Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Saturday, February 8, 2014

MAJINA YA WABUNGE WA BUNGE LA KATIBA YAPO HAPA


MAJINA YA WAJUMBE WA BUNGE MAALUMU LA KATIBA

UTANGULIZI
1.              Uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba Unatawaliwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura, 83 (The Constitutional Review Act, Cap 83). Sheria hii inaweka mamlaka ya uteuzi, masharti, taratibu, vigezo na mambo mengine yote yanayopaswa kuzingatiwa katika uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba. Kwa mujibu wa Kifungu cha 22 (2A) na (2B) vigezo hivi vinajumuisha umri, jinsia, uzoefu, sifa na mahali anapotoka mjumbe husika.
2.           Sheria hii inatamka aina tatu za Wajumbe wa Bunge la Katiba kama ifuatavyo:-
(i)               Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano;
(ii)            Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar; na
(iii)         Wajumbe 201 kwa mujibu wa  Kifungu Na. 22(1c) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo inaonyesha makundi mbalimbali 10 yanayohusika.
3.           Makundi hayo ni  kama ifuatavyo:-
(i)                  Taasisi zisizokuwa za Kiserikali (20)
(ii)               Taasisi za Kidini (20)
(iii)            Vyama vyote vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu (42);
(iv)             Taasisi za Elimu (20);
(v)                Watu wenye Ulemavu (20);
(vi)             Vyama vya Wafanyakazi (19);
(vii)          Vyama vinavyowakilisha Wafugaji (10);
(viii)       Vyama vinavyowakilisha wavuvi (10);
(ix)             Vyama vya Wakulima (20); na
(x)                Vikundi vya Watu wenye Malengo yanayofanana (20).
4.           Mchakato wa uteuzi ulianza kwa kutoa Tangazo la Mwaliko katika Gazeti la Serikali, Tangazo la Serikali Na 443 la tarehe 13 Desemba, 2013. Tangazo hilo lilitolewa kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza ili kuyaalika makundi yaliyotajwa kisheria kuwasilisha mapendekezo ya majina kwa ajili ya uteuzi katika Bunge laMaalum la Katiba. Aidha, Tangazo hilo la mwaliko lilitangazwa pia katika magazeti mbalimbali yanayosomwa hapa nchini. Pamoja na mambo mengine Tangazo la Mwaliko lilitamka ukomo wa muda wa Taasisi na Makundi kuwasilisha mapendekezo ya majina ya wajumbe kuwa ni tarehe 02/01/2014.
5.           Mapendekezo hayo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar, mapendekezo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
6.           Kufuatia mwaliko huo, taasisi 554 kutoka Tanzania Bara na 178 kutoka Zanzibar ziliwasilisha mapendekezo yao. Mapendekezo hayo yalijumuisha majina 2,762 kwa upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar mapendekezo hayo yalihusisha watu 874. Hivyo basi, taasisi na makundi mbalimbali yalipendekeza jumla ya majina 3,636. Lakini, na kinyume na Sheria, watu 118 walijipendekeza wenyewe na kufanya idadi ya majina yaliyopendekezwa kuwa 3,754.
7.           Mchanganuo wa idadi ya watu walipendekezwa katika makundi mbalimbali ni kama ifuatavyo:
Na.
Kundi/Taasisi
Taasisi zilizoleta mapendekezo
Idadi ya Watu Waliopendekezwa
Idadi ya Wajumbe Wanaotakiwa
Idadi ya Walioteuliwa
Tanzania Bara
Zanzibar
Tanzania Bara
Zanzibar
Tanzania Bara
Zanzibar
1.     
Taasisi zisizokuwa za Kiserikali
246
98
1,203
444
20
13
7
2.     
Taasisi za Kidini
55
17
344
85
20
13
7
3.     
Vyama vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu
21
14
129
69
42
28
14
4.     
Taasisi za Elimu
9
9
84
46
20
13
7
5.     
Makundi ya Walemavu
24
6
97
43
20
13
7
6.     
Vyama vya Wafanyakazi
20
1
89
13
19
13
6
7.     
Vyama Vinavyowakilisha Wafugaji
8
1
43
4
10
7
3
8.     
Vyama vinavyowakilisha Wavuvi
7
3
45
12
10
7
3
9.     
Vyama vya Wakulima
22
8
115
44
20
13
7
10.             
Makundi yenye Malengo Yanayofanana
142
21
613
114
20
14
6
Mapendekezo Binafsi
-
-
118
-
Jumla
672
178
2,880
874
201
134
67
Jumla Kuu
850
3,754


