Na,
Doris Meghji Ijumaa Janauri 09, 2015
Manyoni
Singida.
Ukosefu
wa mawasiliono miongoni mwa wananchi wa
kata ya Sanza,vijiji na vitongoji vyake imekuwa kero kwa wananchi ya kata hiyo wilayani Manyoni
Shule ya msingi Sanza halmashauri ya wilaa ya Manyoni (Picha na Doris Meghji) |
Wakiongea
kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi wa kijiji cha Ikasi kata ya sanza
wameziomba kampuni za simu nchini kuwekeza katika kata hiyo na vijiji vyao kwa
kujenga minara ya mawasilino ili nao waweze kufurahia huduma kama ilivyo kwa
maeneo mengine nchini.
Wananchi wa kata ya Sanza katika ofisi ya mtendaji wa kata hiyo (picha na Doris Meghji) |
Kilio
hicho cha kuhitaji huduma ya Mawasilino kinakuja pale wananchi hao wakipata
shida ya kutunza siri zao za mawasiliono pindi wanapokutana eneo mmoja kwa
ajili ya kupata mitandao ya mawasiliano eneo la umbali wa kilomita mbili kutoka kijiji husika.
Mmoja wa wakina mama wa kata ya Sanza wakiwa na baadhi ya wazee wa kata hiyo katika ofisi ya Mtendaji kata ya Sanza(Picha na Doris Meghji) |
Kwa
mujibu wa sensa watu na makazi kijiji
hicho cha Ikasi kina wakazi takribani elfu mbili na hamsini kikiwa ni kijiji kimoja
kati ya vijiji vinne vinavounda kata ya sanza.
Baadhi ya wananchi wa kata ya sanza wakiwa kwenye ofisi a mtendaji wa kata hiyo na kilio chao cha kukusa mawasiliano ya mitandao ya Simu (picha na Doris Meghji) |
Shughuli kuu ya kiuchumi kwa wananchi hao wa Sanza ni Kilimo cha ufuta,alizeti,mahindi na mtama.
Mwisho
No comments:
Post a Comment