Na Evarista Lucas
Singida
Februali 18,2014
Asilimia 54 ya walimu waliotarajiwa kupata mafunzo
ya teknolojia ya habari na mawasiliano(TEKNOHAMA) ngazi ya cheti;
yanayoendeshwa kwa ushirikiano wa chuo
kikuu huria Tanzania na “African Virtual University”(AVU).
Hayo yamebainishwa mapema jana wakati wa ufunguzi
wa mafunzo hayo ya wiki mbili na mkuu wa idara ya mafunzo na
ushauri Taasisi ya Elimu na Menejimenti ya teknolojia chuo kikuu huria
Tanzania; Bwana Benjamin Bussu.
Ndg Benjamini Bussu akiwaeleza washiriki umuhimu wa mafunzo haya kwa waalimu kwa njia ya Teknolojia ya Mawasiliano(Internet).Picha na Doris Meghji |
Amesema; mafunzo hayo ambayo yamelenga kuwaongezea
ujuzi walimu juu ya teknolojia ya
habari na mawasiliano haswa wale
wanaofundisha masomo ya Sayansi na Hisabati ili kuendana na soko la ushindani
katika nyanja za Sayansi na Teknolojia.
Bussu amesema kuwa, upungufu huo wa walimu hao
umepelekewa na washiriki kukosa msaada kutoka wilaya husika ikiwa ni pamoja na
Halmashauri nyingi kusema kuwa hazina
pesa za kutosha kuwagharamia walimu hao hali iliyowafanya baadhi yao kujigharamikia
nauli ili wapate kuhudhuria mafunzo hayo.
Bussu amesema kuwa licha ya baadhi ya wakurugenzi
kukataa kuwalipia walengwa gharama za
usafiri; ameitaja sababu nyingine kuwa
huenda taarifa juu ya mafunzo hayo hazikuwafikia
walengwa kama ilivyotakiwa licha ya taarifa kupelekwa kwa makatibu tawala wa
mikoa yote Tanzania.
Mbali na hayo, Bussu ametoa wito kwa viongozi na
walimu kwa jumla kutambua umuhimu wa mafunzo haya kwa kuzingatia mabadiliko na
maendeleo ya sayansi na teknolojia ambapo Tanzania ni nchi ya nne kwa Afrika mashariki ikilinganishwa nan
chi za Rwanda, Burundi na Kenya ambao wamepiga hatua katika Nyanja hii.
Kwa upande wake mkurugenzi wa chuo kikuu huria tawi
la Singida Dk. Mbaraka Msangi amesema kuwa, mafunzo hayo ni chachu katika maendeleo ya nchi yetu kwa kuwa yamekuja kwa
wakati muafaka ambapo dunia imeingia katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia.
Msangi amewataka
walengwa kuyatumia vizuri mafunzo hayo ili kuleta mabadiliko katika
Nyanja nzima ya soko la elimu haswa kwa masomo ya sanyansi na ukizingatia kuwa
nchi inakabiliwa na tatizo la waalimu wa masomo y sayansi.
Mkurugenzi wa Chuo kikuu Huria cha Tanzania tawi la Singida Ndg.Mbaraka Msangi akitoa neno kwa washiriki wa mafunzo |
Waalimu wanafunzi wakifuatilia hotuba toka kwa Mkurugenzi wa Chuo kikuu Huria cha Tanzania tawi la Singida katika ufunguzi wa mafunzo jana mkoani Singida |
Akilinganisha uchukuaji wa masomo katika mchepuo wa
masomo ya Sayansi halisi(pure Science) kwa kipindi cha miaka ya sabini na sasa;
Msangi amesema kuwa kipindi cha nyuma wanafunzi walikuwa wakigombea kusoma
mchepuo wa Sayansi tofauti na sasa ambapo wanafunzi wanakimbilia masomo ya
sanaa.
Mafunzo hayo
ya TEKNOHAMA ambayo yalipaswa kuwa na washiriki mia tatu(300) na badala yake
wameshiriki walimu 138 kwa Tanzania nzima; yana lengo la kuwafundisha walimu wa
shule za sekondari nchini ili waweze kuhamasisha na kufundisha zaidi masomo ya
Sayansi na Hisabati.
Kwa kituo cha Singida; mafunzo haya yamewakutanisha
walimu kutoka mikoa ya mikoa ya Arusha, Manyara na mwenyeji mkoa wa Singida ambapo wanaoshiriki
mafunzo hayo ni wanafunzi 20 tu badala ya thelathini na sita.
No comments:
Post a Comment