Na Evarista Lucas
Singida,
feb 19,2014
Mkuu wa wilaya ya Singida Mheshimiwa Queen Mlozi amezitaka kata ambazo
hazijakamilisha ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara katika shule za
sekondari za kata kukamilisha ujenzi huo mara moja.
Akihutubia baraza la madiwani katika kikao cha baraza la madiwani wa
Halmashauri ya wilaya ya Singida mapema leo; Mlozi amesema kuwa hatosita
kuwachukulia hatua kali na za kisheria madiwani na watendaji wote ambao
hawajakamilisha ujenzi wa vyumba hivyo.
Amesema; shughuli ya ujenzi ni agizo lililotolewa na Mheshimiwa rais
mnamo tarehe 05.11.2012 akiwa ziarani mkoani Singida na kukumbusha
utekelezaji wa jambo hilo kwa wakuu wa Mikoa.
Sanjari na hayo Mlozi amezitaja baadhi ya shule za sekondari za kata
zilizopiga hatua katika ujenzi wa vyumba hivyo vya maabara kwa kiwango
cha asilimia themanini kuwa ni pamoja na Makuro, Makhojoa, Mrama na
Itaja.
Katikaa kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Mllozi amewataka madiwanihao
kuhakikisha ujenzi wa vyumba hivyo unakamilika Juni 30 mwaka huu (2014)
kama walivyoagizwa na kuwa baada ya hapo sheria kali itachukuliwa dhidi
yao.
Ameongeza kuwa endapo kata husika haitakuwa imekamilisha ujenzi wa
vyumba hivyo; atawawajibisha diwani na mtendaji wa kata husika kwa
mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 14 na 15 vya sheria ya Tawala za
mikoa na Serikali za mitaa ya mwaka 2002 kwa kuvunja amri halali ya
kujenga vyumba vitatu vya maabara.
Kwa upande mwingine; Mlozi amewapongeza baadhi ya viongozi wenzie
waliofanya jitihata kubwa katika kukamilisha ujenzi wa vyumba hivyo vya
maabara.
MWISHO
No comments:
Post a Comment