Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Friday, March 21, 2014

CHINA KUWEKEZA MKOANI SINGIDA

Na Evarista  Lucas
Singida
Machi 21, 2014
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Parseko Kone amemshukuru balozi wa watu wa China nhini Tanzania  Dk. Lu Youqing; kwa ,kuonesha nia ya kushirikiana naye katika kuleta maendeleo ya Mkoa hasa kusaidia kupata wawekezaji  katika mradi wa umeme wa nishati ya upepo.




Katika ziara ya Balozi Youqing na viongozi wengine wachina iliyofanyika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa mapema jana; ilikuwa na lengo la kujadili mipango ya sasa na  ya baadae ya kimaendeleo Mkoani hapa na kuona maeneo ya uwekezaji  ambayo yatainua pato la Mwananchi.

Dk.Kone amesema; umeme  wa upepo hautanufaisha  mkoa wa Singida peke yake bali Taifa kwa ujumla kwa kutoa fursa za ajira, ongezeko la viwanda na pia umeme wa uhakika.
Aidha ; Dk.Kone ameongeza kusema  kuwa wawekezaji kutoka China wana fursa mbali mbali za uwekezaji Mkoani Singida kama vile kilimo na ufugaji na kutilia mkazo uwekezaji katika mazao ya alizeti, vitunguu, pamba na mpunga.

Sanjari na hayo Kone ameongeza kusema kuwa licha ya Wananchii wa Mkoa wa Singida kufuga kuku wa asili ambapo muwekezaji ukifanyika utawaongezea kipato; Mkoa wa Singida unatoa asali bora nchini.
Amesema; kutokana na Mkoa kutoa asali bora uwekezaji katika sekta ya aufugaji nyuki, kiwanda cha uchakataji asali n anta utaongeza thamani ya mazao hayo. 

Kwa upande wake Balozi Youqing amesema kuwa wawekezaji kutoka China wako tayari kuwekeza Mkoani Singida na kuwa tayari Kampuni moja kutokam China imeonesha nia ya  ya kutaka kuwekeza katika umeme wa nishati ya upepo.

Pia Youqing amesisitiza kuwa kutokana na na historia ya ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na China kwa sasa Sekretarieti za Mikoa na Serikali za Mitaa zina fursa ya kushirikiana  na Mamlaka za Serikali za Mikoa nchini China ili kujifunza teknolojia mbali mbali na kutafuta Kampuni za uwekezaji.

MWISHO

Saturday, March 15, 2014

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MACHI 15, 2014 YAPO HAPA

Kurasa za mbele za magezeti ya leo ya Tanzania  Machi 15,2014 yapo hapa. Habari kubwa leo Sita mwenyekiti wa Bunge la katiba, Kalenga hapatoshi kati ya CCM na Chadema katika michezo Yanga uso kwa uso na Mtibwa, Van Prese abaki Man U




Monday, March 10, 2014

AJALI TENA SINGIDA

Ajali imetokea leo majira ya saa 11:45 jioni ikihusisha basi la kampuni ya Princes Muro lenye namba za usajili  T 989 CDH na gari la mizigo aina ya Canter pia lenye namba za usajili  T 348 AFM katika eneo la Jovena , Manispaa ya Singida.  Katika ajali hiyo mashuhuda wameieleza karibusingida blog kwamba ajali hiyo imesababishwa na dereva wa basi la Princes Muro kulipita gari aina ya Canter eneo lisiloruhusiwa pia kuwa katika mwendo kasi uliopitiliza, katika ajali hiyo hakuna majeruhi aliyelipotiwa.
Karibusingida blog inaendelea kuwasiliana na polisi ili kuweza kupata habari zaidi endelea kuwa nasi.

Basi la kampuni ya Princes Muro likivutwa kutoka pembeni mwa barabara inayoelekea Mwanza katika eneo la Jovena baada ya kusababisha ajali leo jioni(Picha na Kipamila jrn)
Gari lenye namba za usajili T 348 AFM likiwa limepinduka baada ya kusabishiwa ajali na basi la Princes Muro(Picha na Kipamila jrn)

Basi la kampuni ya Princes Muro likiwa limetoka barabarani.(Picha na Kipamila jrn)

Baada ya kutolewa pembeni mwa barabara basi la Princes Muro likiwa limeharibika sehemu ya mbele.
(Picha na Kipamila jrn)
Mashuhuda wakiangalia gari aina ya Canter likiwa limepindika pembeni ya barabara baada ya kugongwa na basi.
 (Picha na Kipamila jrn)
Basi likitolewa pembeni mwa barabara inayoelekea Mwanza kutoka Singida. (Picha na Kipamila jrn)
Basi baada ya kutolewa pembeni mwa barabara. (Picha na Kipamila jrn)


             ___________________________ Mwisho ______________________________

Wednesday, March 5, 2014

KIKUNDI CHA AMKA CHA WANAWAKE WAFUGAJI NYUKI CHA NUFAIKA NA MIZNGA YA KIASASA TOKA WMO MKOA WA SINGIDA.

KIKUNDI CHA  AMKA CHA WANAWAKE WAFUGAJI NYUKI KIJIJI CHA  ILONGERO WAKISAFISHA MIZNIGA TAYARI KWA KUVUTA NYUKI MIZNGANI \
AFISA  MALIASILI AKITOA MAELEZO JUU YA UNDAAJI WA MZINGA KWA AJILI YA MAKZI YA NYUKI.(PICHA NA DORIS MEGHJI)



Nta ikichemshwa kwa ajilya ya kuandaa mzinga ili nyuki waangie (picha na Doris Meghji)




WMO- NA UTHUBUTU WAO KATIKA KUMWENDELEZA MWANANKE WA SINGIDA

mkuu wa mkoa wa Singfida Dr.  Parseko Kone akihutubia wananchi katika hafla fupi ya kukabidhi mizinga 80 kwa wanawake afugaji nyuki (picha na Doris Meghj)





Bwana Charles Kidua akitoa maelezo juu ya mazinga ya kisasa ya nyuki katika zoezi la upatikanaji wa asali bora kwenye hafla hiyo kwa Mkuu wa mkoa wa Singida DR Parseko Kone picha na Doris Meghji)


Dr. Parseko Kone Mkuu wa mkoa wa Singida akipata maelezo ya mizinga 80 ya kisasa ya wanawake wafugaji nyuki ( picha na Doris Meghji)