Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Wednesday, January 14, 2015

Chama Cha Mapinduzi (CCM) MAAZIMIO YA KAMATI KUU YA CCM -: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.






MAAZIMIO YA KAMATI KUU YA CCM -:
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Jana tarehe 13/01/2015 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa chini ya uongozi wa Mwenyekiti wake wa Taifa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete ilifanya kikao chake cha kawaida cha siku moja Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Pamoja na mambo mengine baadhi ya mambo yaliyojadiliwa na Kamati Kuu ni pamoja na:-
1. SAKATA LA AKAUNTI YA ESCROW.
Chama Cha Mapinduzi kimesikitishwa sana na sakata hili. Baada ya kulijadili kwa muda mrefu na kwa kina Kamati Kuu imeamua yafuatayo:-,
i). Pamoja na yale ambayo yameshatekelezwa na serikali, Kamati Kuu imeitaka serikali na vyombo vinavyohusika kuendelea kutekeleza maazimio ya bunge juu ya swala hilo.
ii). Kamati Kuu imewataka wote wanaopewa dhamana wajenge utamaduni wa kuwajibika kwa dhamana zao, na wasipowajibika waliowapa dhamana wachukue hatua za kuwawajibisha.
iii). Aidha Kamati Kuu imeiagiza Kamati Ndogo ya Maadili kuchukua hatua za kimaadili kwa wale wote waliohusika na ukiukwaji wa maadili kwenye sakata la Escrow na wako kwenye vikao vya maamuzi vya Chama. Kikao cha Kamati Ndogo ya Maadili kitafanyika tarehe 19/01/2015 kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo.
2. WALIOPEWA ADHABU KWA KUKIUKA MAADILI YA CHAMA.
Itakumbukwa kuna makada sita wa CCM walipewa adhabu kwa kuhusishwa na ukiukwaji wa maadili kwenye mchakato wa kutaka kuteuliwa na CCM kugombea urais, watamaliza muda wa adhabu zao mwezi wa pili mwaka 2015.
Baada ya muda wa adhabu zao kuisha, itafanyika tathimini kuona kama walizingatia mashariti ya adhabu zao. Na kama kuna ambao watakutwa hawakuzingatia mashariti ya adhabu zao wataongezewa adhabu.
3. SOKO LA MAHINDI.
Kamati Kuu imepokea taarifa ya mwenendo wa soko la mahindi nchini. Baada ya tathimini na uchambuzi, pamoja na kazi iliyofanywa na serikali, Kamati Kuu imeiagiza serikali kuangalia upya mfumo unaotumiwa na Hifadhi ya Taifa ya Chakula ( NFRA)katika ununuzi wa mahindi, ili unufaishe zaidi wakulima badala ya utaratibu wa sasa ambao kwa kiasi kikubwa unanufaisha zaidi mawakala badala ya wakulima moja kwa moja.
4. RATIBA YA VIKAO VYA CHAMA.
Kamati Kuu imepitisha ratiba ya shughuli mbalimbali za Chama kwa mwaka 2015.Aidha ratiba ya mchakato wa kuwapata wagombea wa CCM ndani ya dola utapangwa na vikao vijavyo vya Chama.
Nape Moses Nnauye
CCM Secretary for Ideology & Publicity.

Saturday, January 10, 2015

WANANCHI WA KATA A SANZA WALIA KWA KUKOSA MAWASILIANO YA MITANDAO YA SIMU LICHA YA WAO KUMILIKI SIMU ZA VIGANJANI - IMEFAHAMIKA

Na, Doris Meghji Ijumaa Janauri 09, 2015
Manyoni Singida.

Ukosefu wa mawasiliono miongoni mwa  wananchi wa kata ya Sanza,vijiji na vitongoji vyake imekuwa kero  kwa wananchi ya kata hiyo wilayani Manyoni
Shule ya msingi Sanza halmashauri ya wilaa ya Manyoni (Picha na Doris Meghji)


Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi wa kijiji cha Ikasi kata ya sanza wameziomba kampuni za simu nchini kuwekeza katika kata hiyo na vijiji vyao kwa kujenga minara ya mawasilino ili nao waweze kufurahia huduma kama ilivyo kwa maeneo mengine nchini.
Wananchi wa kata ya Sanza katika ofisi ya mtendaji wa kata hiyo (picha na Doris Meghji)

Kilio hicho cha kuhitaji huduma ya Mawasilino kinakuja pale wananchi hao wakipata shida ya kutunza siri zao za mawasiliono pindi wanapokutana eneo mmoja kwa ajili ya kupata mitandao ya mawasiliano eneo la umbali wa  kilomita mbili kutoka kijiji husika.
Mmoja wa wakina mama wa kata ya Sanza wakiwa na baadhi ya wazee wa kata hiyo katika ofisi ya Mtendaji kata ya Sanza(Picha na Doris Meghji)


Kwa mujibu wa sensa watu na makazi  kijiji hicho cha Ikasi kina wakazi takribani  elfu mbili na hamsini kikiwa ni kijiji kimoja kati ya vijiji vinne vinavounda kata ya sanza.
Baadhi ya wananchi wa kata ya sanza wakiwa kwenye ofisi a mtendaji wa kata hiyo na kilio chao cha kukusa mawasiliano ya mitandao ya Simu (picha na Doris Meghji)
Shughuli kuu ya kiuchumi kwa wananchi hao wa Sanza ni Kilimo cha ufuta,alizeti,mahindi na mtama.


Mwisho

Friday, January 2, 2015

DED - IRAMBA BI HALIMA HANJALI PETER ANUSURIKA KULIPULIWA NA BOMU NYUMBANI KWAKE LEO

Na, Doris Meghji Ijumaa Januari 02,2015
Singida

Kitu kinachodhaniwa ni bomu liliotengezwa kienyeji  kimeripuka leo majira ya saa 1:15 asubuhi na kusababisha madhara  eneo la kiomboi tarafa ya Kisiriri wilaya ya Iramba mkoani Singida
Kamanda wa jeshi la polisi  Mkoa wa Singida ACP Thobias Sedoyeka akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya Tukio hilo la mlipuko wa bomu .

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP THOBIAS SEDOYEKA amesema tukio hilo la mlipuko huo wa bomu  limetokea majira ya saa mmoja na dakika kumi na tano za asubuhi nyumbani kwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Iramba Bi Halima Hanjali Peter mwenye umri wa miaka 47  kwa kutoboa godoro la spring kiasi cha nusu nchi kwenda chini na upana wa nchi mbili.
Mwandishi wa habari Nathaniel Limu na afisa habari wa jeshi la polisi Shabani Msangi akiwa taari kumsikiliza kamanda wa jeshi la polisi kutoa taarifa kwa vyombo vya habari.(Picha na Doris Meghji)

Aidha amesema kitu hicho ambacho kilikuwa kimewekwa katika bahasha iliyopelekwa kwa Mkurugenzi huyo wa Iramba kutoka kwa katibu mhutasi wake  siku ya Jumanne tarehe 30 mwaka 2014 majira ya saa nne asubuhi ambapo ndani yake kulikuwa na kadi ya kumpongeza ambayo ilikuwa na kikaratasi chenye ujumbe uliosema “poleni sana hatuwezi kufanya dili la milioni tisini halafu mkala peke yenu sisi mkatudhulumu tukawaacha”

Waandishi wa habari wakipata taarifa toka kwa kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida.(Picha na Doris Meghji )


Kwa mujibu wa kamanda Sedoyeka amesema mkurugenzi huyo alipokuta ujumbe huo ,aliamua kwenda na bahasha hiyo nyumbani kwake bila kujua kuna kitu kingine ndani yake.hivyo ilivyofika siku ya tarehe mbili mwezi wa kwanza mwaka 2015 saa moja na robo asubuhi akiwa anajiandaa wakati ameiweka bahasha hiyo juu ya kitanda chake ili  kutoka nayo kitu kilichokuwa ndani ya bahasha hiyo kililipuka kwa kishindo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakipata kiburudisho cha soda ofisi ya kamanda wa po;isi mkoa wa Singida(picha na Doris Meghji)


Hata hivyo hakuna watu wanaoshikiliwa kwa tukio hilo na hakuna mtu aliyejeruhiwa isipokuwa kuchanika kwa gondoro na shuka lililokuwa limetandikwa katika godoro kitanda cha mkurugenzi huyo.

Jeshi la polisi kwa ushirikiano na wataalamu toka jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) na wataalam wa milipuko watafanya uchunguzi wa kitu hicho.

Jeshi la polisi linaendelea na upelelezi ili kumpata mtu aliyeitoa ile barua kwa hatua za uchunguzi zaidi.
MWISHO.





Friday, December 12, 2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - PATA TAARIFA JUU YA TEUZI ZA TAASISI ZA UMMA ALIZOFANYA MH.RAIS JAKAYA KIKWETE

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bi. Katarina Tengia Revocati kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani kuanzia tarehe 5 Desemba, 2014. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Desemba 11, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, imesema kabla ya uteuzi huo, Bi. Revocati alikuwa Msajili wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Biashara.

Vilevile katika Taarifa hiyo, Rais Kikwete pia amemteua Bwana Rugalema J. Kahyoza kuwa Msajili wa Mahakama Kuu kuanzia tarehe 5 Desemba, 2014. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Kahyoza alikuwa Hakimu Mwandamizi Msaidizi, Mahakama Kuu, Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Menejimenti na Mashauri.

Katika hatua nyingine, Rais Kikwete amemteua Dkt. Fidelice Mafumiko kuwa Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kuanzia tarehe 4 Desemba, 2014. Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Mafumiko alikuwa Naibu Mkuu TEWW.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu Dar es Salaam.
11 Desemba,2014

Tuesday, December 9, 2014

PITIA KURASA ZA MBELE NA NYUMA ZA MAGAZITI YA LEO TAREHE 09 DISEMBA 2014

PATA KURASA ZA MBELE NA NYUMA ZA MAGAZETI YA LEO TAREHE 09,DISEMBA 2014.



























 





NAKUTAKIA MIAKA 53 YA UHURU WA TANGANYIKA MWEMA MUNGU AWABARIKI WAPENDWA WTE WA KARIBU SINGIDA BLOGSPOT.

LEO TANZANIA BARA INAADHIMISHA NA KUSHEREHEKEA MIAKA 53 YA UHURU





Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiinua juu bango  likionyesha sasa Tanganyika Huru toka kwa mkoloni  mwaka 1961.



Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Baba wa Taifa letu akiwasili uwanja wa Uhuru jijini Dare- es salaam  mwaka 1961 akiungana na wananchi wa Tanganyika kusherehekea sikukuu ya Uhuru miaka 53 iliyopita. 




Friday, November 28, 2014

ZIKIWA ZIMEBAKI SIKU CHACHE KUMALIZIKA KWA ZOEZI LA KUANDIKISHA WANANCHI KATIKA DAFTARI LA WAPIGA KURA - KWENYE UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014


ZOEZI LA KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUPIGA KURA KWA AJILI YA CHAGUZI ZA SERIKALI ZA MITAA - MANISPAA YA SINGIDA.

