Na, Doris Meghji Jumamosi, Februari 01,
2014
Jeshi la polisi mkoani Singida
limekusanya zaidi ya shiling milioni 684
kutokana na tozo ya makosa mbali mbali ya ukiukwaji wa sheria za usalama
barabarani katika kipindi cha mwaka 2013.
Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Singida SACP Georfey Kamwela akitoa taarifa ya mwaka ya hali ya uhalifu mkoa wa Singida (Picha na Doris Meghji) |
Akitoa taarifa ya mwaka ya hali ya
uhalifu mkoani singida kwa kipindi cha mwako 2013 kwa waandishi wa habari,kamanda
wa jeshi la Polisi Mkoa wa Singida SACP Geofrey Kamwela amebainisha hayo katika
taarifa hiyo jana ofisi kwake.
Kwa mujibu wa kamanda Kamwela amesema“kutokana
na ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani jumla ya shilingi milioni 684
900,000/= zilikusanya kwa njia ya tozo, kiasi hicho ni ongezeko la shilingi
milioni 185,100,000/= sawa na asilimia 37 ikilinganishwa na kipindi cha mwaka
2012”.alisema kamanda huyo.
Kamanda Geofrey Kamwela akiendela kutoa taarifa ya mwaka 2013 ya hali ya uhalifu mkoa wa singida (Picha na Doris Meghji) |
Katika kutaja makoso hayo amesema jumla
ya makosa 22,584 madogo madogo ya
ukiukwaji wa sheria za usalama
barabarani yaliyoripotiwa, watu 20,127 walikamatwa mkoani hapo na kutozwa tozo.
Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa singida wakiwa makini kufuatila taarifa hiyo ywa mwaka ya hali ya uhali mkoani Singida katika Ofisi ya kamanda ya jeshi la polisi Mkoa (Picha na Doris Meghji) |
Aidha kwa kipindi cha mwaka huo wa 2013
kulitokea ajali 246 ambapo kati ya ajali hizo ajali 116 zilisababisha watu 129 kupoteza maisha sawa
na ongezeo la asilimia 0.8 ya ajali zilizotokea mwaka 2012,huku watu 299
walijeruhiwa katika ajiali hizo ambayo ni pungufu kwa asilimia 15
zikilinganishwa na majeruhi 353 ya majeruhi kwa mwaka 2012.
Mwandishi wa habari na mmoja wa afisa wa polisi wakisikiliza taarifa hiyo tokakwa Kamanda Geoferey Kamwela (Picha na Doris Meghji) |
Hata hivyo jeshi la polisi mkoani
Singida limewatahini watu 2,845 kwa mafunzo ya udereva na kufaulu na kepewa
leseni za udereva kati hao 436 wakiwa ni
pikipiki kwa kipidi cha mwaka 2013.
Kamanda SACP Geofrey Kamwela akitoa taarifa ya hali ya uhalifu ya mwaka mkoa wa Singida katika kipindi cha Janauari 2013 hadi disema 2013 (picha na Doris Meghji) |
Hivyo jeshi hilo mkoani Singida limesema
juhudi bado zinaendelea kufanyika kwa kufanya kazi za operesheni kwa
kushrikiana na wadau wengine kama SUMATRA na TAMISEMI ili kudhibiti ajali za
barabarani hasa kwenye njia kuu na kwenye vituo vya mabasi yaendayo mikoni na
vijijini na maeneo tete yalibanishwa na jeshi hilo.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment