Wednesday, May 20, 2015
Monday, May 18, 2015
WAGOMBEA WA NAFASI ZA UONGOZI MKALAMA WAONYWA KUTOCHAFUANA KTK KIPINDI HIKI
Na,Jumbe Ismailly -Mkalama May,18,2015 Kuchafuana
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Mkalama kimekemea tabia ya baadhi ya wanachama wake wenye nia ya kutaka kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi mkuu ujao wa Rais,wabunge na madiwani baadaye mwaka huu kuacha mara moja kuanza kuwachafua viongozi waliopo madarakani.
Onyo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Mkalama,Elipendo Machafuko alipokuwa kifungua kikao cha baraza la jumuiya hiyo wilayani Mkalama,mara tu baada ya kumpokea Mbunge wa viti maalumu (CCM) Mkoa wa Singda,Mather Mlata aliyekuwa na ziara ya siku moja wilayani hapa.
Kwa mujibu wa Machafuko wakati wakielekea kwenye uchaguzi mkuu mwezi oktoba,mwaka huu kumeanza kujitokeza wingu la watu wenye nia ya kugombea nafasi za uongozi kuanza kuwachafua viongozi waliopo madarakani,jambo ambalo linaweza kuleta mfarakano ndani ya chama.
“Tunaenda kwenye mchakato wa uchaguzi,liko wingu la kuchafuana sanaa..kama unamchafua Mather Mlata bado yupo madarakani,hivi wewe ukichafuliwa utafurahi,utatabasamu,ukimchafua mwenyekiti wa Halmashauri wakati bado anatawala kule Halmashauri atafurahi,iko hii tabia,ipoo?alihoji mwenyekiti huyo wa UWT Mkalama.
Akizungumza na wajumbe wa baraza la UWT wilaya ya Mkalama,Mbunge wa viti maalumu (CCM) Mkoa wa Singida,Marther Moses Mlata alisema demokrasi ndani ya Chama Cha Mapinduzi ni ya kujivunia sana kwani inampa nafasi kila mwanachama kugombea,kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi yeyote ya uongozi.
“Jamani ndani ya chama cha mapinduzi kuna demokrasia,simmeona watu wengine demokrasia hamna sasa hivi tu mnyukano,sisi kuna demokrasia inapofika wakati watu wanajitokeza ili watu wawapime,watu wachaguliwe”alisisitiza Mlata
Hata hivyo Mlata ambaye pia ni mjumbe wa Baraza la UWT Taifa aliwaweka wazi wanachama wa jumuiya hiyo kuwa yeyote yule mwenye nia na uwezo wa kuwatumikia wananchi wa Mkoa huo wakati ukifika wajitokeze kuchukua fomu na kujaza ili waombe nafasi zitakazotangazwa na chama.
Naye katibu wa UWT Mkoa wa Singida,Angela Robert Milembe alitumia fursa hiyo kuwatahadharisha watendaji wa jumuiya hiyo kwamba msaada wa vitendeakazi vilivyotolewa na Mbunge Mlata visije vikawa chanzo cha kuwafarakanisha na badala yake viwazidishie umoja na mshikamano zaidi.
Awali katibu wa CCM wilaya ya Mkalama,Amosi Shimba akimkaribisha Mjumbe huyo wa Baraza la UWT Taifa aliwahakikishia wajumbe na wanachama wa chama hicho kwamba misaada hiyo iliyotolewa na mbunge huyo siyo rushwa bali anatekeleza ilani ya chama tawala.
“Kwa sababu mbunge aliyepo madarakani anayoyafanya siyo rushwa,niombe kutoa wito kwa viongozi wengine mliopo madarakani,msipate kigugumizi,msisite,kukisaidia chama kijipange kujiandaa kwenda kwenye mchakato,mama Mlata kila la kheri”alisisitiza huku akishangiliwa na wajumbe waliohudhuriaa kikao hicho.
MWISHO.
ZIARA YA MBUNGE WA VITI MALUM CCM MKOA WA SINGIDA -MH. MARTHA MOSSES MLATA - WILAYA YA MKALAMA
![]() |
| Ni Baadhi ya wajumbe wa Baraza la UWT wilaya ya Mkalama waliohudhuria kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa ofisi za Chama Cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Mkalama. |
Ni Baadhi ya pikipiki zilizokabidhiwa kwa wenyeviti wa wilaya wa UWT katika Mkoa wa Singida kwa lengo la kuwarahisishia suala la usafiri.PICHA zote Na,Jumbe Ismailly.
![]() |
| Ni Mbunge wa viti maalumu (CCM) Mkoa wa Singida,Bi Marther Mosses Mlata(wa kwanza kulia)akiwakabidhi makatibu wa matawi ya jumuiya ya UWT baiskeli moja kwa kila kata. |
Ni Katibu wa UWT Mkoa wa Singida,Bi Anjela Robert( wa kwanza kushito) akimuelekeza mbunge wa viti maalumu (CCM) Mkoa wa Singida,Bi Marther Mosses Mlata(wa pili kutoka kulia) akimshauri kuonyesha zawadi aliyowapelekea wanachama wa jumuiya hiyo.Wengine ni Bi Christina S.Hamisi(wa kwanza kulia),Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Mkalama,Bi Elipendo Machafuko(wa tatu kutoka kulia) na mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Iramba,Bi Jenifer Miano(wa pili kutoka kushoto)
(PICHA ZOTE NA JUMBE ISMAILY)
Wednesday, May 13, 2015
BENKI YA POSTA KUPELEKA HUDUMA MIKOANI
Benki
ya Posta yajizatiti kupeleka huduma mikioani
Na
Johnson Soah, Singida
May
13, 2015
Benki ya Posta Tanzania (TPB)imejizatiti kupeleka
huduma mikoani ambapo jana Maya 11 mwaka huu imefungua tawi jipya mkoani
Singida, ikiwa ni ishara ya kuleta ushindani mkoani hapa.
Akizungumza katika hafla hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi amesema
kuwa benki hiyo imejipanga kuimarisha huduma zake kwa kufungua matawi mengi ili
kuhakikisha wakazi wengi wanajiunga na benki hiyo.
“Kwa kutambua mahitaji ya wananchi tumejipanga
kuimarisha huduma zetu kwa kufungua matawi mengi nchi nzima na leo mmeona
tumefungua tawi jipya hapa, hivyo ni fursa kwenu wakazi wa mkoa huu na mfanye
hima kuichangamkia”. Alisema.
Naye mwanyekiti wa bodi ya benki hiyo Profesa
Lettice Rutashobya amesema kuwa ni vyema wananchi kutambua kuwa benki ya posta
ni benki ya Watanzania, hivyo ni wajibu wao kujiunga na Benki yao.
“Wakazi wa Mkoa huu na Watanzania kwa Ujumla, hii ni
benki yenu ya kitanzania hivyo ni wajibu wenu kujiunga kwani gharama zake ni
nafuu”. Alisisitiza.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Singida, Bw.
Saidi Ally Amanzi amewahimiza wananchi mkoani Singida Kuwa na moyo wa kupenda
,kuthamini na kujivunia benki yao kuliko kuthamini vitu kutoka nje,
“ Hii ni benki yenu, wananchi kuweni na moyo wa kupeinda, kujivunia na kuithamini”.
Alisema Bw. Amanzi huku akionesha msisitizo huku akihimiza kupunguza gharama
zake ili kuvutia wateja wengi zaidi.
Benki ya Posta Tanzania ina matawi ishirini na nane
na mengine madogo madogo 21 na Akaunti 188 nchi nzima.
Sunday, May 10, 2015
TTCL YAOMBWA KUANZISHA HUDUMA YA KUTUMA NA KUPOKEA PESA KWA NDIA YA MTANDAO WA SIMU -CHEMBA
Na,
Doris Meghji Jumapili Mei 10, 2015
Kijiji
cha Ovada Wilaya ya Chemba –Dodoma
| Mnara wa simu ya kampuni ya TTCL uliojengwa kijiji cha Ovada wilaya ya Chemba mkoa wa Dodoma (Picha na Doris Meghji) |
Kampuni
ya simu Tanzania TTCL imeombwa kuanzisha huduma ya TTCL PESA ili kuwasaidia wanachi kutuma na kupokea pesa katika
maeneo ambayo mtandao huo unapatikana kwa uhakikika kama mitandao mingine ya
simu nchini inavyofanya.
Wananchi
wa kijiji cha OVADA wilaya ya Chemba wametoa ombi hilo kwa kampuni hiyo ya simu
kwenye uzinduzi rasmi wa mnara wa simu uliyojengwa katika kijiji hicho chini mradi
wa kupeleka mawasiliano vijijini kupitia mfuko wa (UCSAF) kwa kuiomba kampuni
hiyo ya simu kuanzisha huduma hiyo ya kutuma na kupokea pesa kwa njia ya simu
kwa kuwa TTCL ndio mtandao pekee
unaopatikana kwa uhakika kijijini hapo
| Meneja waTTCL mkoa wa Singida akitamnulisha wageni katika kijiji cha OVADA kwenye uzinduzi rasmi wa mnara wa mawasilino ya TTCL wilayani Chemba (Picha na Doris Meghji) |
Wakiongea
na blog hii kwa nyakati tofauti bi Garce Vicent mkazi wa Kijiji cha Ovada na
bwana Chilomoto Muyuesegu wameishukuru kampuni hiiyo ya simu kwa kujenga mnara
kijijini hapo kwa kuwarahisha mawasiliano kwa kuwa sasa hawana haja ya kupanda
miti na milima ili kupata mtandao wa simu kwenye kufanya mawsiliano.
“ombi
letu kwa TTCL ni kutuletea huduma ya TTCL pesa ili tuweze kuwatumia au kupkea
pesa kwa njia ya simu kama mitandao mingine,ili isitulazimu kuwa na simu zenye
line ya mitandao mengine tukitaka kufanya hivyo walisema wakazi hao”
| Baadhi ya watumishi wa kampuni ya simu ya TTCL mkoa wa Singida wakimsikiliza mgeni rasmi katika Hafla hiyo ya kuzindua mnara wa mawasilino ya simu kijiji cha OVADA (Picha na Doris Meghji) |
| wananchi wa kijiji cha OVADA wakiwasiliza viongozi wao katikahafla yauzinduzi rasmi wa mnara wa mawasiliano ya simu ya kampuni ya TTCL (Picha na Doris Meghji) |
Kwa
upande wa meneja mkuu wa kanda ya
kaskazini ya kampuni hiyo TTCL Brown Japhet ambaye anasimamia mkoa wa Kilimanjaro,Arusha,Tanga,Manyara
na Singida amesema uzinduzi wa mnara huo unalenga kuhudumia zaidi ya vijiji
saba katika wilaya ya Chemba ambavyo ni Ovada,Baaba,Jogolo,Dinae Mengu,Takwa na
Kinyamshindo vyenye wakazi zaidi ya kumi na tano elfu wenye kugharibu takribani
shilingi milioni 51,300,000/=
Aidha
amewaomba wananchi wa vijiji hivyo kutunza na kulinda miundo mbinu ya mnara huo
ambao unawapatia mawasiliano kwa kuunga mkono jitihada za serikali kuhakikisha
upatikanaji wa mawasilino kwa urahisi zaidi kwa kuchangia ukuaji wa maendeleo
katika maeneo ya vijijini.
| Mh. Diwani Pius Majengo wa kata ya OVADA Akihutubia wananchi wa kikiji cha Ovada katika uzinduzi rasmi wa mnara wa mawasilino ya simu ya TTCL (Picha na Doris Meghji) |
Naye
Diwani wa kata hiyo ya OVADA bwana Pius Majengo kwa niaba ya mgeni rasmi Mkuuwa wilaya ya Chemba ametoa taadhari kwa wananchi wa kijiji na kata
hiyo kutumia fursa hiyo ya mawasilino ya TTCL kutumia vizuri kwa kupeana
taarifa na sio kwa matumizi mengine ya kutukana nana au laa kwa kuwa na
mawsiliano kusilete matatizo miongoni mwao.
Ujenzi
wa mnara huo ulianza rasmi Februari mwaka 2014 na uzinduzi kufanyika MEI 07
MWAKA HUU.
| Kwayaya parokia ya OVADA ikitumbuiza katika hafla ya uzinduzi wa mnara wa kampuni ya TTCL wilaya ya Chema mkoa wa Dodoma(Picha na Doris Meghji) |
| Mjumbe wa bodiya shule ya Sekondari akipokea mmoja ya simu iliyotolewa na Kampuni ya SIMU ya TTCL katika uzinduzi rasmi wa manara wa simu katika kijiji cha OVADA (Picha na Doris Meghji) |
MWISHO.
Friday, April 24, 2015
Thursday, March 19, 2015
Subscribe to:
Posts (Atom)
.jpg)

.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)