Baadhi ya wananchi wa mtaa wa Stesheni kata ya Utemini  - ndani ya manispaa ya Singida waliojitokeza leo katika kituo cha Sido kwa ajili ya kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura - kwa ajili ya kuchagua viongozi wa serikali za mitaa inayotarajiwa kufanyika mwezi Disemba mwaka huu (picha na Doris Meghji)




Bi Angelina Mwagoa Karani mwandikishaji wa daftari la kupiga kura Kituo cha SIDO kwa ajili ya wananchi wa mtaa wa Stesheni - Kata ya Utemini Manispaa ya Singida.(picha na Doris Meghji)



Kushoto ni Ally Mtinange Muna wakala wa CCM akiwa kwenye kituo cha kuandikisha wananchi kwenye daftari la kupigia kura ya kumchagua kiongozi wa serikali za mitaa kataika uchaguzi utakofanyika mwezi ujao lengo likiwa ni kufanya utambuzi wa wananchi wanaoishi mtaa wa Stesheni akiwa pamoja na Betha Kawelega mwananchi wa mtaa huo wa stesheni aliyekuja kujiandikisha.(picha na Doris Meghji)


Ratiba ya siku za kujiandikisha katika zoezi hio la kujindikisha katika daftari la kupiga kura za kuchagua viongozi wa serikali za mitaa- unaotarajiwa kufanyika mwezi Disemba mwaka.(picha na Doris Meghji)


 Innocent Ahonga -karani wa waandikishaji wananchi kwenye daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa akimsainisha mmoja wa wananchi waliofika katika kituo cha shule ya msingi utemini - Mtaa wa Utemini kata ya Utemini -Manispaa ya Singida mara baada ya kumuandikisha jina lake.(picha na Doris Meghji)


Mmoja wa wananchi wa mtaa wa utemini aliyefika katika kituo cha shule ya msingi Utemini akisainishwa kwenye daftari la kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa kuchagua viongozi wa serikali za mitaa mara baada ya kujazwa taarifa yake  karani Innocent Ahonga wa kituo cha utemini mtaa wa utemin.(picha na Doris Meghji)


Kijana Innocent Ahonga akitoa maelezo juu ya changamoto mbali mbali zilizojitokeza katika zoezi hilo la uandikishaji wananchi kwenye daftrai la wapiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Disemba 2014.(picha na Doris Meghji)

Karani Ahonga amezitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na mwitikio mdogo wa wananchi kujitokeza kujiandikisha katika mtaa huo wa utemini hadi kufikia majra ya saa nane mchana leo ameandikisha jumla ya wanaanchi 180.

Suala mawakala wa vyama vya siasa limeonnekana ni changamoto nyingine katika utambuzi wa wananchi wa mtaa huo wa utemini hivyo katika kituo hicho  karani Ahonga ameandikisha wananchi hao kwa kuzingatia vitambulisho vya kupigia kura ili kumtambua mwananchi wa mtaa huo.

Ukiwa mwitikio bado ni mdogo hivyo ameshauri tabia ya kutoa elimu kwa umma kwa viongozi wa serikali za mitaa wapite na kuwahabarisha watu ili waweze kufika katika vituo vya kujiandikisha kupiga kura na wananchi mmoja kwa mmoja anyefika katika kituo hicho amuhabarishe na mwingine ili watu wafike kwenye kituo na kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura ili wafanye haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wao wa serikali za mitaa.

Kwa upande wake Angelina Mwagoa karani wa kito cha SIDO mtaa wa stesheni kata ya utemini amesema mkanganyiko wa wananchi kuja kujiandikisha kwa lengo la kupatiwa vitambulisho vya taifa limejitokeza kwa wananchi wa mtaa huo hivyo ametoa ushauri kwa manispaa kutoa tangazo na kuelimisha watu juu ya zoezi hilo ili watu waelewe na kujitokeza kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao

Kuhusu suala la malipo ya posho za makalani hao ndani ya manispaa ya Singida kwa malipo ya shilingi 10,000/= kwa siku  kiasi hicho cha malipo  kimeonekani ni changamoto kwa baadhi ya makarini wa uandikishaji wa daftari hilo ambapo hadi siku ya jana wamelipwa jumla ya shilingi 30,000/= tangu zoezi hilo lianze  siku Jumapili  tarehe 23 mwezi huu .

Zoezi hilo linatarajiwa kukamilika siku ya Jumamosi Novemba 29 mwaka huu majira ya saa 10:00 jioni.
MWISHO