Na Evarista Lucas
Singida,
Feb 19,2014
Mkulima na mkazi wa kijiji cha Unyanga kata ya Mungumaji Mkoani Singida
Bwana Petro Soghwenda (86); amepoteza maisha nyumbani kwake akiwa
katika harakati za kupelekwa hospitali mara baada ya kupikwa jiwe sehemu
za kichwani.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari mapema leo; Kamanda wa jeshi
la Polisi mkoani Singida ASCP Geofrey Kamwela amesema kuwa; marehemu
Soghwenda alipoteza maisha siku ya tarehe 18.02.2014 baada ya
kushambuliwa na Maria Daudi (16) ambaye pia ni mkulima na mkazi wa
Unyanga.
Aidha; Kamanda Kamwela amesema kuwa katika uchunguzi wake wa awali,
Jeshi la polisi mkoani hapa limebaini kuwa mtuhumiwa ana tatizo la akila
na ugonjwa wa kifafa.
Ameongeza kuwa chanzo cha tuko hilo bado hakijafahamika lakini mtuhumiwa
Maria Daudi anashikiliwa na jeshi la polisi mpaka pale uchunguzi
utakapo kamilika na mtuhumiwa kufikishwa makamani kujibu tuhuma
zinazomkabili.
Mwili wa Marehemu Petro Soghwenda umehifadhiwa katika hospitali ya Mkoa wa Singida.
MWISHO
No comments:
Post a Comment