Na Evarista Lucas
Singida,
Februari 13, 2014
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida; Bwana Geofrey
Kamwela ametoa wito kwa wananchi wapenda amani wa Mkoa wa Singida na Tanzania
kwa ujumla; kufichua maovu ya wizi wa nyara dhidi ya nyara za Serikali.
Wito huo umetolewa
na kamanda Kamwela mapema leo wakati
akitoa taarifa kwa vyombo vya habari
ofisini kwake kufuatia kukamatwa kwa nyara za serikali. Kamwela amesema tukio
hilo lililomuhusisha mkazi wa Mwamagembe Itigi George James (30), limetokea
mapema leo majira ya saa mbili unusu za asubuhi.(2:30asb)
Amesema; George amekamatwa na vipande ishirini na
moja vya meno ya tembo katika kizuizi cha mazao ya misitu na chakula kilichopo
katika kijiji cha Ukimbu, kata ya Mgandu wilayani Manyoni mkoani Singida ambapo
jeshila polisi liliweka mtego mara baada ya kupata taarifa za mtu huyo kutoka
kwa raia wema.
Aidha ; Kamanda Kamwela amesema kuwa Polisi
walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa mabaye alikuwa katika gari aina ya Toyota
Hiace lenye namba za usajili T. 797 wakati akiwa katika harakati za kuzisafirisha nyara
hizo kwenda Itigi mjini.
Kamwela ameongeza kuwa, mara baada ya upekuzi wa
kina; Pembe hizo ambazo zilifichwa kiustadi; zilikutwa zimehifadhiwa katika
mabegi mbali mbali ya nguo kana kwamba
mtuhumiwa alikuwa amebeba nguo.
Aidha katika uchunguzi wake wa awali; jeshila polisi
kwa kushirikiana na idara ya Wanyamapori unaonesha kuwa vipande hivyo
vinakadiriwa kuwa ni vya tembo wane vyenye uzito wa kilogramu 49 na thamani
yake ni zaidi ya shilingi milioni
arobaini na tatu za kitanzania (43,120,000/=).
Kwa upande mwingine Kamanda Kamwela amesema kuwa,
Jeshi la polisi mkoani hapa lianendela na uchunguzi wake ikiwa ni pamojana
kufahamu mtandao anaoshirikiana nao (mtuhumiwa)
kuanzia uwindaji hadi mahali anapopeleka.
MWISHO

__________________________MWISHO_______________________________
No comments:
Post a Comment