Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Saturday, February 22, 2014

MAGAZETI YA LEO FEBRUARI 22, 2014 YAPO HAPA

KURASA ZA MWANZO NA MWISHO ZA MAGAZETI YA LEO YA TANZANIA FEBRUARI 22, 2014 YAPO HAPA, HABARI KUBWA LEO WABUNGE WA BUNGE LA KATIBA WAOMBA KUONGEZEWA POSHO, UFAULU KIDATO CHA NNE JUU KATIKA MICHEZO LIGI KUU TANZANIA BARA KUTIMUA VUMBI LEO.



Wednesday, February 19, 2014

APOTEZA MAISHA BAADA YA KUPIGWA JIWE KICHWANI

Na Evarista Lucas
Singida,
Feb  19,2014

Mkulima  na mkazi wa kijiji cha Unyanga kata ya Mungumaji Mkoani Singida Bwana Petro Soghwenda (86);  amepoteza maisha nyumbani kwake akiwa katika harakati za kupelekwa hospitali mara baada ya kupikwa jiwe sehemu za kichwani.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari mapema leo; Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani  Singida  ASCP  Geofrey Kamwela amesema kuwa; marehemu Soghwenda alipoteza maisha siku ya tarehe 18.02.2014 baada ya kushambuliwa na Maria Daudi (16) ambaye pia ni mkulima na mkazi wa Unyanga.

 Aidha; Kamanda Kamwela amesema kuwa  katika uchunguzi wake wa awali, Jeshi la polisi mkoani hapa limebaini kuwa mtuhumiwa ana tatizo la akila na ugonjwa wa kifafa.

Ameongeza kuwa chanzo cha tuko hilo bado hakijafahamika lakini mtuhumiwa  Maria Daudi  anashikiliwa na jeshi la polisi mpaka pale uchunguzi utakapo kamilika na mtuhumiwa kufikishwa makamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

 Mwili wa Marehemu Petro  Soghwenda umehifadhiwa katika hospitali ya Mkoa wa Singida.

MWISHO

KUKAMILISHA UJENZI WA VYUMBA VYA MAABARA SEKONDARI ZA KATA

Na Evarista Lucas
Singida,
feb 19,2014

Mkuu wa wilaya ya Singida   Mheshimiwa Queen Mlozi amezitaka kata ambazo hazijakamilisha ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara katika shule za sekondari za kata kukamilisha ujenzi huo mara moja.

Akihutubia baraza la madiwani katika kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Singida mapema leo; Mlozi amesema kuwa hatosita kuwachukulia hatua kali na za kisheria madiwani na watendaji wote ambao hawajakamilisha ujenzi wa vyumba hivyo.

Amesema; shughuli ya ujenzi ni agizo lililotolewa na Mheshimiwa rais mnamo tarehe 05.11.2012 akiwa ziarani mkoani Singida na kukumbusha  utekelezaji wa jambo hilo kwa wakuu wa Mikoa.

Sanjari na hayo Mlozi amezitaja baadhi ya shule za sekondari za kata zilizopiga hatua katika ujenzi wa vyumba hivyo vya maabara kwa kiwango cha asilimia themanini kuwa ni pamoja na Makuro, Makhojoa, Mrama na Itaja.

Katikaa kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Mllozi amewataka madiwanihao kuhakikisha ujenzi wa vyumba hivyo unakamilika Juni 30 mwaka huu (2014) kama walivyoagizwa na kuwa baada ya hapo  sheria kali itachukuliwa dhidi yao.


Ameongeza kuwa endapo kata husika haitakuwa imekamilisha ujenzi wa vyumba hivyo; atawawajibisha diwani na mtendaji wa kata husika kwa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 14 na 15 vya sheria ya Tawala za mikoa na Serikali za mitaa ya mwaka 2002 kwa kuvunja amri halali ya kujenga vyumba vitatu vya maabara.

Kwa upande mwingine; Mlozi amewapongeza baadhi ya viongozi wenzie waliofanya jitihata kubwa katika kukamilisha ujenzi wa vyumba hivyo vya maabara.

MWISHO

Tuesday, February 18, 2014

ICT - FOR SECONDARY SCHOOL TEACHERS IS NEEDED

By Doris Meghji Tues, February 18, 2014
Singida

The need of the integration of ICT in education focusing on mathematics and science subjects literate teachers is highly needed to Tanzania Secondary schools on today’s world of science and technology has been advised.

