Ajali imetokea leo majira ya saa 11:45 jioni ikihusisha basi la kampuni ya Princes Muro lenye namba za usajili T 989 CDH na gari la mizigo aina ya Canter pia lenye namba za usajili T 348 AFM katika eneo la Jovena , Manispaa ya Singida. Katika ajali hiyo mashuhuda wameieleza
karibusingida blog kwamba ajali hiyo imesababishwa na dereva wa basi la Princes Muro kulipita gari aina ya Canter eneo lisiloruhusiwa pia kuwa katika mwendo kasi uliopitiliza, katika ajali hiyo hakuna majeruhi aliyelipotiwa.
Karibusingida blog inaendelea kuwasiliana na polisi ili kuweza kupata habari zaidi endelea kuwa nasi.
|
Basi la kampuni ya Princes Muro likivutwa kutoka pembeni mwa barabara inayoelekea Mwanza katika eneo la Jovena baada ya kusababisha ajali leo jioni(Picha na Kipamila jrn) |
|
Gari lenye namba za usajili T 348 AFM likiwa limepinduka baada ya kusabishiwa ajali na basi la Princes Muro(Picha na Kipamila jrn) |
|
Basi la kampuni ya Princes Muro likiwa limetoka barabarani.(Picha na Kipamila jrn) |
|
Baada ya kutolewa pembeni mwa barabara basi la Princes Muro likiwa limeharibika sehemu ya mbele.
(Picha na Kipamila jrn) |
|
Mashuhuda wakiangalia gari aina ya Canter likiwa limepindika pembeni ya barabara baada ya kugongwa na basi.
(Picha na Kipamila jrn) |
|
Basi likitolewa pembeni mwa barabara inayoelekea Mwanza kutoka Singida. (Picha na Kipamila jrn) |
|
Basi baada ya kutolewa pembeni mwa barabara. (Picha na Kipamila jrn) |
|
|
___________________________ Mwisho ______________________________
No comments:
Post a Comment