Na Evarista Lucas
Singida
Februari 18,2014
Jeshi la
polisi mkoani Singida linamshikilia bi Naomi Daud mkazi wa Muhawa kata ya Mungumaji mkoani hapa kwa
kosa la kumuua mtoto wake na kisha kumtupa vichakani.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari ofisini kwake
mapema jana; kamanda wa Polisi mkoa wa Singida ASCP Geofrey Kamwela amesema; Mtuhumiwa
alikamatwa nyumbani kwao Muhawa mara baada ya polisi kupata taarifa za
siri na kufanikisha kukamatwa kwa
mtuhumiwa.
Amesema;
katika uchunguzi wa awali ambao unaonesha kuwa mtuhumiwa alijifungua nyumbani kwao usiku wa manane siku ya tarehe
04.02.2014 kwa kujizalisha mwenyewe huku
mama yake mzazi akimshuhudia na asijue la kufanya; alijifungua salama na mtoto
akiwa mzima.
Kamanda Kamwela ameeleza kuwa; mara baada ya
kujifungua binti huyo alimywesha mtoto huyo lita nzima ya maji ya mvua kutokana
na mvua iliyokuwa ikinyeesha hali iliyopelekea mtoto huyo kutapika sana na baada ya lisaa limoja kichanga hicho
kilipoteza maisha.
Licha ya kitendo hicho cha kikatili dhidi ya kiumbe
kisicho na hatia; binti huyo na mamae walishinda na maiti hiyo siku nzima na siku ya tarehe 05.02.2014 majira ya saa 02:00
za usiku walitoka na kwenda kukitekeleza kichanga hicho eneo la Bomani umbali zaidi ya kilometa tatu kutoka mahali wanapoishi.
Aidha; Kamanda Kamwela amefafanua kuwa kuwa
kukamatwa kwa binti huyo kumetokana na tukio la kuokotwa kwa mwili wa mtoto
mchanga siku ya tarehe 12.04.2014 majira ya saa 02;00 asubuhi eneo la Bomani
baada ya kutupwa na mwanamke ambaye hakujulikana.
Mtuhumiwa Naomi Daudi antarajiwa kufikishwa
mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili mara baada ya taratibu za kiuchunguzi
kukamilika.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment