Na, Doris Meghji Ijumaa Machi 28,2014
Singida
Mamlaka ya mawasiliano nchini Tanzania
(TCRA) imeagiza watoa huduma za kusambaza ving’amuzi walioko mkoani Singida
kuhakikisha wanakuwa na ving’amuzi vya kutosha imeelezwa.
Akiongea na vyombo vya habari mkoani
Singida Innocent Mungy meneja wa mawasiliano wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) ametoa agizo hilo kwa niaba
ya mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) katikati ya wiki
hii katika ukumbi Utemini ndani ya hoteli ya Katala Beach Resorts manispaa ya
Singida
Agizo hilo limekuja zikiwa zimebaki siku
chache kabla ya uzimaji rasmi wa Mitambo ya kurusha matangazo ya televisheni ya
mfumo wa analojia kuzimwa mkoani hapa.
MWANDISHI AWILA SILLA AKIWA KBH KATIKA KIKAO NA TCRA JUU YA UZIMAJI MITAMBO MFUMO WA ANALOJIA KWENDA DIJITALI MACHI 31 SAA SITA USIKU MKOANI SINGIDA |
Kwa mujibu wa bwana Mungy amesema “tumefanya
ukaguzi katika mji wa Singida na tumehakikisha viko ving’amuzi vya kutosha na
tumehakikishiwa kuwa vingine viko njiani kuja mjini Singida kati ya leo na kesho
ambako zaidi ya ving’amuzi 5000 vitakuwa madukani” alisisitiza Mungy.
MWANDISHI WA HABARI BI EVALISTA LUCAS NA DAMINO MKUMBO KWENYE KIKAO HICHO KBH HOTELI NA TCRA MKOANI SINGIDA |
Katika kufafanua zaidi Meneja
Mawasiliano Mungy amewataka wananchi wa
mkoa huo kuhakikisha wanapataiwa risiti na waranti ya mwaka mmoja ya king’amuzi
chake pale atakapo nunua kinga’muzi hicho kwa wasambazaji na wauzaji wa
ving’amuzi hivyo.
BI MARY MSUYA KATIBU WA BARAZA LA USHAURI LA WATUMIAJI WA HUDUMA ZA MAWASILIANO (TCRACCC) AKIJIBU BAADHI YA MASWALI TOKA KWA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA SINGIDA. |
Aidha Mungy ameeleza na kutaja maeneo
ambao yatahusika na mabadilko hao kuwa ni matangazo kwa njia ya utangazaji wa
Satelaiti, Waya (cable) na radio hivyo
amewataka wananchi wa mkoa wa Singida kutotupa Luninga zao za analojia bali wanunue
ving’amuzi ili kupata matangazo ya dijitali.
Akijibu baadhi ya maswali toka kwa
waandishi wa habari mmoja ya swali kuhusu suala la watu wanaopata matangazo kwa
njia ya satelaitidishi na waya (cable) bwana Mungy amewakikishia wananchi na
wakazi wa mkoa wa singida kuwa kwa wale wote wanaopata matangazo ya televisheni
kwa kutumia madishi na waya kuwa wao hawatahusika na mabadiko hayo ya mfumo wa
analojia kwa kuwa wao wako tayari kidijitali.
Naye Mary Msuya katibu mtendaji wa
baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasilianao (TCRACCC) amewataka
wananchi wa mkoa wa singida kununua ving’amuzi kwa wazambazaji wanaotambulika
na mamlaka hiyo ambao ni Uncle JJ,Msele fashion,Mushi Original,Bei Mpya,Super
Dealers,na Sam electronics ndani ya Manispaa hiyo ya Singida
INNOCENT MUNGY MENEJA WA MAWASILIANO WA TCRA AKIJIANDAA KUTOA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MAANDALIZI YA UZIMAJI WA MITAMBO YA MATANGAZO TELEVISHENI TOKA MFUMO WA ANALOJIA KWENDA DIJITALI. |
Bwana Mungy amezitaja faida za kuhamia
dijitali ni pamoja na muonekano mzuri wa picha za televisheni,ongezeko la vituo vitano vya ndani ya televisheni
kuonekana kuoneka katika mfumo huo ukilinganisha na muonekano wa kituo kimoja
cha televisheni kilichokuwa kikioneka katika mfumo wa analojia ambavyo ni
TBC,STARTV,ITV,Chanel Ten, na EastTV.
Hata hvyo uzimwaji rasmi wa mitambo hiyo ya utangazaji ya mfumo
wa analojia utafanyika Machi 31 saa sita Usiku mwaka huu ikihusisha mkoa wa
Singida na Tabara ikiwa ni awamu ya pili ya uzimaji wa mitambo ya kurushia
matangazo ya analojia nchini Tanzania.
MWISHO
No comments:
Post a Comment