Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Mh.Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Awaabisha leo Jijini Dar-es salaam jumla ya mawaziri nane wa baraza la mawaziri na manaibu waziri watano kushika nafasi hizo
katika wizara hizo.
Kuapishwa kwa mawaziri hao na manaibu
waziri ni baada ya kujiuzulu kwa mawaziri wawili wa wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya
makazi Prof.Anna Kajumulo Tibaijuka na pamoja
na wizara ya Nishati na madini Prof.
Sosepeter Muhongo kufuatia sakata la Akaunti ya Tegeta Eskro
Mabadiliko ya baraza hilo la Mawaziri
limetangazwa leo na Katibu mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue mbele ya waandishi
wa habari leo jijini Dar-es- salaam.
Na mawaziri walioteuliwa na kuapishwa leo kuwa ni
1.
George Simbachawene – Waziri
wa Nishati na Madini
2.
Mary Nagu – Waziri wa Nchi
mawasiliano na uratibu
3.
Christopher Chiza Waziri
uwezeshaji na uwekezaji
4.
Harrison Mwakembe –
Ushirikiano wa Afrika Mashariki
5.
William Lukuvu – waziri ya
Ardhi numba na maendeleo ya Makazi
6.
Steven Wassira – Waziri wa
Kilimo chakula na ushirika
7.
Samwel Sitta - Waziri wa Uchukuzi
8.
Jenista Muhagama – Sera na
uratibu wa Bunge
Huku manaibu waziri
walioteuliwa na kuapishwa leo kuwa ni
1.
Stephen Masele – Naibu waziri
ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira
2.
Anjela – Jasmini Kairuki
Naibu waziri wa Ardhi
3.
Ummy Ally Mwalimu – Naibu waziri
Katiba na Sheria
4.
Anna Kilango Malecela –
Naibu waziri wa Elimu
5.
Charles Mwijage – Naibu waziri
wa Nishati na Madini.
Kati
ya manaibu hao manaibu waziri wapya ni
Anna
Kilango Malecela – Wa elimu
na
Charles
Mwijage wa Nishati na Madini.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment