Na, Doris Meghji Ijumaa Januari 02,2015
Singida
Kitu kinachodhaniwa ni bomu
liliotengezwa kienyeji kimeripuka leo
majira ya saa 1:15 asubuhi na kusababisha madhara eneo la kiomboi tarafa ya Kisiriri wilaya ya
Iramba mkoani Singida
Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Singida ACP Thobias Sedoyeka akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya Tukio hilo la mlipuko wa bomu . |
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP THOBIAS SEDOYEKA amesema tukio
hilo la mlipuko huo wa bomu limetokea
majira ya saa mmoja na dakika kumi na tano za asubuhi nyumbani kwa mkurugenzi
wa halmashauri ya wilaya ya Iramba Bi Halima Hanjali Peter mwenye umri wa miaka
47 kwa kutoboa godoro la spring kiasi
cha nusu nchi kwenda chini na upana wa nchi mbili.
Mwandishi wa habari Nathaniel Limu na afisa habari wa jeshi la polisi Shabani Msangi akiwa taari kumsikiliza kamanda wa jeshi la polisi kutoa taarifa kwa vyombo vya habari.(Picha na Doris Meghji) |
Aidha amesema kitu hicho ambacho
kilikuwa kimewekwa katika bahasha iliyopelekwa kwa Mkurugenzi huyo wa Iramba
kutoka kwa katibu mhutasi wake siku ya
Jumanne tarehe 30 mwaka 2014 majira ya saa nne asubuhi ambapo ndani yake
kulikuwa na kadi ya kumpongeza ambayo ilikuwa na kikaratasi chenye ujumbe
uliosema “poleni sana hatuwezi kufanya
dili la milioni tisini halafu mkala peke yenu sisi mkatudhulumu tukawaacha”
Waandishi wa habari wakipata taarifa toka kwa kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida.(Picha na Doris Meghji ) |
Kwa mujibu wa kamanda Sedoyeka amesema
mkurugenzi huyo alipokuta ujumbe huo ,aliamua kwenda na bahasha hiyo nyumbani
kwake bila kujua kuna kitu kingine ndani yake.hivyo ilivyofika siku ya tarehe
mbili mwezi wa kwanza mwaka 2015 saa moja na robo asubuhi akiwa anajiandaa wakati ameiweka bahasha hiyo juu ya kitanda chake ili kutoka nayo kitu kilichokuwa ndani ya bahasha hiyo kililipuka kwa kishindo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakipata kiburudisho cha soda ofisi ya kamanda wa po;isi mkoa wa Singida(picha na Doris Meghji) |
Hata hivyo hakuna watu wanaoshikiliwa
kwa tukio hilo na hakuna mtu aliyejeruhiwa isipokuwa kuchanika kwa gondoro na shuka lililokuwa limetandikwa katika godoro kitanda cha mkurugenzi huyo.
Jeshi la polisi kwa ushirikiano na wataalamu toka jeshi la
wananchi Tanzania (JWTZ) na wataalam wa milipuko watafanya uchunguzi wa kitu
hicho.
Jeshi la polisi linaendelea na upelelezi
ili kumpata mtu aliyeitoa ile barua kwa hatua za uchunguzi zaidi.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment