Na, Doris Meghji Jumapili Machi 23,2014
Singida
Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa
Singida (SINGPRESS) imepitisha jumla ya shiling million 39 ikiwa ni bajeti ya
mapato na matumizi katika kipindi cha Januari hadi Disemba mwaka huu
Bwana Nathaniel Limu Mheka hazina
Msaidizi wa klabu hiyo amesoma bajeti ya mapato na matumizi kwenye mkutano mkuu
wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Singida jana katika ukumbi wa mikutano wa Kanisa
katoliki Parokia ya Manyoni wilayani Manyoni mkoa wa Singida
MWANDISHI HALIMA JAMAL KUSHOTO NA KULIA NI EVALISTA LUCAS KWENYE MKUTANO MKUU WA SINGPRESS ULIOFANYIKA WILAYNI MANYONI MACHI 22 MWAKA HUU (PICHA NA DORIS MEGHJI) |
Aidha Mwekahazina huyo msaidizi wa klabu
ya waandishi wa habari ametaja shilingi
600,000/= zinatokana na kiingilio na ada za wanachama wa klabu hiyo toka kwa
wanachama 25 kwa mwaka,shilingi milioni 29 za mafunzo na semina,mkutano mkuu, kawaida
na dharura toka muungano wa klabu za waandishi wa habari Tanzania(UTPC) huku shiling
million 3,600,000/= toka UTPC za mshahara wa mratibu wa klabu hiyo.
Mapato menginie ni shiling million 1,200,000/-
toka mradi wa Internet,shilingi milioni
2,400,000/= kutoka mradi wa kuchapa na kuprint,kukodisha vifaa shilingi milioni
1,200,000/= na fedha toka kwa wahisani mbali mbali ikiwa nis hilingi milioni
1,000,000/=
SEIF TAKAZA MWENYEKITI WA SINGPRESS AKISISITIZA JAMBO WAKATI AKIFUNGA MKUTANO MKUU WA SINGPRESS MWAKA HUU WILAYANI MANYONI MACHI 22(PICHA NA DORIS MEGHJI) |
Kwa mujbu Natahieli Limu amesema klabu hiyo
inatarajia kutumia jumla shilingi miloni 37,584,600/= katika kipindi hicho
cha mwaka, katika matumizi hayo shilingi miloni 5,000,000/= zinatarjiwa kutumika
kwa ajili ya ujezi wa jengo la klabu ya waandishi wa habari mkoani humo.
Hata hivyo wanachama wa klabu ya
waandishi wa habari hiyo wameridhia na kuipitisha bajeti ya mapato na matumizi ya klabu katika
kipindi cha mwezi Januari hadi Disemba mwaka huu kwenye mkutano mkuu huo wa
kawaidi wa mwaka.
Wakati huo huo wanachama wa klabu ya
waandishi wa habari mkoa wa singida wamefanya uchaguzi wa kumchagua Pascal
Ntatau kuziba nafasi ya katibu mtendaji wa klabu ambapo na ameibuka mshindi katika uchaguzi huo mdogo
wa nafasi ya katibu Mtendaji kwa kupata kura 15 za ndio kati ya kura 18
zilizopigwa huku kura (1) mmoja ikiharibika na kura (2) mbili zikiwa za hapana katika uchaguzi huo
mdogo na kutangazwa kuwa katibu mtendaji mpya wa wa klabu hiyo.
Kufanyika kwa uchaguzi huo mdogo kumekuja
mara baada ya Abby Nkungu alikuwa katibu mtendaji wa klabu hiyo kujiuzulu kwa
sababa za maradhi ya kichwa kufuatia upasuaji wa jicho aliofanyiwa mwaka 2009
hivyo kwa kushauriwa na daktari wake toka Nairobi nchini Kenya kumtaka apumzike.
Uchaguzi mkuu wa uongozi wa klabu hiyo unaratajiwa kufanyika mwaka kesho ambapo uongozi mpya wa klabu hiyo utafanyika ikiwa ni moja ya mabadiriko yaliyofanyika kwa klabu zote nchini kutakiwa kufanya chaguzi sambamba na chaguzi za muungano wa klabu za waandishi nchini (UTPC)
Mwisho.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment