Na,
Doris Meghji Jumamosi Januari 31,2015
Singida
– Manispaa
Zaidi
ya shlingi bilioni tatu zinahitajika katika halmashauri ya manispaa ya singida
ikiwa ni ombi maalum la bajeti ya manispaa katika kuzikabiri changamoto mbali
mbali zinazoikumba manispaa hiyo kwa
sasa.
Madiwani wa manispaa wakimsikiliza Mkurugenzi wa manispaa ya Singida (picha na Doris Meghji) |
Akiwasilisha
ombi hilo maalum kwa niaba ya mkurugenzi wa manispaa mbele ya kikao cha baraza la madiniwani wa manispaa ya singida
Mchumi wa manispaa hiyo Nurfus Ndee
amesema ombi hilo limekuja kwenye bajeti hiyo kutokakana na changamoto mbali
mbali zinazikabili manispaa ya Singida zikiwemo changamoto za kuongezeka kwa
uhitaji wa huduama za kijamii ,uhitaji wa uboreshaji wa wa miundo mbinu mbali
mbali zikiwemo barabara, masoko na kuongezeka shughuli za kiutawala kwa
manispaa hiyo
Baadhi ya madiwani wa manispaa ya singida wakimsikiliza mchumi wa manispaa ya singida wakati akiwakilisha ombi hilo maalum kwenye kikao cha baraza la manispaa ya Singida(picha na Doris Meghji) |
Aidha
ametaja jumla ya shilingi billion 3,059 821,150/= zinahitajika kwa ajili ya
kuzikabili changamoto hizo ambapo
shilingi bilioni 2,700,000 zitatumika katika ujenzi wa jengo jipya la utawala la halmashauri ya manispaa ya singida
na shilingi milioni 359 821 150,000/= ni kwa ajili ya ukamilishaji wa mabaoma
ya shule za msingi ndani ya manispaa hiyo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Shekhe Mahami akiongea neno katika baraza la madiwani wa manispaa ya Singida katika kikao cha baraza la bajeti la manispaa hiyo( picha na Doris meghji) |
Hata
hivyo dira ya manispaa ya singida inaonyesha kuwa ifikapo mwaka 2015 itakuwa
manispaa yenye kutoa huduma bora kwa wananchi wa manispaa hiyo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment