Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Friday, February 7, 2014

MADIWANI WA HALMASHAURI YA IKUNGI WAITAKA SERIKALI KUINGILIA KATI SUALA LA UVAMIZI WA MISITU

Na Evarista Lucas
Singida,
Februali 07,2014


Wajumbe wa baraza la madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wameitaka Serikali ya Mkoa wa Singida; Kulivalia njuga sula la uvamizi haramu katika msitu wa asili wa Minyughe kama ilivyokuwa kwa usala la uuzaji wa mkaa bara barani
Jambo hilo limezungumzwa mapema leo katika  mkutano wa Baraza la madiwani robo ya pili Oktoba hadi Desemba 2013 uliofanyika  katika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida.
Wakionesha kuchoshwa na jambo hilo; wajumbe hao wamesema kuwa suala la uvamizi wa hifadhi ya asili ya msitu wa Minyughe limekuwa kama wimbo katika vikao mbali mbali na kutokujua kama linafanyiwa kazi.
Sanjari na hayo wajumbe hao wameainisha sababu zinazowafanya kupigia kelele hifadhi hizo ni pamoja na uharibifu unaofanywa na wavamizi ambao wanatoka nje ya Mkoa.
Wameongeza kuwa; wavamizi hao wamejenga makazi ya kudumu na kuendesha biashara mbali mbali kinyume na sheria zikiwemo mashine za kusagia hali inayoikosesha Halmashauri kipato.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa baraza hilo la madiwani Halmashauri ya wilaya ya Ikungi na diwani wa kata ya Siuyu; Bwana Sestine Iyunde amewaasa wajumbe wa Baraza hilo  kutokukata tama na  kuwa ni jukumu lao kutetea msitu huo kwa manufaa ya wananchi wao.
Kwa upande wake mkuu wa idara ya ardhi, maliasili na mazingira Bwana Karolius Lukondo amesema; kutokana na uharibifu katika hifadhi ya asili ya  msitu wa Minyughe;  serikali ya kijiji pamoja na wanachi waliingia maridhiano ya kuutunza Msitu huo.
Amesema; awali msitu huo wa Minyughe ambao ulikuwa chini ya usimamizi wa miradi ya kutoka nje ya nchi ikiwemo SIDA na LANP ambayo ilisimamia kikamilifu utunzaji wa misitu hiyo ikiwea ni mwaka 1992 hadi mwaka 2002.
Lukondo amesema kuwa; mara baada ya wafadhili hao kuondoka ndipo hifadhi ilivamiwa na watu kutoka mikoa mingine na haswa Wasukuma ambao wanafanya shughuli za ukulima na kupelekea ukataji wa misitu.
Aidha; Lukondo amezitaja sababu kubwa zinzopelekea makabila ya nje ya Mkoa huu kufanya uvamizi ni kutokana na rasilimali zilizopo katika msitu huo ikiwemo ardhi yenye rutuba.
Kwa upande mwingine lukondo amesema Serikali imeweka mkataba wa makubaliano ya hifadhi ya pamoja msitu wa Minyughe  kati ya vijiji vinavyouzunguka msitu huo na Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi; na kuhuisha kamati za  usimamizi misitu na sheria ndogo.
Sanjari na hayo makubaliano ya taratibu zote za uhifadhi wa misitu huo kuanzia ngazi ya viji,WDC, Baraza la madiwani na Kamati ya ushauri ya Mkoa na mwisho itapelekwa wizara husika na kutangazwa kwenye gazeti la Serikali(GeneralNotice).
Hifadhi ya Msitu wa asili wa Minyughe wenye ukubwa wa hekta 264,600 unazungukwa na vijiji vipatavyo ishirini na visita ambavyo vilipewa jukumu la kuulinda msitu huo ikiwemo Minyughe, Ighombwe, Mtunduru na vinginevyo.
____________________MWISHO____________________
 

No comments:

Post a Comment