Na Evarista Lucas
Singida
Machi 21, 2014
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Parseko Kone amemshukuru balozi wa watu wa China nhini Tanzania Dk. Lu Youqing; kwa ,kuonesha nia ya kushirikiana naye katika kuleta maendeleo ya Mkoa hasa kusaidia kupata wawekezaji katika mradi wa umeme wa nishati ya upepo.
Katika ziara ya Balozi Youqing na viongozi wengine wachina iliyofanyika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa mapema jana; ilikuwa na lengo la kujadili mipango ya sasa na ya baadae ya kimaendeleo Mkoani hapa na kuona maeneo ya uwekezaji ambayo yatainua pato la Mwananchi.
Dk.Kone amesema; umeme wa upepo hautanufaisha mkoa wa Singida peke yake bali Taifa kwa ujumla kwa kutoa fursa za ajira, ongezeko la viwanda na pia umeme wa uhakika.
Aidha ; Dk.Kone ameongeza kusema kuwa
wawekezaji kutoka China wana fursa mbali mbali za uwekezaji Mkoani
Singida kama vile kilimo na ufugaji na kutilia mkazo uwekezaji katika
mazao ya alizeti, vitunguu, pamba na mpunga.
Sanjari
na hayo Kone ameongeza kusema kuwa licha ya Wananchii wa Mkoa wa
Singida kufuga kuku wa asili ambapo muwekezaji ukifanyika utawaongezea
kipato; Mkoa wa Singida unatoa asali bora nchini.
Amesema;
kutokana na Mkoa kutoa asali bora uwekezaji katika sekta ya aufugaji
nyuki, kiwanda cha uchakataji asali n anta utaongeza thamani ya mazao
hayo.
Kwa
upande wake Balozi Youqing amesema kuwa wawekezaji kutoka China wako
tayari kuwekeza Mkoani Singida na kuwa tayari Kampuni moja kutokam China
imeonesha nia ya ya kutaka kuwekeza katika umeme wa nishati ya upepo.
Pia
Youqing amesisitiza kuwa kutokana na na historia ya ushirikiano mzuri
uliopo kati ya Tanzania na China kwa sasa Sekretarieti za Mikoa na
Serikali za Mitaa zina fursa ya kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mikoa nchini China ili kujifunza teknolojia mbali mbali na kutafuta Kampuni za uwekezaji.
MWISHO
Click here to Reply, Reply to all, or Forward
|
No comments:
Post a Comment