8.           Sheria ya Mabadiliko ya Katiba imeweka masharti ya kuzingatiwa katika uteuzi wa wajumbe 201 wa Bunge la Maalum la Katiba. Masharti hayo ni pamoja na wajumbe wasiopungua theluthi moja wanatakiwa kutoka Zanzibar na theluthi mbili kutoka Tanzania Bara. Kwa sababu hiyo, katika wajumbe 201, wajumbe 67 watatoka Zanzibar na wajumbe 134 watatoka Tanzania Bara. Aidha, mgawanyo wa wajumbe wanawake na wanaume unatakiwa uwe nusu kwa nusu. Pamoja na hayo, wajumbe hao wawakilishe sura ya wananchi wa Tanzania kwa ufuasi wa vyama vya siasa, dini, umri, na maeneo wanayotoka. Katika mazingira haya, zoezi la kupata wajumbe 201 halikuwa rahisi hata kidogo. Mwitikio wa makundi ulikuwa mkubwa sana ikilinganishwa na nafasi zilizopo.
9.           Kama nilivyoeleza hapo awali, mapendekezo kutoka Tanzania Bara yalikuwa 2,880 wakati nafasi za wajumbe ni 134. Kwa upande wa Zanzibar, majina yaliyopendekezwa yalikuwa 874 ikilinganishwa na idadi ya wajumbe 67 wanaotakiwa kuteuliwa. Kwa nyongeza ya maelezo kuhusu uwingi wa mapendekezo, ni kwamba ukichukua taasisi zisizo za kiserikali kwa upande wa Tanzania Bara walipendekezwa watu 1,203, wakati nafasi zilizokuwa zinatakiwa kujazwa ni 13 tu. Kwa upande Zanzibar, taasisi zisizokuwa za kiserikali zilikuwa zimependekeza majina 444 ikilinganishwa na nafasi 7 tu zilizokuwa zinatakiwa kujazwa kutokana na taasisi hizi.
WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA
10.      Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania wakishirikiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpainduzi Zanzibar wamekamilisha uteuzi wa wajumbe 201. Kabla ya kutaja orodha ya wajumbe walioteuliwa, napenda kufafanua mambo yafuatayo:
(a)             Uteuzi umezingatia ushiriki wa watu wa rika zote, yaani vijana, watu wazima na wazee. Kwa ajili hiyo, wajumbe vijana yaani wenye umri wa kati miaka 22-35, ni wajumbe 35. Wajumbe wenye umri wa kati, yaani miaka 36-64, ni 145; na wajumbe wazee, yaani wenye umri wa miaka 65 na kuendelea ni 21.
(b)             Sheria inataka kuwepo na uwiano sawa kwa ajumbe wanawake na wanaume. Jambo hili limezingatiwa ipasavyo, na katika orodha hii wajumbe wanawake ni 100 na wanaume 101. Kwa vile, haiwezekani kuwa na nusu mtu, ndiyo maana idadi ya wajumbe wanaume ni 101.
(c)              Uwakilishi wa vyama vya siasa ambao unahitaji kila chama chenye usajili wa kudumu kiwe na wajumbe wawili umezingatiwa. Kwa kuwa kuna vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu 21, jumla ya wajumbe 42 wamechaguliwa kwa maana ya kuwa wajumbe wawili wameteuliwa kutoka katika kila chama.
Baada ya maelezo hayo ya utangulizi, ifuatayo ndiyo orodha ya wajumbe 201 wa Bunge Maalum la Katiba waliobahatika kuteuliwa:

TAASISI ZISIZOKUWA ZA KISERIKALI- (WAJUMBE 20)

TANZANIA BARA (13)

1.     Magdalena Rwebangira
2.        Kingunge Ngombale Mwiru
3.     Asha D. Mtwangi
4.        Maria Sarungi Tsehai
5.     Paul Kimiti
6.        Valerie N. Msoka
7.     Fortunate Moses Kabeja
8.        Sixtus Raphael Mapunda
9.     Elizabeth Maro Minde
10.   Happiness Samson Sengi
11. Evod Herman Mmanda
12.   Godfrey Simbeye
13. Mary Paul Daffa
TANZANIA ZANZIBAR (7)
1.     Idrissa Kitwana Mustafa
2.          Siti Abbas Ali
3.     Abdalla Abass Omar
4.          Salama Aboud Talib
5.     Juma Bakari Alawi
6.          Salma Hamoud Said
7.     Adila Hilali Vuai
TAASISI ZA KIDINI- (WAJUMBE 20)
TANZANIA BARA (13)
1.   Tamrina Manzi
2.        Olive Damian Luwena
3.   Shamim Khan
4.        Mchg. Ernest Kadiva
5.   Sheikh Hamid Masoud Jongo
6.        Askofu Mkuu (Mstaafu) Donald Leo Mtetemela
7.   Magdalena Songora
8.        Hamisi Ally Togwa
9.   Askofu Amos J. Muhagachi
10.   Easter Msambazi
11.                                                           Mussa Yusuf Kundecha
12.   Respa Adam Miguma
13.                                                           Prof. Costa Ricky Mahalu
TANZANIA ZANZIBAR (7)
1.     Sheikh Thabit Nouman Jongo
2.     Suzana Peter Kunambi
3.     Sheikh Nassoro Mohammed Ibrahimu
4.     Fatma Mohammed Hassan
5.     Louis Majaliwa
6.     Yasmin Yusufali E. H alloo
7.     Thuwein Issa Thuwein


VYAMA VYOTE VYA SIASA
VYENYE USAJILI WA KUDUMU – (WAJUMBE 42)
TANZANIA BARA (28)
1.        Hashim Rungwe Spunda
2.           Thomas Magnus Mgoli
3.        Rashid Hashim Mtuta
4.           Shamsa Mwangunga
5.        Yusuf  S. Manyanga
6.           Christopher Mtikila
7.        Bertha Ng’angompata
8.           Suzan Marwa
9.        Dominick Abraham Lyamchai
10.      Mbwana Salum Kibanda
11.   Peter Kuga Mziray
12.      Isaac Manjoba Cheyo
13.   Dr. Emmanuel John Makaidi
14.      Prof. Ibrahim Haruna Lipumba
15.   Modesta Kizito Ponera
16.      Prof. Abdallah Safari
17.   Salumu Seleman Ally
18.      James Kabalo Mapalala
19.   Mary Oswald Mpangala
20.      Mwaka Lameck Mgimwa
21.   Nancy  S. Mrikaria
22.      Nakazael Lukio Tenga
23.   Fahmi Nasoro Dovutwa
24.      Costantine  Benjamini Akitanda
25.   Mary Moses Daudi
26.      Magdalena Likwina
27.   John Dustan Lifa Chipaka
28.      Rashid Mohamed Ligania Rai
TANZANIA ZANZIBAR (14)
1.     Ally Omar Juma
2.     Vuai Ali Vuai
3.     Mwanaidi Othman Twahir
4.     Jamila Abeid Saleh
5.     Mwanamrisho Juma Ahmed
6.     Juma Hamis Faki
7.     Tatu Mabrouk Haji
8.     Fat –Hiya Zahran Salum
9.     Hussein Juma
10.     Zeudi Mvano Abdullahi
11.     Juma Ally Khatibu
12.     Haji Ambar Khamis
13.     Khadija Abdallah Ahmed
14.     Rashid Yussuf Mchenga