The advice have given yesterday with Mr. Benjamin Bussu the program coordinator of training during the opening of the ICT training program for secondary school teachers, held at Open University of Tanzanian Singida Centre for 13 participants’ teachers from Arusha, Manyara and Singida

According to Mr. Bussu few participation of the secondary school teachers on the training of ICT integration education which focus on Mathematics and science subjects let down the efforts made by Tanzania government, OUT and the African Virtual University who sponsored the ICT training program for secondary teachers aiming to improving and enable to integrate ICT knowledge and skills with science subjects, have been reported. 

Benjamin Bussu, said that the ICT training program for secondary school teachers facilitate by African Virtual University, in collaboration with Open University of Tanzania and TAMISEMI pointed the finger to district and municipal directors for not allowing their teachers to attend to the ICT training programmed held at OUT Singida Centre.

‘In this training in OUT Singida centre supposed to have 24 participants’ teachers ,only 13 attended to this training this is the challenge we face, most of district council directors complains  on financial deficit, despite of worthiness  and  the efforts  of the training is to secondary school teachers’.  Said Mr. Bussu

However Bussu wanted the teachers participated on that training to take ICT as help for this world of science and technology especially for teachers it will assist on getting a lot of materials on preparing notes instead of using the old methods they used on preparing their lesson scheme.

In this training program 300 secondary schools teachers supposed to be trained whereby AVU agree to pay 300 USD for tuition fees of each teacher participate in this program countrywide only 138 teacher have been allowed to attend to this training program due to carelessness at district level countrywide
Whereby TAMISEMI agreed to pay the accommodation and transport allowance through the local government to the teachers attended to that program while the Open University of Tanzania providing the ICT laboratories and facilitator in the regional centre available in Tanzania.

Elaborating on it, Benjamin Bussu pointed the finger to district and municipal council directors for not allowing their secondary school teacher to attend to this ICT training by complaining on financial deficit on their councils.emphasized Mr. Bussu 

On the other hand the Director of Open University Of Tanzania Singida center Dr. Mbaraka Msangi emphasized on the use of integration ICT will be the help for future development and world competitions economically, socially and politically.

 He said ‘we all aware of high speed in breaking through in science and technology globally, recently about a month ago one daily news paper pointed out that we have about only 2,600 science teachers in the country this show how the situations is, therefore this ICT training program is one of the government efforts on taking all possible measures aimed at revising this unpleasant trend in country.   

In the side of the District Education officer for Singida district council Mr. Voster Mgina said that the ICT training program will be meaningful if the teacher could make use of it as the fruitful of them and other stakeholders, when advised them to use right opportunity of having that training during opening remarks of ICT training at Singida OUT centre. 

“the knowledge you get here you need to share with other teachers most of schools don’t have  ICT in yours schools.  having this training is a nice thing in these days, using ICT integration one teacher could   teach three classrooms at a time, without ICT you can’t. Said Mr. Mgina on emphasizing the importance of that training to them.

Also DEO Mgina appreciate the African Virtual University,TAMISEMI and OUT for sponsored that training program for building the capacity  of the Secondary schools teachers of Singida region  and Tanzania in general

That ICT training will be conducted for fourteen days whereby basic skills and ICT integration focusing particularly on mathematics and science subjects will be trained at Singida OUT centre.
THE END








AKAMATWA KWA KUUA MTOTO NA KUMTUPA VICHAKANI

Na Evarista Lucas
Singida
Februari 18,2014
 
Jeshi la  polisi mkoani Singida linamshikilia  bi Naomi Daud  mkazi wa Muhawa kata ya Mungumaji mkoani hapa kwa kosa la kumuua mtoto wake na kisha kumtupa vichakani.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari ofisini kwake mapema jana; kamanda wa Polisi mkoa wa Singida  ASCP Geofrey Kamwela amesema; Mtuhumiwa alikamatwa nyumbani kwao Muhawa mara baada ya polisi kupata taarifa za siri  na kufanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa.
 
Amesema;  katika uchunguzi wa awali ambao unaonesha kuwa mtuhumiwa alijifungua  nyumbani kwao usiku wa manane siku ya tarehe 04.02.2014  kwa kujizalisha mwenyewe huku mama yake mzazi akimshuhudia na asijue la kufanya; alijifungua salama na mtoto akiwa mzima.
 
Kamanda Kamwela ameeleza kuwa; mara baada ya kujifungua binti huyo alimywesha mtoto huyo lita nzima ya maji ya mvua kutokana na mvua iliyokuwa ikinyeesha hali iliyopelekea mtoto huyo kutapika sana na  baada ya lisaa limoja kichanga hicho kilipoteza maisha.
 
Licha ya kitendo hicho cha kikatili dhidi ya kiumbe kisicho na hatia; binti huyo na mamae walishinda na maiti hiyo siku nzima na  siku ya tarehe 05.02.2014 majira ya saa 02:00 za usiku walitoka na kwenda kukitekeleza kichanga hicho  eneo la Bomani umbali zaidi ya kilometa tatu  kutoka mahali wanapoishi.
 
Aidha; Kamanda Kamwela amefafanua kuwa kuwa kukamatwa kwa binti huyo kumetokana na tukio la kuokotwa kwa mwili wa mtoto mchanga siku ya tarehe 12.04.2014 majira ya saa 02;00 asubuhi eneo la Bomani baada ya kutupwa na mwanamke ambaye hakujulikana.
 
Mtuhumiwa Naomi Daudi antarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili mara baada ya taratibu za kiuchunguzi kukamilika.

MWISHO.

WALIMU KUFUNDISHWA JUU YA TEHEMA

Na Evarista Lucas
Singida
Februali 18,2014

Asilimia 54 ya walimu waliotarajiwa kupata mafunzo ya teknolojia ya habari na mawasiliano(TEKNOHAMA) ngazi ya cheti; yanayoendeshwa  kwa ushirikiano wa chuo kikuu huria Tanzania na “African Virtual University”(AVU).
Hayo yamebainishwa mapema jana wakati wa ufunguzi wa  mafunzo hayo  ya wiki mbili na mkuu wa idara ya mafunzo na ushauri Taasisi ya Elimu na Menejimenti ya teknolojia chuo kikuu huria Tanzania; Bwana Benjamin Bussu.

Ndg Benjamini Bussu akiwaeleza washiriki umuhimu wa mafunzo haya kwa waalimu kwa njia ya Teknolojia ya Mawasiliano(Internet).Picha na Doris Meghji
Amesema; mafunzo hayo ambayo yamelenga kuwaongezea ujuzi walimu  juu ya teknolojia ya habari  na mawasiliano haswa wale wanaofundisha masomo ya Sayansi na Hisabati ili kuendana na soko la ushindani katika nyanja za Sayansi na Teknolojia.
Bussu amesema kuwa, upungufu huo wa walimu hao umepelekewa na washiriki kukosa msaada kutoka wilaya husika ikiwa ni pamoja na Halmashauri nyingi kusema  kuwa   hazina pesa za kutosha kuwagharamia walimu hao hali iliyowafanya baadhi yao kujigharamikia nauli ili wapate kuhudhuria mafunzo hayo.
Bussu amesema kuwa licha ya baadhi ya wakurugenzi kukataa kuwalipia  walengwa gharama za usafiri; ameitaja  sababu nyingine kuwa huenda taarifa juu ya mafunzo hayo  hazikuwafikia walengwa kama ilivyotakiwa licha ya taarifa kupelekwa kwa makatibu tawala wa mikoa yote Tanzania.
 
Mbali na hayo, Bussu ametoa wito kwa viongozi na walimu kwa jumla kutambua umuhimu wa mafunzo haya kwa kuzingatia mabadiliko na maendeleo ya sayansi na teknolojia ambapo Tanzania ni nchi ya  nne kwa Afrika mashariki ikilinganishwa nan chi za Rwanda, Burundi na Kenya ambao wamepiga hatua katika Nyanja hii.
Kwa upande wake mkurugenzi wa chuo kikuu huria tawi la Singida Dk. Mbaraka Msangi amesema kuwa, mafunzo hayo ni chachu katika  maendeleo ya nchi yetu kwa kuwa yamekuja kwa wakati muafaka ambapo dunia imeingia katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia.
Msangi amewataka  walengwa kuyatumia vizuri mafunzo hayo ili kuleta mabadiliko katika Nyanja nzima ya soko la elimu haswa kwa masomo ya sanyansi na ukizingatia kuwa nchi inakabiliwa na tatizo la waalimu wa masomo y sayansi.
 
Mkurugenzi wa Chuo kikuu Huria cha Tanzania tawi la Singida Ndg.Mbaraka Msangi akitoa neno kwa washiriki wa mafunzo
Waalimu wanafunzi wakifuatilia hotuba toka kwa Mkurugenzi wa Chuo kikuu Huria cha Tanzania tawi la Singida katika ufunguzi wa mafunzo jana mkoani Singida

Akilinganisha uchukuaji wa masomo katika mchepuo wa masomo ya Sayansi halisi(pure Science) kwa kipindi cha miaka ya sabini na sasa; Msangi amesema kuwa kipindi cha nyuma wanafunzi walikuwa wakigombea kusoma mchepuo wa Sayansi tofauti na sasa ambapo wanafunzi wanakimbilia masomo ya sanaa. 
Mafunzo  hayo ya TEKNOHAMA ambayo yalipaswa kuwa na washiriki mia tatu(300) na badala yake wameshiriki walimu 138 kwa Tanzania nzima; yana lengo la kuwafundisha walimu wa shule za sekondari nchini ili waweze kuhamasisha na kufundisha zaidi masomo ya Sayansi na Hisabati.
Kwa kituo cha Singida; mafunzo haya yamewakutanisha walimu kutoka mikoa ya mikoa ya Arusha, Manyara na  mwenyeji mkoa wa Singida ambapo wanaoshiriki mafunzo hayo ni wanafunzi 20 tu badala ya thelathini na sita.

MWISHO

Thursday, February 13, 2014

AKAMATWA NA NYARA ZA SERIKALI SINGIDA

Na Evarista Lucas
Singida,
Februari 13, 2014
 
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida; Bwana Geofrey Kamwela ametoa wito kwa wananchi wapenda amani wa Mkoa wa Singida na Tanzania kwa ujumla; kufichua maovu ya wizi wa nyara dhidi ya nyara za Serikali.

Wito huo umetolewa  na kamanda  Kamwela mapema leo wakati akitoa taarifa  kwa vyombo vya habari ofisini kwake kufuatia kukamatwa kwa nyara za serikali. Kamwela amesema tukio hilo lililomuhusisha mkazi wa Mwamagembe Itigi George James (30), limetokea mapema leo majira ya saa mbili unusu za asubuhi.(2:30asb)

Amesema; George amekamatwa na vipande ishirini na moja vya meno ya tembo katika kizuizi cha mazao ya misitu na chakula kilichopo katika kijiji cha Ukimbu, kata ya Mgandu wilayani Manyoni mkoani Singida ambapo jeshila polisi liliweka mtego mara baada ya kupata taarifa za mtu huyo kutoka kwa raia wema.

Aidha ; Kamanda Kamwela amesema kuwa Polisi walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa mabaye alikuwa katika gari aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T. 797  wakati akiwa katika harakati za kuzisafirisha nyara hizo kwenda Itigi mjini.

Kamwela ameongeza kuwa, mara baada ya upekuzi wa kina; Pembe hizo ambazo zilifichwa kiustadi; zilikutwa zimehifadhiwa katika mabegi mbali mbali ya nguo kana kwamba  mtuhumiwa alikuwa amebeba nguo.

Aidha katika uchunguzi wake wa awali; jeshila polisi kwa kushirikiana na idara ya Wanyamapori unaonesha kuwa vipande hivyo vinakadiriwa kuwa ni vya tembo wane vyenye uzito wa kilogramu 49 na thamani yake ni  zaidi ya shilingi milioni arobaini na tatu za kitanzania (43,120,000/=).

Kwa upande mwingine Kamanda Kamwela amesema kuwa, Jeshi la polisi mkoani hapa lianendela na uchunguzi wake ikiwa ni pamojana kufahamu mtandao anaoshirikiana  nao (mtuhumiwa) kuanzia uwindaji hadi mahali anapopeleka.
 
MWISHO
Na Evarista Lucas
Singida,
Februari 13, 2014
 
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida; Bwana Geofrey Kamwela ametoa wito kwa wananchi wapenda amani wa Mkoa wa Singida na Tanzania kwa ujumla; kufichua maovu ya wizi wa nyara dhidi ya nyara za Serikali.

Wito huo umetolewa  na kamanda  Kamwela mapema leo wakati akitoa taarifa  kwa vyombo vya habari ofisini kwake kufuatia kukamatwa kwa nyara za serikali. Kamwela amesema tukio hilo lililomuhusisha mkazi wa Mwamagembe Itigi George James (30), limetokea mapema leo majira ya saa mbili unusu za asubuhi.(2:30asb)

Amesema; George amekamatwa na vipande ishirini na moja vya meno ya tembo katika kizuizi cha mazao ya misitu na chakula kilichopo katika kijiji cha Ukimbu, kata ya Mgandu wilayani Manyoni mkoani Singida ambapo jeshila polisi liliweka mtego mara baada ya kupata taarifa za mtu huyo kutoka kwa raia wema.

Aidha ; Kamanda Kamwela amesema kuwa Polisi walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa mabaye alikuwa katika gari aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T. 797  wakati akiwa katika harakati za kuzisafirisha nyara hizo kwenda Itigi mjini.

Kamwela ameongeza kuwa, mara baada ya upekuzi wa kina; Pembe hizo ambazo zilifichwa kiustadi; zilikutwa zimehifadhiwa katika mabegi mbali mbali ya nguo kana kwamba  mtuhumiwa alikuwa amebeba nguo.

Aidha katika uchunguzi wake wa awali; jeshila polisi kwa kushirikiana na idara ya Wanyamapori unaonesha kuwa vipande hivyo vinakadiriwa kuwa ni vya tembo wane vyenye uzito wa kilogramu 49 na thamani yake ni  zaidi ya shilingi milioni arobaini na tatu za kitanzania (43,120,000/=).

Kwa upande mwingine Kamanda Kamwela amesema kuwa, Jeshi la polisi mkoani hapa lianendela na uchunguzi wake ikiwa ni pamojana kufahamu mtandao anaoshirikiana  nao (mtuhumiwa) kuanzia uwindaji hadi mahali anapopeleka.
 
__________________________MWISHO_______________________________

Saturday, February 8, 2014

MAJINA YA WABUNGE WA BUNGE LA KATIBA YAPO HAPA


MAJINA YA WAJUMBE WA BUNGE MAALUMU LA KATIBA

UTANGULIZI
1.              Uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba Unatawaliwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura, 83 (The Constitutional Review Act, Cap 83). Sheria hii inaweka mamlaka ya uteuzi, masharti, taratibu, vigezo na mambo mengine yote yanayopaswa kuzingatiwa katika uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba. Kwa mujibu wa Kifungu cha 22 (2A) na (2B) vigezo hivi vinajumuisha umri, jinsia, uzoefu, sifa na mahali anapotoka mjumbe husika.
2.           Sheria hii inatamka aina tatu za Wajumbe wa Bunge la Katiba kama ifuatavyo:-
(i)               Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano;
(ii)            Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar; na
(iii)         Wajumbe 201 kwa mujibu wa  Kifungu Na. 22(1c) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo inaonyesha makundi mbalimbali 10 yanayohusika.
3.           Makundi hayo ni  kama ifuatavyo:-
(i)                  Taasisi zisizokuwa za Kiserikali (20)
(ii)               Taasisi za Kidini (20)
(iii)            Vyama vyote vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu (42);
(iv)             Taasisi za Elimu (20);
(v)                Watu wenye Ulemavu (20);
(vi)             Vyama vya Wafanyakazi (19);
(vii)          Vyama vinavyowakilisha Wafugaji (10);
(viii)       Vyama vinavyowakilisha wavuvi (10);
(ix)             Vyama vya Wakulima (20); na
(x)                Vikundi vya Watu wenye Malengo yanayofanana (20).
4.           Mchakato wa uteuzi ulianza kwa kutoa Tangazo la Mwaliko katika Gazeti la Serikali, Tangazo la Serikali Na 443 la tarehe 13 Desemba, 2013. Tangazo hilo lilitolewa kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza ili kuyaalika makundi yaliyotajwa kisheria kuwasilisha mapendekezo ya majina kwa ajili ya uteuzi katika Bunge laMaalum la Katiba. Aidha, Tangazo hilo la mwaliko lilitangazwa pia katika magazeti mbalimbali yanayosomwa hapa nchini. Pamoja na mambo mengine Tangazo la Mwaliko lilitamka ukomo wa muda wa Taasisi na Makundi kuwasilisha mapendekezo ya majina ya wajumbe kuwa ni tarehe 02/01/2014.
5.           Mapendekezo hayo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar, mapendekezo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
6.           Kufuatia mwaliko huo, taasisi 554 kutoka Tanzania Bara na 178 kutoka Zanzibar ziliwasilisha mapendekezo yao. Mapendekezo hayo yalijumuisha majina 2,762 kwa upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar mapendekezo hayo yalihusisha watu 874. Hivyo basi, taasisi na makundi mbalimbali yalipendekeza jumla ya majina 3,636. Lakini, na kinyume na Sheria, watu 118 walijipendekeza wenyewe na kufanya idadi ya majina yaliyopendekezwa kuwa 3,754.
7.           Mchanganuo wa idadi ya watu walipendekezwa katika makundi mbalimbali ni kama ifuatavyo:
Na.
Kundi/Taasisi
Taasisi zilizoleta mapendekezo
Idadi ya Watu Waliopendekezwa
Idadi ya Wajumbe Wanaotakiwa
Idadi ya Walioteuliwa
Tanzania Bara
Zanzibar
Tanzania Bara
Zanzibar
Tanzania Bara
Zanzibar
1.     
Taasisi zisizokuwa za Kiserikali
246
98
1,203
444
20
13
7
2.     
Taasisi za Kidini
55
17
344
85
20
13
7
3.     
Vyama vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu
21
14
129
69
42
28
14
4.     
Taasisi za Elimu
9
9
84
46
20
13
7
5.     
Makundi ya Walemavu
24
6
97
43
20
13
7
6.     
Vyama vya Wafanyakazi
20
1
89
13
19
13
6
7.     
Vyama Vinavyowakilisha Wafugaji
8
1
43
4
10
7
3
8.     
Vyama vinavyowakilisha Wavuvi
7
3
45
12
10
7
3
9.     
Vyama vya Wakulima
22
8
115
44
20
13
7
10.             
Makundi yenye Malengo Yanayofanana
142
21
613
114
20
14
6
Mapendekezo Binafsi
-
-
118
-
Jumla
672
178
2,880
874
201
134
67
Jumla Kuu
850
3,754


8.           Sheria ya Mabadiliko ya Katiba imeweka masharti ya kuzingatiwa katika uteuzi wa wajumbe 201 wa Bunge la Maalum la Katiba. Masharti hayo ni pamoja na wajumbe wasiopungua theluthi moja wanatakiwa kutoka Zanzibar na theluthi mbili kutoka Tanzania Bara. Kwa sababu hiyo, katika wajumbe 201, wajumbe 67 watatoka Zanzibar na wajumbe 134 watatoka Tanzania Bara. Aidha, mgawanyo wa wajumbe wanawake na wanaume unatakiwa uwe nusu kwa nusu. Pamoja na hayo, wajumbe hao wawakilishe sura ya wananchi wa Tanzania kwa ufuasi wa vyama vya siasa, dini, umri, na maeneo wanayotoka. Katika mazingira haya, zoezi la kupata wajumbe 201 halikuwa rahisi hata kidogo. Mwitikio wa makundi ulikuwa mkubwa sana ikilinganishwa na nafasi zilizopo.
9.           Kama nilivyoeleza hapo awali, mapendekezo kutoka Tanzania Bara yalikuwa 2,880 wakati nafasi za wajumbe ni 134. Kwa upande wa Zanzibar, majina yaliyopendekezwa yalikuwa 874 ikilinganishwa na idadi ya wajumbe 67 wanaotakiwa kuteuliwa. Kwa nyongeza ya maelezo kuhusu uwingi wa mapendekezo, ni kwamba ukichukua taasisi zisizo za kiserikali kwa upande wa Tanzania Bara walipendekezwa watu 1,203, wakati nafasi zilizokuwa zinatakiwa kujazwa ni 13 tu. Kwa upande Zanzibar, taasisi zisizokuwa za kiserikali zilikuwa zimependekeza majina 444 ikilinganishwa na nafasi 7 tu zilizokuwa zinatakiwa kujazwa kutokana na taasisi hizi.
WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA
10.      Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania wakishirikiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpainduzi Zanzibar wamekamilisha uteuzi wa wajumbe 201. Kabla ya kutaja orodha ya wajumbe walioteuliwa, napenda kufafanua mambo yafuatayo:
(a)             Uteuzi umezingatia ushiriki wa watu wa rika zote, yaani vijana, watu wazima na wazee. Kwa ajili hiyo, wajumbe vijana yaani wenye umri wa kati miaka 22-35, ni wajumbe 35. Wajumbe wenye umri wa kati, yaani miaka 36-64, ni 145; na wajumbe wazee, yaani wenye umri wa miaka 65 na kuendelea ni 21.
(b)             Sheria inataka kuwepo na uwiano sawa kwa ajumbe wanawake na wanaume. Jambo hili limezingatiwa ipasavyo, na katika orodha hii wajumbe wanawake ni 100 na wanaume 101. Kwa vile, haiwezekani kuwa na nusu mtu, ndiyo maana idadi ya wajumbe wanaume ni 101.
(c)              Uwakilishi wa vyama vya siasa ambao unahitaji kila chama chenye usajili wa kudumu kiwe na wajumbe wawili umezingatiwa. Kwa kuwa kuna vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu 21, jumla ya wajumbe 42 wamechaguliwa kwa maana ya kuwa wajumbe wawili wameteuliwa kutoka katika kila chama.
Baada ya maelezo hayo ya utangulizi, ifuatayo ndiyo orodha ya wajumbe 201 wa Bunge Maalum la Katiba waliobahatika kuteuliwa:

TAASISI ZISIZOKUWA ZA KISERIKALI- (WAJUMBE 20)

TANZANIA BARA (13)

