Na, Doris Meghji Ijumaa
Januari 30,2015
Singida – Manispaa
Kushoto ni Mkurugenzi wa manispaa a Singida Joseph Mchina,Katikati ni Mstahiki Meya wa manispaa ya Singida Shekhe Mahame kulia ni Naibu meya wa manispaa hii (picha na Doris Meghji) |
Zaidi ya shilingi bilioni 32.25
zinatarajia kutumika katika halmashauri ya manispaa ya singida ikiwa ni makisio
ya mpango na bajeti ya mwaka wa fedha 2015- 2016 mkoani singida
Mchumi wa manispaa ya Singida Nurfus Azizi Ndee akiwakilisha makisio ya mpango na bajeti ya mwaka 2015-2016 katika baraza la madiwani( picha na Doris meghji) |
Akisoma
kwa niaba ya mkurugenzi wa manspaa ya Singida makisio ya mpango na
bajeti ya mwaka fedha 2015/2016 mbele ya kikao cha baraza la madiwani wa
manispaa ya Singida mchumi wa Manispaa
hiyo Nurfus Azizi Ndee amesema jumla ya shilingi bilioni thelathini na mbili,
milioni mia mbili hamsini na saba,laki tatu sabini na nne elfu
mia nne sabini na mbili zinatarajiwa kutumika katika kipindi hicho cha
mwaka wa fedha.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida akifungua kikao cha baraza la madiniwani katika kupitisha makisiao na mpango wa bajeti ya manispaa hiyo 2015- 2016 (Picha na Doris Meghji) |
Aidha ametaja jumla ya shilingi
20,883,349,248/= kwa ajili ya mishahara ya na matumizi mengine ya manispaa hiyo,shilingi bilioni 1,780,450,000 zikiwa ni fedha za matumizi
ya kawaida, fedha za rukuzu ya miradi ya
maendeleo toka serikali kuu ni shilingi
bilioni 6,403,326,223.62/= huku shilingi bilioni 2,986,364,000/= ni mapato ya
ndani ya manispaa ya singida katika kipindi hicho cha mwaka wa fedha.
baadhi ya madiwani wa manispaa ya singida wakisikiliza taarifa ya makisio ya bajeti ya manispaa yao (picha na Doris Meghji) |
Kwa mujibu wa mchumi Ndee amezitaja
changamoto mbali mbali zinazoikabili manispaa hio kuwa ni pamoja na kuongezeka
kwa uhitaji wa huduma za kijamii,uhitaji wa maafisa ugani,uhitaji na uboreshaji
wa miundombinu mbali mbali hasa za
barabara,masoko na shughuli za kuitawala hii ni kutokana na changamoto ya
ukuaji haraka wa manispaa ya Singida.
Mh. Yagi Kiaratu diwani wa viti maalum ccm akiunga mkono makisio ya mpango na bajeti ya manispaa hiyo kwa niaba ya madiwani wa manispaa ya singida (picha na Doris Meghji0 |
Mwisho
No comments:
Post a Comment