngazi ya viji,WDC, Baraza la madiwani na Kamati ya ushauri ya Mkoa na mwisho itapelekwa wizara husika na kutangazwa kwenye gazeti la Serikali(GeneralNotice).
Hifadhi ya Msitu wa asili wa Minyughe wenye ukubwa wa hekta 264,600 unazungukwa na vijiji vipatavyo ishirini na visita ambavyo vilipewa jukumu la kuulinda msitu huo ikiwemo Minyughe, Ighombwe, Mtunduru na vinginevyo.
____________________MWISHO____________________
 

Thursday, February 6, 2014

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS FEBRUARI 06, 2014 yapo hapa

Kurasa za mwanzo na mwisho za magazeti ya Tanzania leo Alhamis Februari 06,2014 yapo hapa.Habari kubwa leo Jeshi la Polisi lafanya mabadiliko ya makamanda wa mikoa, Simba yatolewa jasho na Mtibwa










JESHI LA POLISI TANZANIA LAFANYA MABADILIKO

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
Inspekta Jenerali wa jeshi la Polisi(IGP) Ernest Mangu

Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu amefanya mabadiliko ya baadhi ya makamanda wa mikoa, wakuu wa upelelezi wa mikoa, wakuu wa usalama barabarani wa mikoa pamoja na watendaji wengine wa vikosi na vitengo mbalimbali ndani ya Jeshi la Polisi.

Miongoni mwa makamanda wa mikoa waliofanyiwa mabadiliko ni pamoja na aliyekuwa kamanda wa Mkoa wa Ruvuma Kamishna msaidizi mwandamizi (SACP) Deusdedit Nsimeki anayekwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara, Aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara kamishna msaidizi (ACP) Akili Mpwapwa anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma.

Wengine ni aliyekuwa Afisa Mnadhimu mkoa wa Lindi Kamishna msaidizi (ACP) Renatha Mzinga anakuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi, aliyekuwa afisa Mnadhimu Mkoa wa Dodoma Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Suzan Kaganda amehamishwa kwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora na aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora kamishna msaidizi (ACP) Peter Ouma amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi.

Zaidi ya hao wengine waliyohamishwa ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa upelelezi Mkoa wa Mtwara Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Eliyakimu Masenga anakwenda kuwa Mkuu wa upelelezi kikosi cha Tazara, aliyekuwa mkuu wa upelelezi Mkoa wa Tabora Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) David Mnyambuga anakwenda kuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Ilala, na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Ilala, Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Juma Bwire, anakwenda kuwa Afisa Mnadhimu Mkoa wa Tabora .

Aidha, aliyekuwa afisa Mnadhimu mkoa wa Tabora Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) John Kauga anakuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Tabora, aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Rombo (SSP) Mrakibu mwandamizi Ralph Meela anakwenda kuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Mtwara na aliyekuwa Mkuu wa upelelezi wa kikosi cha Tazara Mrakibu wa Polisi (SP) Isack Msengi anakwenda kuwa Kaimu mkuu wa upelelezi mkoa wa Pwani.

Kwa upande wa wakuu wa Polisi wa mikoa wa Usalama Barabarani ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Kinondoni, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Ibrahim Mwamakula ambaye amehamishiwa Trafiki Kanda Maalum Dar es Salaam, aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Mtwara, Mrakibu wa Polisi (SP) Awadh Haji anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Kinondoni, na Mrakibu wa Polisi (SP) Ezekiel Kiko Mgeni aliyekuwa ofisi ya RPC Temeke, anakuwa Mkuu wa Trafiki mkoa wa Temeke.

Wengine ni aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Lindi Mrakibu wa Polisi (SP) James Kiteleki anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Njombe, aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Ilala, Mrakibu wa Polisi (SP) Meloe Buzema anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Lindi, aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Temeke Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Prackson Kibogoyo anakwenda kuwa Mkuu wa Operesheni Mkoa wa Pwani, na aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Njombe, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Chacha Nsaho Maro anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Ilala.

Mabadiliko hayo ni ya kawaida kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi katika kuhakikisha kwamba wananchi wanaendelea kupata huduma bora ya usalama.

Imetolewa na:
Advera Senso-SSP

Msemaji wa Jeshi la Polisi.
_____________________________MWISHO_______________________________

Wednesday, February 5, 2014

MAGAZETI YA LEO JUMATANO, JANUARI 05,2014 yapo hapa

Kurasa za mwanzo na mwisho za magazeti ya Tanzania leo yapo hapa, habari za Siasa, Michezo na Udaku