1.     Magdalena Rwebangira
2.        Kingunge Ngombale Mwiru
3.     Asha D. Mtwangi
4.        Maria Sarungi Tsehai
5.     Paul Kimiti
6.        Valerie N. Msoka
7.     Fortunate Moses Kabeja
8.        Sixtus Raphael Mapunda
9.     Elizabeth Maro Minde
10.   Happiness Samson Sengi
11. Evod Herman Mmanda
12.   Godfrey Simbeye
13. Mary Paul Daffa
TANZANIA ZANZIBAR (7)
1.     Idrissa Kitwana Mustafa
2.          Siti Abbas Ali
3.     Abdalla Abass Omar
4.          Salama Aboud Talib
5.     Juma Bakari Alawi
6.          Salma Hamoud Said
7.     Adila Hilali Vuai
TAASISI ZA KIDINI- (WAJUMBE 20)
TANZANIA BARA (13)
1.   Tamrina Manzi
2.        Olive Damian Luwena
3.   Shamim Khan
4.        Mchg. Ernest Kadiva
5.   Sheikh Hamid Masoud Jongo
6.        Askofu Mkuu (Mstaafu) Donald Leo Mtetemela
7.   Magdalena Songora
8.        Hamisi Ally Togwa
9.   Askofu Amos J. Muhagachi
10.   Easter Msambazi
11.                                                           Mussa Yusuf Kundecha
12.   Respa Adam Miguma
13.                                                           Prof. Costa Ricky Mahalu
TANZANIA ZANZIBAR (7)
1.     Sheikh Thabit Nouman Jongo
2.     Suzana Peter Kunambi
3.     Sheikh Nassoro Mohammed Ibrahimu
4.     Fatma Mohammed Hassan
5.     Louis Majaliwa
6.     Yasmin Yusufali E. H alloo
7.     Thuwein Issa Thuwein


VYAMA VYOTE VYA SIASA
VYENYE USAJILI WA KUDUMU – (WAJUMBE 42)
TANZANIA BARA (28)
1.        Hashim Rungwe Spunda
2.           Thomas Magnus Mgoli
3.        Rashid Hashim Mtuta
4.           Shamsa Mwangunga
5.        Yusuf  S. Manyanga
6.           Christopher Mtikila
7.        Bertha Ng’angompata
8.           Suzan Marwa
9.        Dominick Abraham Lyamchai
10.      Mbwana Salum Kibanda
11.   Peter Kuga Mziray
12.      Isaac Manjoba Cheyo
13.   Dr. Emmanuel John Makaidi
14.      Prof. Ibrahim Haruna Lipumba
15.   Modesta Kizito Ponera
16.      Prof. Abdallah Safari
17.   Salumu Seleman Ally
18.      James Kabalo Mapalala
19.   Mary Oswald Mpangala
20.      Mwaka Lameck Mgimwa
21.   Nancy  S. Mrikaria
22.      Nakazael Lukio Tenga
23.   Fahmi Nasoro Dovutwa
24.      Costantine  Benjamini Akitanda
25.   Mary Moses Daudi
26.      Magdalena Likwina
27.   John Dustan Lifa Chipaka
28.      Rashid Mohamed Ligania Rai
TANZANIA ZANZIBAR (14)
1.     Ally Omar Juma
2.     Vuai Ali Vuai
3.     Mwanaidi Othman Twahir
4.     Jamila Abeid Saleh
5.     Mwanamrisho Juma Ahmed
6.     Juma Hamis Faki
7.     Tatu Mabrouk Haji
8.     Fat –Hiya Zahran Salum
9.     Hussein Juma
10.     Zeudi Mvano Abdullahi
11.     Juma Ally Khatibu
12.     Haji Ambar Khamis
13.     Khadija Abdallah Ahmed
14.     Rashid Yussuf Mchenga


TAASISI ZA ELIMU- (WAJUMBE 20)
TANZANIA BARA
1.     Dr. Suzan Kolimba
2.     Prof. Esther Daniel Mwaikambo
3.     Dr. Natujwa Mvungi
4.     Prof. Romuald Haule
5.     Dr. Domitila A.R. Bashemera
6.     Dr. Jasmine Bendantunguka Tiisekwa
7.     Prof. Bernadeta Kilian
8.     Teddy Ladislaus Patrick
9.     Dr. Francis Michael
10.    Prof. Remmy J. Assey
11.               Dr. Tulia Ackson
12.               Dr. Ave Maria Emilius Semakafu
13.               Hamza Mustafa Njozi
TANZANIA ZANZIBAR (7)
1.     Makame Omar Makame
2.     Fatma Hamid Saleh
3.     Dr. Aley Soud Nassor
4.     Layla Ali Salum
5.     Dkt. Mwinyi Talib Haji
6.     Zeyana Mohamed Haji
7.     Ali Ahmed Uki
WATU WENYE ULEMAVU-(WAJUMBE 20)
TANZANIA BARA (13)
1.        Zuhura Musa Lusonge
2.     Frederick Msigala
3.        Amon Anastaz Mpanju
4.     Bure Zahran
5.        Edith Aron Dosha
6.     Vincent Venance Mzena
7.        Shida Salum Mohamed
8.     Dr. Henry Mwizengwa Nyamubi.
9.        Elias Msiba Masamaki
10.                   Faustina Jonathan Urassa
11.   Doroth Stephano Malelela
12.                   John Josephat Ndumbaro
13.   Ernest Njama Kimaya
TANZANIA ZANZIBAR (7)
1.     Haidar Hashim Madeweyya
2.     Alli Omar Makame
3.     Adil Mohammed Ali
4.     Mwandawa Khamis Mohammed
5.     Salim Abdalla Salim
6.     Salma Haji Saadat
7.     Mwantatu Mbarak Khamis
VYAMA VYA WAFANYAKAZI-(WAJUMBE 19)
TANZANIA BARA (13)
1.     Honorata Chitanda
2.     Dr. Angelika Semike
3.     Ezekiah Tom Oluoch
4.     Adelgunda Michael Mgaya
5.     Dotto M. Biteko
6.     Mary Gaspar Makondo
7.     Halfani Shabani Muhogo
8.     Yusufu Omari Singo
9.     Joyce Mwasha
10.                   Amina Mweta
11.                   Mbaraka Hussein Igangula
12.                   Aina Shadrack Massawe
13.                   Lucas Charles Malunde
TANZANIA ZANZIBAR (6)
1.   Khamis Mwinyi Mohamed
2. Jina Hassan Silima
3.   Makame Launi Makame
4. Asmahany Juma Ali
5.   Mwatoum Khamis Othman
6. Rihi Haji Ali
VYAMA VINAVYOWAKILISHAWAFUGAJI-(WAJUMBE 10)
TANZANIA BARA (7)
1.     William Tate Olenasha
2.     Makeresia Pawa
3.     Mabagda Gesura Mwataghu
4.     Doreen Maro
5.     Magret Nyaga
6.     Hamis Mnondwa
7.     Ester Milimba Juma
TANZANIA ZANZIBAR (3)
1.     Said Abdalla Bakari
2.     Mashavu Yahya
3.     Zubeir Sufiani Mkanga
VYAMA VINAVYOWAKILISHAWAVUVI –(WAJUMBE 10)
TANZANIA BARA (7)
1.     Hawa A. Mchafu
2.     Rebecca Masato
3.     Thomas Juma Minyaro
4.     Timtoza Bagambise
5.     Tedy Malulu
6.     Rebecca Bugingo
7.     Omary S. Husseni
TANZANIA ZANZIBAR (3)
1.     Waziri Rajab
2.     Issa Ameir Suleiman
3.     Mohamed Abdallah Ahmed


VYAMA VYAWAKULIMA-(WAJUMBE 20)
TANZANIA BARA (13)
1.     Agatha  Harun Senyagwa
2.     Veronica Sophu
3.     Shaban Suleman Muyombo
4.     Catherine Gabriel Sisuti
5.     Hamisi Hassani Dambaya
6.     Suzy Samson Laizer
7.     Dr. Maselle Zingura Maziku
8.     Abdallah Mashausi
9.     Hadijah Milawo Kondo
10.                                                   Rehema Madusa
11.                  Reuben R. Matango
12.                                                   Happy Suma
13.                  Zainab Bakari Dihenga
TANZANIA ZANZIBAR (7)
1.     Saleh Moh’d Saleh
2.     Biubwa Yahya Othman
3.     Khamis Mohammed Salum
4.     Khadija Nassor Abdi
5.     Fatma Haji Khamis
6.     Asha Makungu Othman
7.     Asya Filfil Thani
WATU WENYE MALENGO YANAYOFANANA – (WAJUMBE 20)
TANZANIA BARA (14)
1.        Dr. Christina Mnzava
2.     Paulo Christian Makonda
3.        Jesca Msambatavangu
4.     Julius Mtatiro
5.        Katherin Saruni
6.     Abdallah Majura Bulembo
7.        Hemedi Abdallah Panzi
8.     Dr. Zainab Amir Gama
9.        Hassan Mohamed Wakasuvi
10.               Paulynus Raymond Mtendah
11.   Almasi Athuman Maige
12.               Pamela Simon Massay
13.   Kajubi Diocres Mukajangwa
14.               Kadari Singo
TANZANIA ZANZIBAR (6)
1.     Yussuf Omar Chunda
2.     Fatma Mussa Juma
3.     Prof. Abdul Sheriff
4.     Amina Abdulkadir Ali
5.     Shaka Hamdu Shaka
6.     Rehema Said Shamte
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.