TAASISI ZA ELIMU- (WAJUMBE 20)
TANZANIA BARA
1.     Dr. Suzan Kolimba
2.     Prof. Esther Daniel Mwaikambo
3.     Dr. Natujwa Mvungi
4.     Prof. Romuald Haule
5.     Dr. Domitila A.R. Bashemera
6.     Dr. Jasmine Bendantunguka Tiisekwa
7.     Prof. Bernadeta Kilian
8.     Teddy Ladislaus Patrick
9.     Dr. Francis Michael
10.    Prof. Remmy J. Assey
11.               Dr. Tulia Ackson
12.               Dr. Ave Maria Emilius Semakafu
13.               Hamza Mustafa Njozi
TANZANIA ZANZIBAR (7)
1.     Makame Omar Makame
2.     Fatma Hamid Saleh
3.     Dr. Aley Soud Nassor
4.     Layla Ali Salum
5.     Dkt. Mwinyi Talib Haji
6.     Zeyana Mohamed Haji
7.     Ali Ahmed Uki
WATU WENYE ULEMAVU-(WAJUMBE 20)
TANZANIA BARA (13)
1.        Zuhura Musa Lusonge
2.     Frederick Msigala
3.        Amon Anastaz Mpanju
4.     Bure Zahran
5.        Edith Aron Dosha
6.     Vincent Venance Mzena
7.        Shida Salum Mohamed
8.     Dr. Henry Mwizengwa Nyamubi.
9.        Elias Msiba Masamaki
10.                   Faustina Jonathan Urassa
11.   Doroth Stephano Malelela
12.                   John Josephat Ndumbaro
13.   Ernest Njama Kimaya
TANZANIA ZANZIBAR (7)
1.     Haidar Hashim Madeweyya
2.     Alli Omar Makame
3.     Adil Mohammed Ali
4.     Mwandawa Khamis Mohammed
5.     Salim Abdalla Salim
6.     Salma Haji Saadat
7.     Mwantatu Mbarak Khamis
VYAMA VYA WAFANYAKAZI-(WAJUMBE 19)
TANZANIA BARA (13)
1.     Honorata Chitanda
2.     Dr. Angelika Semike
3.     Ezekiah Tom Oluoch
4.     Adelgunda Michael Mgaya
5.     Dotto M. Biteko
6.     Mary Gaspar Makondo
7.     Halfani Shabani Muhogo
8.     Yusufu Omari Singo
9.     Joyce Mwasha
10.                   Amina Mweta
11.                   Mbaraka Hussein Igangula
12.                   Aina Shadrack Massawe
13.                   Lucas Charles Malunde
TANZANIA ZANZIBAR (6)
1.   Khamis Mwinyi Mohamed
2. Jina Hassan Silima
3.   Makame Launi Makame
4. Asmahany Juma Ali
5.   Mwatoum Khamis Othman
6. Rihi Haji Ali
VYAMA VINAVYOWAKILISHAWAFUGAJI-(WAJUMBE 10)
TANZANIA BARA (7)
1.     William Tate Olenasha
2.     Makeresia Pawa
3.     Mabagda Gesura Mwataghu
4.     Doreen Maro
5.     Magret Nyaga
6.     Hamis Mnondwa
7.     Ester Milimba Juma
TANZANIA ZANZIBAR (3)
1.     Said Abdalla Bakari
2.     Mashavu Yahya
3.     Zubeir Sufiani Mkanga
VYAMA VINAVYOWAKILISHAWAVUVI –(WAJUMBE 10)
TANZANIA BARA (7)
1.     Hawa A. Mchafu
2.     Rebecca Masato
3.     Thomas Juma Minyaro
4.     Timtoza Bagambise
5.     Tedy Malulu
6.     Rebecca Bugingo
7.     Omary S. Husseni
TANZANIA ZANZIBAR (3)
1.     Waziri Rajab
2.     Issa Ameir Suleiman
3.     Mohamed Abdallah Ahmed


VYAMA VYAWAKULIMA-(WAJUMBE 20)
TANZANIA BARA (13)
1.     Agatha  Harun Senyagwa
2.     Veronica Sophu
3.     Shaban Suleman Muyombo
4.     Catherine Gabriel Sisuti
5.     Hamisi Hassani Dambaya
6.     Suzy Samson Laizer
7.     Dr. Maselle Zingura Maziku
8.     Abdallah Mashausi
9.     Hadijah Milawo Kondo
10.                                                   Rehema Madusa
11.                  Reuben R. Matango
12.                                                   Happy Suma
13.                  Zainab Bakari Dihenga
TANZANIA ZANZIBAR (7)
1.     Saleh Moh’d Saleh
2.     Biubwa Yahya Othman
3.     Khamis Mohammed Salum
4.     Khadija Nassor Abdi
5.     Fatma Haji Khamis
6.     Asha Makungu Othman
7.     Asya Filfil Thani
WATU WENYE MALENGO YANAYOFANANA – (WAJUMBE 20)
TANZANIA BARA (14)
1.        Dr. Christina Mnzava
2.     Paulo Christian Makonda
3.        Jesca Msambatavangu
4.     Julius Mtatiro
5.        Katherin Saruni
6.     Abdallah Majura Bulembo
7.        Hemedi Abdallah Panzi
8.     Dr. Zainab Amir Gama
9.        Hassan Mohamed Wakasuvi
10.               Paulynus Raymond Mtendah
11.   Almasi Athuman Maige
12.               Pamela Simon Massay
13.   Kajubi Diocres Mukajangwa
14.               Kadari Singo
TANZANIA ZANZIBAR (6)
1.     Yussuf Omar Chunda
2.     Fatma Mussa Juma
3.     Prof. Abdul Sheriff
4.     Amina Abdulkadir Ali
5.     Shaka Hamdu Shaka
6.     Rehema Said Shamte
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment